Wanachojua ni kugawana maposho tu na vikao vya kwenda njeAsante Mkuu. Kweli kabisa hizi jitihada zilitakiwa ziwe zinafanywa na Taasisi zinazohusika na masuala ya Mazingira ila ndo ivyo zimelala hadi ziamshwe
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wanachojua ni kugawana maposho tu na vikao vya kwenda njeAsante Mkuu. Kweli kabisa hizi jitihada zilitakiwa ziwe zinafanywa na Taasisi zinazohusika na masuala ya Mazingira ila ndo ivyo zimelala hadi ziamshwe
Wanatia hasira sana Kwa kweli!Wanachojua ni kugawana maposho tu na vikao vya kwenda nje
Naunga mkono hoja. Mimi ninaposafiri nakushuhudia mistu inavyochomwa moto nahuzunika sana
Hii nchi kama hatujachukua hatua madhubuti sasa tunaweza jikuta tuko kwenye ukame mkubwa na tuna uganda wa chakula ambao hatujawai kushuhudiaFirst time napita Tabora msimu wa kiangazi nilishangaa kama hii ni Tanzania. Kulikuwa na jua kali sana na hakuna miti ni vichaka tu. Hapo nimetoka kanda ya kijani kibichi sijawahi ona unatembea mwendo wa lisaa road bila kukutana na daraja. Nilipofika Dodoma ndio kabisa nikachoka
Umuhumu wa miti wanaujua ispokuwa wanaangalia maslahi ya mwaka mmoja miwili tuSio siri ila wafugaji wabaya sana mfano Wasukuma nimewashuhudia wakikata miti sana
Yaani anataka akifika mahali aonekane maili kadhaa kwamba huo ni mji wake kwa hiyo anaanzisha vita na Miti yote iliyopo hapo
Halafu kibaya zaidi hawa wanaohama hama wanakaa mda mchache halafu wanahama tena kwenda kuharibu sehemu zingine
Halafu wakipigwa faini wanaanza kulia na kutishia kuroga hapo ndio huwa wanaharibu kabisa
Hawa wanahitaji somo kubwa sana kwa jamii za wafugaji wote aidha kwa kufundishwa au wasipotaka kuelewa wafilisiwe kabisa
Serikali hairogwi dawa yao hawa watu ni kuwarudisha kwenye maeneo yao ya asili na kuwalazimisha waishi huko na kufanya uzalishaji huko. Sheria zitungwe za kuwafanya watu kufuga idadi kadhaa ya MIFUGO na kuhakikisha wanafuga kibiashara na sio Kama sifa tena Kwa teknolojia bora!Sio siri ila wafugaji wabaya sana mfano Wasukuma nimewashuhudia wakikata miti sana
Yaani anataka akifika mahali aonekane maili kadhaa kwamba huo ni mji wake kwa hiyo anaanzisha vita na Miti yote iliyopo hapo
Halafu kibaya zaidi hawa wanaohama hama wanakaa mda mchache halafu wanahama tena kwenda kuharibu sehemu zingine
Halafu wakipigwa faini wanaanza kulia na kutishia kuroga hapo ndio huwa wanaharibu kabisa
Hawa wanahitaji somo kubwa sana kwa jamii za wafugaji wote aidha kwa kufundishwa au wasipotaka kuelewa wafilisiwe kabisa
Nadiriki kusema Jamii za wafugaji na baadhi za wakulima ( Mf Wasukuma na Wamasai) Hawajui umuhimu wa Miti. Na mbaya zaidi wanaikata huku hawajui kuwa kuikata hiyo Miti ndo kumesababisha kwao kuwe kukame na Hadi wanahamia maeneo mengine ambapo badala ya kutunza mazingira kwenye hayo maeneo wao wanazidi kuyaharibu kwa kukata miti!Umuhumu wa miti wanaujua ispokuwa wanaangalia maslahi ya mwaka mmoja miwili tu
Serikali hairogwi dawa yao hawa watu ni kuwarudisha kwenye maeneo yao ya asili na kuwalazimisha waishi huko na kufanya uzalishaji huko. Sheria zitungwe za kuwafanya watu kufuga idadi kadhaa ya MIFUGO na kuhakikisha wanafuga kibiashara na sio Kama sifa tena Kwa teknolojia bora!
Kwa walivyoharibu Katavi, Rukwa, Tabora na maeneo ya Morogoro itafika kipindi hata haya mabwawa ya umeme tunayojenga kwa gharama kubwa yatakosa maji ya kuzaliwa umeme maana hii nchi inakoelekea ni kukumbwa na ukame wa kutisha utakaoathiri kuanzia upatikanaji wa chakula hadi umeme kwenye mabwawa yetu!
Tukiendelea kucheka kana kwamba hakuna kesho tutajikuta nchi ina uhaba wa mvua, chakula hakitoshi na mabwawa yetu ya umeme tuliyoyajenga kwa gharama kubwa hayana maji ya kutosha kuzalisha umeme!Hili suala la upandaji miti kwa kweli linahitaji msukumo wa kipekee wa serikali na asasi nyingine binafsi.
