Consigliere
Platinum Member
- Sep 9, 2010
- 12,901
- 27,423
Anawaelekeza jinsi ya kuroga wagombea kama wanavyowaelekeza Tume na Polisi kutangaza nani mshindi au nani akamatwe.Wakuu,
Akizungumza leo kwenye Tamasha la Utamaduni la Bulabo la Kanda ya ZIWA, leo tarehe 21 Juni, 2025, Rais Samia amesema:
"Ombi langu hasa kwa viongozi hasa wa kimila, waganga wale wa kienyeji ombi langu, kipindi hiki wanaoomba kupata nafasi mbalimbali watawatembelea na wanapo watembelea niombe sana tusifanye ramli chonganishi kwa sababu hizo ndizo zinazovunja amani katika uchaguzi
"Kama atakuja na fungu we kula fungu, umemuona atashinda mwambie utashinda umemuona hatashinda, mwambie we nenda tu mambo mazuri, kula pesa yako nenda kalale. Lakini tusifanye ramli chonganishi. Kwamba naona kama utashinda lakini kuna katibu wako huyu wa mkoa naona kama hakupendi pendi hivi. Twende tufanye mambo kwa murua ili watu wote waende vizuri tumalize uchaguzi vizuri"
Huyu ataishia kutoa siri zote kwa kinywa chake. Hii ziara ni ya kumchosha tu mwili na kiakili ili waweze kum prove kuwa ni unfit.