Jamal Akbar
JF-Expert Member
- Oct 9, 2014
- 413
- 471
Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Wakulima (Nanenane) yaliyofanyika Jijini Mbeya, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka vijana kujishughulisha na kilimo kwani Serikali imetenga mashamba na imeshatafuta masoko kwa ajili ya mazao yatakayozalishwa.
"Vijana njooni kwenye sekta ya kilimo, tumejipanga kuwapatia mashamba na mashamba hayo yatakuwa na hati zitakazotoka kwa majina yenu wenyewe aidha kwa makundi au kwa mtu mmoja mmoja. Tumejipanga kuwaunganisha na mabenki ili yawapatie mikopo laini (Mikopo ya riba nafuu), tumekaa na mabenki wako tayari. Niwaombe sana vijana ingieni kwenye kilimo." ameeleza Rais Samia
Rais Saima ameeleza kuwa Serikali imejipanga vyema kutafuta masoko na kwamba kila kitakachozalishwa tayari kina soko lake la uhakika.
Amefafanua kuwa ziara anazozifanya nje ya nchi anakwenda kutafuta masoko ya bidhaa zitakazozalishwa na tayari kuna masoko ambayo yanasubiri bidhaa/mazao kutoka Tanzania.