Lakini pia sisi wenyewe raia tubadilike maana wanaokata miti na kuharibu misitu ni sisi wenyewe au ndugu zetu.
Vinginevyo tutawaacha watoto wetu kwenye nchi ya taabu na majuto makubwa na watalaani makaburi yetu.
EeeeenHeeee,Tukiendelea kucheka kana kwamba hakuna kesho tutajikuta nchi ina uhaba wa mvua, chakula hakitoshi na mabwawa yetu ya umeme tuliyoyajenga kwa gharama kubwa hayana maji ya kutosha kuzalisha umeme!
Hapo ndo watoto wetu watafungua Kweli makabuli na kuchunguza vichwa vyetu
afforestation+guatemala+2020&sxsrf=AOaemvJHysCZeVmk0GH2NV0EAHHtOXTRCw:1634561252336&source=lnms&tbm=isch&sa=X&ved=2ahUKEwie-buW_9PzAhUBJBoKHV6GDrkQ_AUoAXoECAEQAw&biw=1366&bih=657&dpr=1Nakusalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano Tanzania Mama!
Kwanza nikupongeze kwa Mafanikio makubwa yanayoonekana kwenye suala la kuwahamisha Machinga na kuwapeleka maeneo rasmi. Na furaha nchi sasa imeanza kupendeza hasa majiji yetu! Nimepita Posta mpya leo na Kweli nimeiona Posta niliyoijua miaka ya 90 mwanzoni. Hongera Kwa hili! Majiji Yanaanza kupendeza bila ya kutumia ubabe wala bunduki!
Nirudi kwenye mada yangu!
Leo napenda tena kutumia fursa hii kukushauri Mhe Rais wa JMT Mama yetu Samia Suluhu Hassan baada ya kufanya utafiti kidogo juu ya hali ya mazingira hapa Tanzania.
Kwenye utafiti wangu huu, nimegundua mambo yafuatayo ambayo yamenifanya Leo niandikie humu kukushauri!
1. Nyanda za Juu kusini hasa mikoa ya Iringa, Mbeya na Songwe kuna hatari kubwa sana ya mikoa hii kukubwa na ukame miaka michache ijayo. Hii ni kutokana na shughuli za ukataji miti zinazoendelea kwa kasi kwenye mikoa hii na kasi ndogo ya kupanda Miti kwenye mikoa hii. Mikoa hii ni moja ya mikoa tegemezi kwa uzalishaji chakula. Ukataji wa Miti na kuongezeka kwa ukame kwenye mikoa hii kunaleta hatari ya mikoa hii kutozalisha chakula cha kutosha huko miaka ya mbele na kuifanya nchi kuanza kuwa tegemezi kwenye chakula!
2. Kanda ya Kati hasa Dodoma , Singida na Tabora hali ni mbaya sana. Kuna ukame mkubwa sana kwenye haya maeneo na hali ikiendelea kuwa hivi Kuna hatari kubwa hii mikoa kushindwa kabisa kuzalisha chakula. Hakuna Miti na wala Hakuna jitihada zozote kuongeza Miti na uoto kwenye maeneo haya.
Kwa Tabora ambako kulikuwa na Miti mingi, kwa sasa Kuna ukataji mkubwa sana wa miti unaofanywa na wahamiaji kutoka mikoa ya kanda ya Magharibi na kanda ya Ziwa. Wahamiaji hawa wanaharibu kweli mazingira na kusema kweli tusipoangalia hii mikoa itakuja kukosa kabisa mvua na uoto mzuri kutokana na ukataji Miti wa kutisha unaoendelea kwenye mikoa hii! Kwa sasa haizalishi chakula cha kutosha na kwa uharibifu huu wa mazingira huko mbeleni inaonekana hali itakuwa mbaya zaidi
3. Kanda ya Magharibi hasa Mikoa ya Rukwa, Kigoma na Katavi huku Pia yanayoendelea sio mazuri, wahamiaji kutoka kanda ya ziwa na nchi za jirani wanaingia kwa kasi kwenye mikoa hii na kukata Miti kwa Kiwango cha kutisha. Mikoa ya Rukwa na Katavi imeanza kupata mvua kwa Kiwango kisichoridhisha na hii ni kutokana na ukataji mkubwa wa Miti unaofanyika kwenye mikoa hii.
Kwa sasa Tanzania inategemea mikoa hii pamoja na RUVUMA, Mbeya, Iringa na Njombe bila kusahau morogoro ila kwa hali inavyokwenda, huko mbele inaonekana ukataji huu wa kutisha wa miti kwenye mikoa yote hii, utapelekea nchi kupata mvua kwa Kiwango cha chini hivyo kupungua kwa uzalishaji wa chakula na kuanza kutegemea chakula kutoka nje!
4. Kanda ya Ziwa mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Simiyu bila kusahau Geita, huku ndo hakufai pia! Watu wa mikoa hii wameharibu sana mikoa yao kwa kukata Miti hivyo kupelekea kutokupata kwa mvua ya kutosha na kushindwa kuzalisha chakula cha kutosha!
