Rais Samia, anatakiwa kutambua kuwa nje ya Serikali (TISS), kuna supper intelligence ambayo TISS haipo.
Huku nje ya Serikali, kuna wataalam wa uchumi ambao kwenye Wizara ya mipango na uchumi, hawapo.
Huko nje ya Jeshi la Polisi, kuna watu wanajua nadharia ya usalama ambayo ndani ya Jeshi la Polisi, haipo.
Huku nje ya Serikali, mahakama na Bunge, kuna watu wanajua sheria na katiba kwa kiwango ambacho kwenye vyombo nilivyovitaja hawapo.
Huku nje ya Serikali, kuna watu ambao wamenyoka, wanaaminika, na wana uwezo wa kuzungumza na kiongozi yeyote Duniani awe wa nchi au taasisi za kimataifa, kwa urahisi na kwa ufanisi kuliko yeyote ambaye yupo Serikalini.
Unatakiwa ufahamu, na uichukulie hii ni sauti ya mtu aliaye nyikani, unaweza kupuuza, kama ilivyo kawaida;
Maamuzi yalifikiwa nini kifanyike dhidi ya awamu ya 5 kutokana na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na demokrasia. Maamuzi yale yangeanza kutekelezwa nusu ya pili ya mwaka 2021. Lakini Mungu muweza wa yote alikuwa na yake yasiyoweza kuhojiwa na mwanadamu. Yakatokea yaliyotokea.
Maamuzi yale hayakufutwa, lakini kukajengeka nadharia 2 zinazobishaniwa:
1) Mabadiliko ya kiongozi mkuu hayatabadili chochote kwa sababu udikteta uliopo Tanzania umejengeka kwenye mfumo, na kiongozi mkuu ana nafasi ndogo ya kubadilisha mfumo wa kidikteta na kusimika mfumo wa uongozi wa kistaarabu.
2) Rais ana madaraka makubwa sana, anaweza kufanya chochote. Kama ana dhamira ya kuondokana na mfumo wa kidikteta, anaweza.
Maamuzi:
1) Balozi zianishe mabadiliko, kama yapo, kwa kufuatilia na kuzungumza na taasisi zinazopinga udikteta, vyama vya upinzani, na inapowezekana kushuhudia matukio ya ukiukwaji wa haki na demokrasia.
2) Kuanisha ulinganifu wa taarifa zilizokusanywa
3) Kufuta maamuzi yaliyofanywa dhidi ya awamu ya 5 kama kuna mabadiliko chanya
4) Kutekeleza maamuzi yaliyofanywa dhidi ya awamu ya 5 kama hakuna mabadiliko ya msingi. Mabadiliko ya msingi ni lazima yahusishe ujenzi wa taasisi huru za kulinda, kukuza na kustawisha demokrasia, haki na uhuru wa watu.
Kosa Kubwa, na Urahisi Uliotengenezwa:
1) Siku zako za mwanzo kabisa zilikuwa ni muhimu sana ili kupeleka ujumbe, kama awamu ya sasa ni kama iliyopita au ni tofauti. Lakini awamu ya 6 ikachukua uamuzi wa kuwa si moto, si baridi, mistake number 1
2) Wakati balozi zikitafuta uthibitisho usio na shaka, awamu ya 6 ikawarahisishia kazi kwa kumbambikia mtu kesi ya ugaidi, kukamata na kuswekwa watu ndani ovyo, yaani kwa kosa la kutaka kuhudhuria kongamano la ndani. Mistake number 2
3) Kukumbatia uovu. Kuna watu walifanya uovu wa kupindukia. Badala ya kuwakamata na kuwafikisha mahakamani, walibadilishwa tu nafasi, na wengine kuachwa wakirandaranda huru. Mmoja tu, pekee ndiye alifikishwa mahakamani. Matukio makubwa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu yakaachwa bila uchunguzi. Mistake number 3
Mambo ni mengi, muda ni kidogo. Kalamu imeanza kutick utekelezaji wa maamuzi yale yaliyokuwa dhidi ya awamu ya 5.