Rais Samia wape meno TFS, anzisha kampeni ya upandaji na utunzaji Miti Tanzania nzima. Iongozwe na vijana wa kujitolea JKT

Asante Mkuu. Kweli kabisa hizi jitihada zilitakiwa ziwe zinafanywa na Taasisi zinazohusika na masuala ya Mazingira ila ndo ivyo zimelala hadi ziamshwe
Wanachojua ni kugawana maposho tu na vikao vya kwenda nje
 
First time napita Tabora msimu wa kiangazi nilishangaa kama hii ni Tanzania. Kulikuwa na jua kali sana na hakuna miti ni vichaka tu. Hapo nimetoka kanda ya kijani kibichi sijawahi ona unatembea mwendo wa lisaa road bila kukutana na daraja. Nilipofika Dodoma ndio kabisa nikachoka
 
Naunga mkono hoja. Mimi ninaposafiri nakushuhudia mistu inavyochomwa moto nahuzunika sana

Sio siri ila wafugaji wabaya sana mfano Wasukuma nimewashuhudia wakikata miti sana

Yaani anataka akifika mahali aonekane maili kadhaa kwamba huo ni mji wake kwa hiyo anaanzisha vita na Miti yote iliyopo hapo

Halafu kibaya zaidi hawa wanaohama hama wanakaa mda mchache halafu wanahama tena kwenda kuharibu sehemu zingine

Halafu wakipigwa faini wanaanza kulia na kutishia kuroga hapo ndio huwa wanaharibu kabisa

Hawa wanahitaji somo kubwa sana kwa jamii za wafugaji wote aidha kwa kufundishwa au wasipotaka kuelewa wafilisiwe kabisa
 
Hii nchi kama hatujachukua hatua madhubuti sasa tunaweza jikuta tuko kwenye ukame mkubwa na tuna uganda wa chakula ambao hatujawai kushuhudia

Mikoa yenye miti Mingi kama Njombe, Ruvuma na Kagera hawana shida ya mvua na uzalishaji wa chakula Uko sawa! Ila mikoa yote yenye ukataji Miti wa hovyo kama Tabora hali inatisha Kwa kweli!
 
Umuhumu wa miti wanaujua ispokuwa wanaangalia maslahi ya mwaka mmoja miwili tu
 
Serikali hairogwi dawa yao hawa watu ni kuwarudisha kwenye maeneo yao ya asili na kuwalazimisha waishi huko na kufanya uzalishaji huko. Sheria zitungwe za kuwafanya watu kufuga idadi kadhaa ya MIFUGO na kuhakikisha wanafuga kibiashara na sio Kama sifa tena Kwa teknolojia bora!

Kwa walivyoharibu Katavi, Rukwa, Tabora na maeneo ya Morogoro itafika kipindi hata haya mabwawa ya umeme tunayojenga kwa gharama kubwa yatakosa maji ya kuzaliwa umeme maana hii nchi inakoelekea ni kukumbwa na ukame wa kutisha utakaoathiri kuanzia upatikanaji wa chakula hadi umeme kwenye mabwawa yetu!
 
Umuhumu wa miti wanaujua ispokuwa wanaangalia maslahi ya mwaka mmoja miwili tu
Nadiriki kusema Jamii za wafugaji na baadhi za wakulima ( Mf Wasukuma na Wamasai) Hawajui umuhimu wa Miti. Na mbaya zaidi wanaikata huku hawajui kuwa kuikata hiyo Miti ndo kumesababisha kwao kuwe kukame na Hadi wanahamia maeneo mengine ambapo badala ya kutunza mazingira kwenye hayo maeneo wao wanazidi kuyaharibu kwa kukata miti!
 
