Rais Samia: Wameanza kuandika kwenye vigazeti kwamba sitasimama 2025, nani kawaambia?

Rais Samia: Wameanza kuandika kwenye vigazeti kwamba sitasimama 2025, nani kawaambia?

Hakuna cha mitano tena wala nini yeye amalize urithi wake asepe akacheze na wajukuu ufukweni huko!!!..Hatutaki tena raisi mwanamke kwenye nchii hii,Raisi unashindwa kuwa na maamuzi binafsi yaani unapangiwa cha kufanya mpaka raia wanashtukia mchezo mzima..Tunataka raisi mwenye misimamo wa kariba ya Magufuli(RIP)
 
"Sasa ndugu zangu Rais mwanamke tutamuweka madarakani mwaka 2025, wameanza kutuchokoza kuandika kwenye vigazeti kwamba Samia hatasimama nani kawaambia?"

SikuYaDemokrasiaDuniani
 
Rais Samia Suluhu amesema wanawake bado hawajamuweka Rais mwanamke bali aliyekuwepo amepatikana kwa kudra ya Mungu na matakwa ya katiba. Amesema walichofanikiwa wanawake ni kusukuma mpaka kumpata makamu wa Rais mwanamke.

Mengineyo, Rais Samia amesema ataendeleza mema yote katika awamu zote na watajitahidi kuongeza mema mengine.

Kuhusu usawa wa jinsia amesema hawajafika lakini wanawake wataendelea kuongezeka kwani asipofanya yeye hakuna ambae atafanya.
Hii nchi hii daah
 
Hayo ameyasema leo akizungumza na wanawake
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amesema hayo akishiriki katika maadhimisho ya siku ya Demokrasia duniani DIAMOND JUBILEE Dodoma kwa kusema wanawake hao wanapaswa kusimika Rais kwa kumchagua na yeye amesema mwaka 2025 ndio mwaka ambao Rais wa kike atachaguliwa.

Amesema hayo baada ya kurejea kwamba Rais mwanamke aliyepo kwa sasa ni kwa kudura za mwenyezi Mungu na matakwa ya katiba.
Hivyo mwaka 2025 wanawake wajitafakari na kuweka/kusimika Rais wa kike.
Ni haki yake ya kikatiba ila tunataka katiba mpya na tume huru ya uchaguzi kabla ya uchaguzi wa 2025.
 
Back
Top Bottom