Rais Samia: Wakurugenzi (DEDs) muda wenu wa uangalizi (probation) unaisha 18/02/2022 baada ya hapo tutaamua nani abaki nani aondoke

Rais Samia: Wakurugenzi (DEDs) muda wenu wa uangalizi (probation) unaisha 18/02/2022 baada ya hapo tutaamua nani abaki nani aondoke

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Rais Samia Hassan Suluhu amesema Wakurugenzi wa halmashauri walikuwa kwenye kipindi cha matazamio (probation) cha miezi sita ambayo inakamilika 18/02/2022.

Rais Samia amesema baada ya tarehe hiyo Waziri ataandaa performance report ya wakurugenzi wote ili ijulikane wanaobaki na wale watakaotumbuliwa wakaungane na wale wengine wanne waliotumbuliwa juzi.

Chanzo: TBC
 
Mpaka pale utaratibu wa teua teua ya kujuana utakapokoma ndio tutegemee uwajibikaji wa kimaadili na weledi.

Tanzania ina watu wengi wengi wenye Sifa na uwezo wa hizo kazi na pia wako interested na utayari.

Lakini wengi hawako tayari kujipendekeza kwa wnasiasa na kuwangukia kwa kufanya lobbying ili wateuliwe.

Maana mtu anaweza kuwa na Sifa lakini uwezo wa ku deliver hana au hapendelei tu hiyo kazi na maadili hana.

Lakini ukiwekwa utaratibu wa kutangaza hizo nafasi wenye utayari wakaomba wakachujwa na kufanya kwa mikataba renewable ingeweza kuleta tija sana kwa Taifa hili na vizazi vijavyo.
 
Asiishie kwa ma DED bali aende hadi kwa Wakuu wa Idara,wenye kukwamisha tunaomba Waziri wa Utumishi wapigwe chini na kushushwa cheo.

RC Happy kawalilia Sana leo na kasema hata ukiwahamisha hakuna unafanya.

Mwisho hivi madiwani Kazi yao nini? Kwa nini hawawezi kuwasimamisha Kazi Hawa? Yaani wakipewa vibahasha basi.
 
Wengine elimu zao za kuungaunga tu form four failures Eti anakuwa kiongozi wa watu kwa ngazi ya Wilaya au Halmashauri na kuendelea [emoji848][emoji848]

Hata uwezo wa kujenga, kujadili au kupangua hoja hana.

Uwezo wa kuongea mbele za watu hawanaga!

Kinachosukuma kufanya lobbying ni njaa na wala siyo uwezo wa kufanya kazi yenye kuleta matokeo dhahiri yenye tija.
 
Mama tupe rahaa, hawa wakurugenzi wanajikuta miungu watu halafu wezi tu...kipimo kianzie kwenye matumizi ya fedha ya covid, watabaki wachache mno.
 
Back
Top Bottom