Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Kwa kuangalia siku 100 za kwanza za Rais Samia Suluhu Hassan zilivyokuwa zimeleta matumaini makubwa kwa watanzania, katika kuijenga demokrasia na kuheshimu haki za binadamu, kwa namna alivyopiga U turn, katika siku chache zilizopita, ndipo hapo wananchi wanajiuliza, kimetokea nini tena kwa Rais Samia Suluhu Hassan?
Ningependa kulitolea jibu lake kama ifuatavyo:-
Nilichogundua ni kuwa Rais Samia amedanganywa na watu wake wa karibu kuwa wapinzani wanakupuuza wewe kutokana na maumbile yako ya kike.
Wanaendelea kumpotosha kwa kumwambia kuwa mbona alipokuwepo Magufuli, hukuona wapinzani wakidai Katiba mpya na badala yake wote waliufyata?
Sasa kutokana na Rais Samia naye kuwa na hiyo dhana ya kudharauliwa kutokana na maumbile yake ya kike, naye ndiyo hivyo ameingia "kingi" kwa kuwaamini hao "wapambe" wake naye kushusha rungu lake na "kum-victimize" huyo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
Hata hivyo naamini huyu Rais Samia Suluhu Hassan "ali-underestimate" matokeo yake baada ya dhana hiyo.
Kwa kuwa yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu, basi ni kama "amejiapiza" kuwa watakiona cha mtema kuni kutokana na dhana yao hiyo, kwa kuvitumia vyombo vya dola "kumbambikia" Mbowe makosa hayo ya ugaidi, kwa lengo tu la kumkomoa, kutokana na kile anachoamini yeye kuwa Mwenyekiti huyo, amedharau mamlaka yake!
Hata ukifuatilia hotuba zake zinadhihirisha hiyo "inferior complex" aliyo nayo, kwa kuwa mara kadhaa katika hotuba zake, amenukuliwa akijitapa kuwa yeye ni Rais mwenye maumbile ya kike!
Watanzania tunajiuliza, hivi kuna haja gani, kuyasema hayo wakati Watanzania wote tunajua kuwa wewe ndiye Rais wetu na Amiri Jeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi na usalama hapa nchini?