Mtoa mada umenena vyema kabisa misitu inazidi kupungua kwa Kasi Sana,,, nikipita mikoa hasa ya Kanda ya Kati Dom, Tabora au singida huwa naona maeneo jinsi yalivy nusu jangwa nasikitika Sana alaf kitu kingine huwa sipend no kuona misitu na mapori makubwa yanaungua hii naonaga San home ruvuma has wakat wa kiangazi unaona milimani kunaungua Moto mkubwa kabisa inauma Sana yan
 
Hili suala la upandaji miti kwa kweli linahitaji msukumo wa kipekee wa serikali na asasi nyingine binafsi.

Lakini pia sisi wenyewe raia tubadilike maana wanaokata miti na kuharibu misitu ni sisi wenyewe au ndugu zetu.

Vinginevyo tutawaacha watoto wetu kwenye nchi ya taabu na majuto makubwa na watalaani makaburi yetu.
 

Hawana akili Mkuu
Imagine baba ana ng’ombe 1000 halafu watoto 20 baada wanamuuwa baba kwa ajili ya mali mda hata mwaka hauishi wameuza zote wanaanza kuwa majambazi na wizi wa ng’ombe tena
Hawafai kabisa ni waharibifu sana
 
Tukiendelea kucheka kana kwamba hakuna kesho tutajikuta nchi ina uhaba wa mvua, chakula hakitoshi na mabwawa yetu ya umeme tuliyoyajenga kwa gharama kubwa hayana maji ya kutosha kuzalisha umeme!

Hapo ndo watoto wetu watafungua Kweli makabuli na kuchunguza vichwa vyetu
 
Wafungwa watumike kupanda miti nchi nzima hii inawezekana
 
Sijasoma uliyoandika humo ndani, lakini kufuatana na kichwa cha mada yako, hii inaweza kuwa moja ya mada muhimu sana kujadiliwa hapa JF.

Naunga mkono na miguu kwa pamoja.
 
EeeeenHeeee,
'Lord' Bhwanaaa; itasaidia kitu gani kama kaTanzania haka kanafanya unavyotaka, huku msitu mzima wa Congo unateketea!
Hii siyo kazi ya nchi moja mkuu!
 
afforestation+guatemala+2020&sxsrf=AOaemvJHysCZeVmk0GH2NV0EAHHtOXTRCw:1634561252336&source=lnms&tbm=isch&sa=X&ved=2ahUKEwie-buW_9PzAhUBJBoKHV6GDrkQ_AUoAXoECAEQAw&biw=1366&bih=657&dpr=1
 
afforestation+guatemala+2020&sxsrf=AOaemvJHysCZeVmk0GH2NV0EAHHtOXTRCw:1634561252336&source=lnms&tbm=isch&sa=X&ved=2ahUKEwie-buW_9PzAhUBJBoKHV6GDrkQ_AUoAXoECAEQAw&biw=1366&bih=657&dpr=1
Duh
 
EeeeenHeeee,
'Lord' Bhwanaaa; itasaidia kitu gani kama kaTanzania haka kanafanya unavyotaka, huku msitu mzima wa Congo unateketea!
Hii siyo kazi ya nchi moja mkuu!
Tanzania tufanye sehemu yetu. Tukitunza mazingira vizuri tutakula matunda ya kutunza mazingira vizuri.

Tusipotunza tutajikuta Kuna mda tunaagiza chakula chote kutoka nje! Hapo ndo kutakuwa na hatari kwenye amani na Usalama wetu maana kwa hali yetu ya kiuchumi hatutaweza kuwa na amani tukiwa tegemezi kichakula
 
SAWA, lakini ninachosemaaaa, ni kwamba Tanzania kutunza mazingira kwa upande wake haitoshi pasipo kuwepo na ushirikiano na majirani zetu
Msitu tutakaotunza sisi si ajabu ukawa na manufaa zaidi kwa majirani zetu kuliko sisi katika upatikanaji wa mvua. Sisi tunaweza tukawa tunategemea zaidi misitu ya Congo na kwingineko na bahari ya hindi kuliko misitu yetu pekee katika upatikanaji wa mvua za kutosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…