Watu wa mikoa hii sasa wanahamia mikoa ya Tabora, Rukwa , Katavi na Singida na wanachokifanya kule ndo walichofanya kwenye mikoa yao jambo lililopelekea kukubwa na ukame na kushindwa kuzalisha chakula cha kutosha. Ukienda katavi leo wanaingia katikati ya misitu ikiwemo hifadhi na wanakata Miti na kuanzisha mashamba! Wanafanya hivi huku wakitegemea serikali mtarasimisha hayo maeneo na kuwapa kuendelea na makazi! Wanaiweka nchi kuwa na hatari ya kuwa jangwa katika siku chache zijazo
5. Kanda ya Mashariki- Hasa Mkoa wa Morogoro na Pwani ambako wamasai baada ya kusababisha ukame maeneo ya ARUSHA sasa wamehamia kwa kasi kwenye mikoa hii ambako wanachofanya ni kukata Miti , kuharibu uoto wa asili kutokana na wingi wa MIFUGO yao. Hili linapelekea ukame kukua na kuinyemelea kwa kasi Kubwa mikoa hii ya PWANI na Morogoro.
Ushauri wangu
1. Naomba Serikali yako iache kurasimisha maeneo yanayovamiwa na watu hasa mapori na hifadhi. Tanzania haijaisha maeneo. Watu warudishwe kwenye maeneo yao ya asili na waelekezwe namna ya kuishi huko kwa kupanda Miti na kutunza mazingira na kufanya uzalishaji huko. Tabia hii ya kuacha watu wanavamia maeneo alafu badae wanapewa uhalali wa kuishi huko ndo inazidi kuifanya nchi yetu kuzidi kuwa jangwa na badae tutashindwa hata kuzalisha chakula cha kutosha Kwa kukosa mvua!
Kwenye hili kama Jamii ni ya wafugaji, wapewe teknolojia na wafundishwe kufuga wanyama wachache kibiashara. Suala la mtu kumiliki ng’ombe 5000 wakati hana teknolojia ya kuwalisha bila kuharibu mazingira limepitwa na wakati! Watu wafuge kwa teknolojia Bora ya kisasa tena kibiashara.
Ni vizuri serikali ikaanza kuweka Sheria ya kudhibiti idadi ya mifugo ya aina ya teknolojia ya ufugaji ili kuokoa mazingira yetu na uhai wetu
2. Wape meno Wakala wa Misitu wasimamiw Kweli Sheria zetu. Kwa hili napenda kukiri kuwa TFS wako vizuri ila wanarudishwa nyuma na wanasiasa. Kwenye hili Naomba wape meno TFS wasimamie misitu yote iliyovamiwa na wawaondoe watu wote waliovamia maeneo hayo!
TFS pia wapewe mandate ya kuhakikisha mapori ya misitu iliyoharibiwa vinarudishwa katika hali yake ya ubora! Hili litaokoa maeneo yetu ya kufanya nchi iendelee kupata mvua Nzuri na kuendeleza kilimo
3. Kupitia vijana wa JKT na TFS pia , naomba uanzishe kampeni kabambe ya upandaji Miti. Ethiopia waliofanya hivi miaka ya 90-2000 na sasa wamefanikiwa sana na upandaji ule wa Miti uliwawezesha kupata mvua za kutosha na sasa wameweza zalisha chakula kingi.
Naomba uanzishe hili Tanzania na kipaumbele iwe mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora, kanda ya Ziwa bila kusahau Songwe na Morogoro, huku ipandwe Miti mingi ikiwezekana hata Miti Bil 1 nchi nzima na ifanyiwe kampeni ya kuitunza na kuilinda. Hapa nafikiri tutafanikiwa sana!
Naomba kuishia hapa!
Duhafforestation+guatemala+2020&sxsrf=AOaemvJHysCZeVmk0GH2NV0EAHHtOXTRCw:1634561252336&source=lnms&tbm=isch&sa=X&ved=2ahUKEwie-buW_9PzAhUBJBoKHV6GDrkQ_AUoAXoECAEQAw&biw=1366&bih=657&dpr=1
Tanzania tufanye sehemu yetu. Tukitunza mazingira vizuri tutakula matunda ya kutunza mazingira vizuri.EeeeenHeeee,
'Lord' Bhwanaaa; itasaidia kitu gani kama kaTanzania haka kanafanya unavyotaka, huku msitu mzima wa Congo unateketea!
Hii siyo kazi ya nchi moja mkuu!
SAWA, lakini ninachosemaaaa, ni kwamba Tanzania kutunza mazingira kwa upande wake haitoshi pasipo kuwepo na ushirikiano na majirani zetuTanzania tufanye sehemu yetu. Tukitunza mazingira vizuri tutakula matunda ya kutunza mazingira vizuri.
Tusipotunza tutajikuta Kuna mda tunaagiza chakula chote kutoka nje! Hapo ndo kutakuwa na hatari kwenye amani na Usalama wetu maana kwa hali yetu ya kiuchumi hatutaweza kuwa na amani tukiwa tegemezi kichakula