Pre GE2025 Rais Samia: Wananchi muache kuwachagua wanaowapa khanga na hongo hao sio wawajibikaji

Pre GE2025 Rais Samia: Wananchi muache kuwachagua wanaowapa khanga na hongo hao sio wawajibikaji

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Choice Variable.....nakuheshimu wewe ni kijani mwenzangu lakini hapo kwa LUHAGA MPINA unazinguq
Kura za maoni zitaamua.Kama anakubalika jimboni ila hayuko royal kwenye chama Kwa nini asihamie upande wa pili si atachagulowa tuu?
 
Si aruhusu aone iwapo atabaki...!
Nakushangaa aruhusu nini? Wewe umewahi msikia mwana CCM yeyeote akitamka hadharani kwamba anataka kupimana na Samia? Wote wanasema mama anatosha Sasa ruhusa ya nini unayotaka wewe?

Nimekuuliza mlichapisha fomu 1 mwaka 2020 Kwa Ajili ya Jiwe Kwa nini? Membe alijitokeza hadharani kupingana na Mwendazake na nyie jitokezeni kupingana na Samia shida nini?
 
Naunga Mkono hoja. Pia Labda utaratibu wa kulambisha wajumbe asali ubadilike!!!
Ndio maana ya kuwa na Mwenyekiti.Siku hizi wajumbe wanalamba asali na hawakuchagui.

Mwenyekiti atafyeka wote ambao hawakubaliki bila kujalisha walishinda Kwa asali
 
Mwaka 2020 mlichapisha Kasi ngapi za mgombea?

Fomu nyingi za nini wakati sijasikia mtu yeyote akitoka hadharani kusema anataka kushindana na Samia kama Membe alivyojitokeza? Mpaka hapo Kuna haja ya fomu nyingi?

Harafu yeye hajawahi kusema ila wanaomkubali ndio wanasema fomu Moja bwege wewe
Mwaka 2015 JPM alipigiwa kura na Halmashauri kuu ya CCM pamoja na wagombea wengine watano akiwemo Membe, J. Makamba, Asha Rose Migiro, na Amina salum akashinda.

Baadaye akiwa na wagombea wengine watatu yaan JPM, ASHANA AMINA wakapigiwa kura na mkutano mkuu wa CCM Magufuli akashinda
Je Samia amewahi Kushindanishwa na nani nafasi ya urais ndani ya CCM na akashinda ?
 
No,kwani Lazima mwenye mtazamo tofauti atoke upande wa pili. MPINA wahuni ndani ya chama wanamhujumu
Hana staha Huwa anafanya ukosoaji kama ugomvi,kuna wengi wanakosoa kama Gachuma,Mbunge wa Makete,Yule wa Sengerema nk

Wako wengi wanawasha moto sana ila Mpina ana nongwa.
 
Mwaka 2015 JPM alipigiwa kura na Halmashauri kuu ya CCM pamoja na wagombea wengine watano akiwemo Membe, J. Makamba, Asha Rose Migiro, na Amina salum akashinda.

Baadaye akiwa na wagombea wengine watatu yaan JPM, ASHANA AMINA wakapigiwa kura na mkutano mkuu wa CCM Magufuli akashinda
Je Samia amewahi Kushindanishwa na nani nafasi ya urais ndani ya CCM na akashinda ?
Na Mimi nimesema watu wajitokeze hadharani wachukue fomu kama wanaweza mshinda Samia ila Kwa kuwa wako kimya manake wanakubali mama anatosha zaidi ya kutosha.

Kwani mnaogopa nini? 😂😂😁😁

Ukimya wenu manake mumejipima mkaona msisumbue watu mama ni Moja kwa Moja Hadi 2030 pale ni fungulia mbwa 😆😆
 
Wakuu habari zenu.

Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa JMT Samia SH amesema Chama hicho kikubwa na makini kitawachuja na kuwaengua Wabunge wote ambao hawawanibiki Kwa Wapiga kura wao na wanaosababisha chama kupakwa matope.

Kwa mustakabali wa CCM na Taifa ni vyema tumsaidie Mwenyekiti kuwataja Wabunge ambao hawawajibiki Kwa Wananchi na chama Chao.

