Rais Samia: Viwango vya Fidia kwa wanaoathiriwa na uvamizi wa Wanyama viangaliwe

Rais Samia: Viwango vya Fidia kwa wanaoathiriwa na uvamizi wa Wanyama viangaliwe

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Rais Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Utalii aone uwezekano wa kupitia Kanuni za Fidia kwa wanaothiriwa na Wanyama kuvamia mashamba, wakati huohuo amesisitiza Serikali inaendelea kutafuta mbinu mbalimbali za kuwazuia Wanyama kufanya uharibifu huo.

Ameyasema hayo leo Februari 24, 2025 wakati akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Lushoto

Februari 11, 2025, Mdau wa JamiiForums.com alishauri viwango vya fidia hizo vipitiwe kwa madai haviendani na uharibifu, akitoa mfano Wakazi wa Ngara waliovamiwa na Tembo wa Hifadhi ya Burigi kuwa hawakusaidiwa na Sheria ya Wanyamapori, bali iliwaumiza zaidi.

Pia soma ~ Serikali ingilieni kati Fidia ya Uharibifu wa Mazao yaliyoharibiwa na Tembo Wilayani Ngara - Kagera: Sheria ya Wanyamapori inakandamiza Wakulima
 
Back
Top Bottom