Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, akizindua Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi leo tarehe 04 Oktoba 2024, jijini Dar es Salaam, amesema kuwa malalamiko ya walipa kodi yanatokana na ukweli kwamba kodi ni jambo gumu na mara nyingi si rahisi kukubalika. Amesema kuwa ni kawaida kwa mtu kuwa tayari kulipa faini kwa kosa, lakini kutokuwa tayari kulipa kodi, ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya taifa.