Listi Inaanza na Hawa,unaweza ongeza na wengine 👇

1. Luhaga Mpina (Kisesa)
2. Hammis Kigwangala (Nzega Vijijini)
3...
Unaweza ongeza na wengine

My Take: Hakuna Ubunge wa Mseleleko 2025.

============

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema chama hicho kitawapima viongozi wao wakiwemo wabunge, wawakilishi na Madiwani kutokana na utendaji kazi wao kama ambavyo ilani ya CCM ilivyoahidi kuwaletea maendeleo wananchi wake

Rais Dkt. Samia ameeleza hayo wakati akizundua kituo cha wajasiriamali kilichopo Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja kilichojengwa na Mwakilishi wa viti Maalum UWT kupitia Mkoa huo na Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Riziki Pembe Juma

Akiwa katika eneo hilo Dkt Samia amewataka wana-CCM kuwachagua viongozi wanaowajibika na kuacha kurubuniwa kwa kanga na fedha huku shughuli za maendeleo zikizorota

Amesema chama hicho kitataka kupata tathmini na kujionea juu ya hatua za maendeleo zilizofanywa na viongozi hao

Akiyataja mafanikio yatakayopatikana katika kituo hicho cha Wajasiriamali ni pamoja na kuwawezesha wananchi kiuchumi kupata shughuli rasmi ya kujiingizia kipato huku akiahidi kuongeza idadi ya Cherehani kwaajili ya kuendeleza harakati za kituo hicho

Dkt. Samia amehitimisha ziara yake leo katika mkoa wa Kaskazini Unguja ambapo kesho atamalizia ziara hiyo katika mkoa wa Kusini Unguja, Mjini na Magharibi

View: https://twitter.com/ccm_tanzania/status/1747622176277119336?t=dgSH5swozEznW9QWqIN4MA&s=19

Yeye mwenyewe anatakiwa achujwe.
 
Wakuu habari zenu.

Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa JMT Samia SH amesema Chama hicho kikubwa na makini kitawachuja na kuwaengua Wabunge wote ambao hawawajibiki Kwa Wapiga kura wao na wanaosababisha chama kupakwa matope.

Kwa mustakabali wa CCM na Taifa ni vyema tumsaidie Mwenyekiti kuwataja Wabunge ambao hawawajibiki Kwa Wananchi na chama Chao.

Listi Inaanza na Hawa,unaweza ongeza na wengine 👇

1. Luhaga Mpina (Kisesa)
2. Hammis Kigwangala (Nzega Vijijini)
3...
Unaweza ongeza na wengine

My Take: Hakuna Ubunge wa Mseleleko 2025.

============

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema chama hicho kitawapima viongozi wao wakiwemo wabunge, wawakilishi na Madiwani kutokana na utendaji kazi wao kama ambavyo ilani ya CCM ilivyoahidi kuwaletea maendeleo wananchi wake

Rais Dkt. Samia ameeleza hayo wakati akizundua kituo cha wajasiriamali kilichopo Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja kilichojengwa na Mwakilishi wa viti Maalum UWT kupitia Mkoa huo na Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Riziki Pembe Juma

Akiwa katika eneo hilo Dkt Samia amewataka wana-CCM kuwachagua viongozi wanaowajibika na kuacha kurubuniwa kwa kanga na fedha huku shughuli za maendeleo zikizorota

Amesema chama hicho kitataka kupata tathmini na kujionea juu ya hatua za maendeleo zilizofanywa na viongozi hao

Akiyataja mafanikio yatakayopatikana katika kituo hicho cha Wajasiriamali ni pamoja na kuwawezesha wananchi kiuchumi kupata shughuli rasmi ya kujiingizia kipato huku akiahidi kuongeza idadi ya Cherehani kwaajili ya kuendeleza harakati za kituo hicho

Dkt. Samia amehitimisha ziara yake leo katika mkoa wa Kaskazini Unguja ambapo kesho atamalizia ziara hiyo katika mkoa wa Kusini Unguja, Mjini na Magharibi

View: https://youtu.be/sr8TOTZwZo4?si=lplOV1SmplGf6ShT

Kwa mara nyingine mods wamebadili heading.Hovyo kabisa

View: https://www.instagram.com/reel/C2Rw5L7qnib/?igsh=NnhvNm1iamdudmZn
 
Back
Top Bottom