Rais Samia unapotoshwa sana, Magufuli alikuwa sahihi sehemu nyingi japokuwa ana makosa ya kibinadamu

Rais Samia unapotoshwa sana, Magufuli alikuwa sahihi sehemu nyingi japokuwa ana makosa ya kibinadamu

Huhitaji umri na udadisi wowote hapa. Tundu Antipas Lissu ndio ushahidi unaoishi wa vitendo viovu vya Magufuli na watu wake. Hivi unawezaje wewe kuwa na akili timamu kutetea yanayoendelea nchini?

Umehama sasa kwenye Swali uliloulizwa, hajazungumzia kutetea yanayoendelea unamlisha maneno, Magu hakuanzisha haya Wala kwa Samia hayatakua yamwisho. Mfumo ni zaidi ya Rais.
Kama unautimamu kamili, nikuulize kwani kina Dr Ulimboka au Dr Mvungi walikutana na uvamizi kipindi Gani?
 
Unauliza maswali magumu kwa kichwa kizito.
 
Umehama sasa kwenye Swali uliloulizwa, hajazungumzia kutetea yanayoendelea unamlisha maneno, Magu hakuanzisha haya Wala kwa Samia hayatakua yamwisho. Mfumo ni zaidi ya Rais.
Kama unautimamu kamili, nikuulize kwani kina Dr Ulimboka au Dr Mvungi walikutana na uvamizi kipindi Gani?
Mvungi na Ulimboka waliuawa kwa mizozo na watu binafsi na sio na serikali kama wakati wa Magufuli na dada yake Samia. Tunaona kabisa Jeshi la Polisi na TISS wakishiriki kwenye mauaji ya kisiasa. Inasikitisha sana na haya yote Magu aliyafanya kwa kiwango kikubwa kuliko awamu nyingine yoyote ile. Lissu anajua vizuri ushenzi huu.
 
Magufuli tunamsifu kwa uweledi wake wa kuibadili hii nchi.
Toka nianze kujielewa sijai ona rais ambaye alikua na uthubutu kama Mafuguli.
Ndio uthubuti hata wa kuuwa wapinzani na demokrasi nzima, alifanya kweli kweli hayo na la ajabu bado ana washabiki wengi. Nadhani hawa mashabiki wake ni watu wasio na mioyo ya kibinadamu kabisa au ni wajinga kupindukia.
 
Mvungi na Ulimboka waliuawa kwa mizozo na watu binafsi na sio na serikali kama wakati wa Magufuli na dada yake Samia. Tunaona kabisa Jeshi la Polisi na TISS wakishiriki kwenye mauaji ya kisiasa. Inasikitisha sana na haya yote Magu aliyafanya kwa kiwango kikubwa kuliko awamu nyingine yoyote ile. Lissu anajua vizuri ushenzi huu
Kumbe Ulimboka aliishauawa?😥😥
Eti mizozo ya watu binafsi😂😂
Ngoja nikuache na akili zako fazili.
 
Kumbe Ulimboka aliishauawa?😥😥
Eti mizozo ya watu binafsi😂😂
Ngoja nikuache na akili zako fazili.
Nafikiri umepata pointi kafikirie vizuri acha kushabikia wauaji.
 
Nafikiri umepata pointi kafikirie vizuri acha kushabikia wauaji.
Point ipi? Umemuua Ulimboka tayari😂 . Dr Mvungi umemjulia kwa kumsoma mtandaoni? Hakika lile swali la Kujua Umri wako Lilikua la msingi sana. Jioni njema
 
Una uhakika control namba hazipo? Wizi ulidhibitiwa kipindi Cha Magu? Una uhakika?

Kila mtu anakuja na mfumo wake kama upi,weka uthibitisho wa haya madai Yako.

Miaka yote Madini Huwa yanasafirishwa na Serikali? Mbona unaropoka tuu bila utaratibu? Ni lini upotoshaji wa Madini uliwahi isha?

Mwisho pamoja na hayo unayodai wewe kwamba Kuna shida,huoni kwamba Mapato ya Madini yameongezeka mara 2 na sekta ya Madini Sasa inachangia 10% ya GDP na inaongoza Kwa forex?

Unahisi Kipimo chako na madai Yako Yako sahihi kiasi gani ilihali namba zinaongea +ve?
Amesema Control Number imesitishwa?
Unadandia hoja kizembe sana
 
Huhitaji umri na udadisi wowote hapa. Tundu Antipas Lissu ndio ushahidi unaoishi wa vitendo viovu vya Magufuli na watu wake. Hivi unawezaje wewe kuwa na akili timamu kutetea yanayoendelea nchini?
Nimesemaje, kamuulize Ulimboka.

Kuna mwingine akiitwa Wangwe, yeye alifariki kabisa na tetesi zikazagaa kibao.

Huwezi kuelewa ukiendelea kufikiri kwa tumbo!
 
Watanzania acheni ujinga wa kutetea wanasiasa na wakati huo huo mna hali ngumu kimaisha, ni ujinga mkubwa kwa kijana kutetea uwepo wa miaka 65 wa CCM!
 
Back
Top Bottom