PostGE2025 Rais Samia unatupoteza muda na kufuja pesa za walipa kodi, tume ya haki Jinai ya Jaji Chande ilimaliza kila kitu

PostGE2025 Rais Samia unatupoteza muda na kufuja pesa za walipa kodi, tume ya haki Jinai ya Jaji Chande ilimaliza kila kitu

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Heparin

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2021
Posts
450
Reaction score
3,368
Tume ya Haki Jinai iliyoongozwa na Jaji Othman Chande iliyozunguka nchi nzima mwaka 2023 ilimaliza kila kitu.

Ilishauri mambo mazuri sana ambayo kama yangefanyiwa kazi, utekaji, wasiojulikana, changamoto za mahakama zetu pamoja na haki zingine za raia zingekuwa hazibagazwi na kubanagwa kama ilivyo sasa.

Mathalani, tume hii ilibaini uwepo wa mahabusu hewa zinazotesa na kuhifadhi watu, walibaini matumizi makubwa ya silaha za kivita kwa raia wasio na hatia, rushwa, ubambikiaji kesi na unyanyasaji wanaofanya polisi kwa raia.

Ripoti ilichunguza pia taasisi ya Mahakama na TAKUKURU na ilishauri nini kifanyike kwa kila taasisi.

Mfano kwa Polisi, ilishauri Jeshi hili lifumuliwe upya kimuundo na kisheria maana lina mentality za kikoloni, liwe National Police Service pia mafunzo kwenye syllabus yao yabadilishwe, wanafundishwa vitu visivyoendana na uhalisia wa dunia ya sasa, wao ni nguvu tu na kutisha raia.

Kwa maoni yangu, ilikosa tu kipengele cha Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi ambazo wote tunajua vinahitajika kwa sasa.

1000512249.jpg


Pia soma Rais Samia aunda Tume Huru ya Uchunguzi wa matukio yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi 2025
 
Back
Top Bottom