LGE2024 Rais Samia, vijana tunataka tuwe viongozi, tunaomba sheria ya mgombea binafsi ili tupate nafasi kwenye vyama vya siasa, ni ngumu vijana kupenya

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

cutelove

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2017
Posts
3,448
Reaction score
7,972
Tunapoelekea uchaguzi wa 2025 nakuomba mama Samia na Serikali yako itunge sheria na kubadili katiba ya kuruhusu mgombea binafsi ili vijana tusio na maokoto tupate nafasi ya kugombea udiwani, ubunge na Urais.

Kwa hali ilivyo kwenye vyama vya siasa ni ngumu sana kupenya kwa sababu ya wajumbe wanampitisha wale wenye pesa kuwa mgombea wao ni bora tukawa na mgombea binafsi naamini vijana wengi tutakuwa viongozi kupitia mgombea binafsi na wanawake wengi tutakuwa viongozi kupitia mgombea binafsi

Nawaomba vijana na wanawake tupaze sauti tunataka mgombea binafsi ili vijana na wanawake tuwe viongozi kwa wingi, wazee wenye pesa wameteka vyama vya siasa.
 
Una hoja nzuri sana ila ujana ni very relative term and quite irrelevant kwenye hoja yako.

Mgombea Binafsi👍

Hoja za umri na sura na jinsia haina issue kabisa kwenye siasa za dunia ya Sasa...

Mgombea Binafsi ni swala la kikatiba, CCM wanaogopa sana betrayal....

Unawezaje kum controll mgombea Binafsi?

Kwa mazingira ya siasa zetu hilo jambo ni gumu karibu na kutowezekana kwa Sasa...

It's out of bound and scope kwa huyo unayemuomba... Unfortunately.
 
Likikubaliwa kiburi ya vyama vya siasa itakuwa mwisho kuwaringia wagombea na kukusanya michango na ada.
 
Tunapoelekea uchaguzi wa 2025 nakuomba mama Samia na Serikali yako itunge sheria na kubadili katiba ya kuruhusu mgombea binafsi ili vijana tusio na maokoto tupate nafasi ya kugombea udiwani, ubunge na Urais.

Kwa hali ilivyo kwenye vyama vya siasa ni ngumu sana kupenya kwa sababu ya wajumbe wanampitisha wale wenye pesa kuwa mgombea wao ni bora tukawa na mgombea binafsi naamini vijana wengi tutakuwa viongozi kupitia mgombea binafsi na wanawake wengi tutakuwa viongozi kupitia mgombea binafsi

Nawaomba vijana na wanawake tupaze sauti tunataka mgombea binafsi ili vijana na wanawake tuwe viongozi kwa wingi, wazee wenye pesa wameteka vyama vya siasa.
mbele ya ccm huo mfupa ni mgumu kuliko ugumu wenyewe na ndo uliompelekea Mchungaji machachari Mtikila kaburini
 
Una hoja!. Ningetamani vijana 1000 elfu moja wenye mawazo kama hayo kujitokeza kwa nguvu kudai nafasi za ajira na uongozi kuliko kukumbatia uchawa.

Vijana mnatakiwa kuwaondoa kwa nguvu wazee wa miaka zaidi ya sitini waliojazana kwenye nafasi nyeti huku vijana wakiishia kuridhika na mgao wa pesa na vijizawadi.

Nawashauri vijana kuanzia mwaka huu, wajitokeze kugombea nafasi za uongozi kwenye ngazi ya Serikali za mitaa, huko kuna viongozi wa mitaa na vitongoji wanaotumia akili ya kuzaliwa kuongoza badala ya elimu ya darasani. Hawa ndio wanaotumika kama pipi na chama tawala kubaki madarakani.
 
Vijana huwa wanajitokeza kwa wingi shida ipo kwenye vyama vya siasa,kijana kupitishwa ni ngumu sana labda awe na historia ya kifamilia njia rahisi kijana kugombea ni mgombea binafsi
 
Katiba sio takwa la sa100 ni takwa la wananchi na Kwa vile vijana wengi wameridhika na uchawa acha tuongozwe na vikongwe Sasa.
 
Kwenye hili suala la kuwa na mgombea binafsi, hata vyama vya upinzani huwa vinaungana na CCM kuhakikisha katiba iwe ya zamani au mpya, hairuhusu jambo hilo.

Wakisimama majukwaani utawasikia wanasema, kwa mfano, hakuna mtu aliye mkubwa kuliko chadema au CUF nk, hapo ni tayari wametofautiana kimtazamo na mwanachama mmoja.

Ni waumini sana wa vyama na wanavitumia hivyo kuwatishia wanachama walio na uongozi, mfano wabunge au madiwani, kufanya yale ambayo chaka kinataka na sio yale ambayo wananchi waliomchagua wanataka.
 
Tupaze sauti watuelewe
Jamii ndiyo inaweza kwa maana washika tonge wameamua kujizima data, kuahirisha kufikiri kizalendo, (unyumbu wa kisiasa), unyumbu wa kisiasa ni tabia ya waliopewa dhamana kuahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kujipendekeza ama kulitumikia kundi fulani kwa masilahi binafsi na uoga kwa viongozi wao bila utii, (unafiki)
 
Tunapoelekea uchaguzi wa 2025 nakuomba mama Samia na Serikali yako itunge sheria na kubadili katiba ya kuruhusu mgombea binafsi ili vijana tusio na maokoto tupate nafasi ya kugombea udiwani, ubunge na Urais.

Kwa hali ilivyo kwenye vyama vya siasa ni ngumu sana kupenya kwa sababu ya wajumbe wanampitisha wale wenye pesa kuwa mgombea wao ni bora tukawa na mgombea binafsi naamini vijana wengi tutakuwa viongozi kupitia mgombea binafsi na wanawake wengi tutakuwa viongozi kupitia mgombea binafsi

Nawaomba vijana na wanawake tupaze sauti tunataka mgombea binafsi ili vijana na wanawake tuwe viongozi kwa wingi, wazee wenye pesa wameteka vyama vya siasa.
Hiyo sheria ya viti maalumu iwalenge Vijana na wanawake tuu.

Naunga mkono hoja ila sio Kwa level ya Urais.
 
Tunapoelekea uchaguzi wa 2025 nakuomba mama Samia na Serikali yako itunge sheria na kubadili katiba ya kuruhusu mgombea binafsi ili vijana tusio na maokoto tupate nafasi ya kugombea udiwani, ubunge na Urais.

Kwa hali ilivyo kwenye vyama vya siasa ni ngumu sana kupenya kwa sababu ya wajumbe wanampitisha wale wenye pesa kuwa mgombea wao ni bora tukawa na mgombea binafsi naamini vijana wengi tutakuwa viongozi kupitia mgombea binafsi na wanawake wengi tutakuwa viongozi kupitia mgombea binafsi

Nawaomba vijana na wanawake tupaze sauti tunataka mgombea binafsi ili vijana na wanawake tuwe viongozi kwa wingi, wazee wenye pesa wameteka vyama vya siasa.
Duh!

Wewe ume-'feli' hata kabla ya kuanza! Eti "Unaomba"", tena unaomba mtu ambaye ananogewa sana na hali iliyopo?

Huu ujana wa siku hizi umekuwa na walakini nyingi sana.
 
Back
Top Bottom