Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea kuonesha dhamira yake ya dhati ya kuboresha maisha ya vijana kwa kutaka kuongezwa kwa uwekezaji katika ujenzi wa nyumba za bei nafuu.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995, toleo la 2023, Rais Samia amesema vijana wengi wanakumbana na changamoto za makazi, hasa wale wanaoanza maisha baada ya kumaliza masomo na kupata ajira mbali na nyumbani kwao.
Ameeleza kuwa vijana wengi wanaishi kwenye nyumba za kupanga vyumba vidogo ambako wanakosa faragha na utulivu, jambo linaloweza kuathiri ustawi wao na utendaji kazi.
"Tunayemlenga hapa ni kijana ambaye leo anaanza maisha. Vijana wanaoishi kwenye nyumba za kupanga chumba kimoja... Na vijana wetu siku hizi wana mambo chungu nzima lakini wakipita hivi shangazi anamtazama kwa huku, akipita hivi huyu mwingine anamtazama kwa kule, mara watu wako nje wanangoja huyu kijana kapita na nani, anatoka saa ngapi... eeh!!" alisema Rais kwa uchangamfu, akieleza hali halisi wanayopitia vijana.
Rais Samia amesisitiza kuwa kuna haja ya kuwa na mpango wa makazi maalum kwa vijana wanaoanza maisha, ili wanapohamia mikoa mingine kwa ajili ya kazi, wakute mazingira bora yanayowawezesha kuishi kwa amani na utulivu.
"Ili kumpa raha afanye kazi yake vizuri, ni vema kule anakokwenda akute kuna nyumba inamsubiri. Akifika aambiwe nyumba yako hii hapa, lipa kodi kwa gharama nafuu," alieleza kwa msisitizo.