SI KWELI Rais samia: Watanzania, ipo siku mtanikumbuka kwa mazuri ninayowafanyia

SI KWELI Rais samia: Watanzania, ipo siku mtanikumbuka kwa mazuri ninayowafanyia

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Kumekuwepo na nukuu inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikidaiwa kutolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ikisema:"Watanzania, ipo siku mtanikumbuka kwa mazuri ninayowafanyia."

Nukuu hiyo imesambazwa kwenye kupitia vikundi vya facebook ikiwa na graphic ya proje updates

He ni upin uhalisia wa nukuu hiyo ?
SAMIA NUKUU.jpg
 
Tunachokijua
Julai 20, 2026 Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alikuwa Kigoma akiweka jiwe la ujenzi wa reli ya kisasa ya umeme mkoani humo pamoja na uzinduzi wa meli za mizigo.

Madai

Kupitia mitandao ya kijamii kumeibuka nukuu inayodaiwa kuwa imetolewa na kiongozi huyo akisema kuwa "Watanzania mtanikumbuka kwa mazuri ninayowafanyia"

Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imefuatila na kujiridhisha kuwa nukuu hiyo si ya kweli na haijatolewa na Rais Samia. Hakuna kumbukumbu zozote kuonesha kuwa Rais Samia alitoa nukuu hiyo.

Katika hotuba yake aliyoitoa Kigoma, Rais Samia alizungumzia umuhimu wa reli hiyo kwa taifa na kuwataka wananchi watunze amani na kudumisha umoja na mshikamano. Rejelea hotuba hiyo hapa. Sambamba na hilo ufuatiliaji zaidi umebaini kuwa hakuna chanzo cha kuaminika kilichochapisha taarifa hiyo
Hawezi kusema hivyo maana anajijua alivyotuharibia tanganyika yetu.tutamkumbuka kwa mabaya.mfano kuua watanganyika mamilioni na mamilioni siku ya mo29
 
Aisee watu wamemlisha mheshimiwa rais maneno yao. Wachukuliwe hata kwa mujibu wa Sheria za matumizi mbaya ya mitandao ya kijamii
 
Back
Top Bottom