Rais Samia: Watunza kumbukumbu mnapaswa kutunza siri za Serikali

Kwa hiyo kunasiri ambazo wananchi hatutakiwikuzijua?Nchi ni yetu wote kwanini tuwekeane mipaka
 
Kwamba records management nayo ni profession? Ukarani masjala nao ni taaluma eti.
We nae punguwani.kama sio taaluma ni nini? Hivi wewe unaweza kukaa pale ujue folio hii inaenda wap.? Dispatching na kujua mafail wakina nani wamelala nayo hawayatoi na kuyapa kumb namba na mfumo kuyaona yanavotembea.au unafikir rahis kama unavyotawazaga na kopo lako la maji
 
Kumbukumbu za nyaraka ni kwa ajili ya historia ya nchi/jamii husika na rejea ili kujifunza kutokana na mafanikio au makosa ya awali.

Ni kweli kuna kumbukumbu zinatakiwa zisiwekwe hadharani mpaka kipindi fulani kipite ambacho kinatakiwa kiwekwe kwa mujibu wa sheria. Pia siri haihusu masuala ambayo ni ya jinai.Tatazo la taalauma hii ni umakini, wingi na usahihi wa kumbukumbuku zenyewe.

Fanya utafiti wa masuala ya 1970s hapa Tanzania ndipo utaona kumbukumbuku zenyewe zilipo na zilivyo. Hapo ndipo utajua kama muhimu ni siri au kazi yenyewe kufanyika katika viwango vya kimataifa ili vizazi vijavyo vijue historia ya nchi/jamii yao!
 
Rais Samia Suluhu Hassan amewahakikishia watunza kumbukumbu na nyaraka nchini kuwa Serikali itawalinda kwa kutambua kada hiyo ni kitovu cha Serikali.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Jumapili Novemba 27, 2022 jijini Arusha katika mkutano mkuu wa 10 wa Chama cha Taaluma ya Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA).

Amewataka watunza kumbukumbu kutunza siri za Serikali kwa uadilifu na weledi, kwani wasipofanya hivyo watadhulumu haki za watu.

“Chukua picha wewe ni mtunza kumbukumbu kwenye sekta ya kilimo, kuna mambo ya ruzuku hufanyi uadilifu uaanacha kompyuta kaingia mtu mwingine kaingilia hizo taarifa, wakulima wanasubiri mbolea wewe taarifa ulizonazo si hizo zilizokusanywa kwenye field

“Unawakosesha wakulima mbolea msimu unapita, tunakwenda bila chakula, akiba ya chakula hakuna angalia kosa lako dogo linavyoleta athari,” amesema.

Amesema kumekuwa na utaratibu mbovu wa nyaraka za Serikali kuwekwa mitandaoni, jambo alilosema linakwenda kinyume na utaratibu wa taalamu hiyo na kuleta athari katika utoaji haki za watu.

Chanzo: Mwananchi
 
Yaan kama kuna kitu kinahitaji mawanda mapana ni kuhusu kumbukumbu za kiserikali na teknolojia ya mawasiliano

Ufikishaji wa taarifa na sembuse hata utunzaji wa kumbukumbu hizo unategemea kwa kiasi kikubwa teknolojia ya mawasiliano ambayo ndio changamoto kubwa kwa kufikisha hizo taarifa hata mahala pasipofaa kupitia emails, whatsup, telegrams, texts n.k

Maana hata hapa tunazipata hizi taarifa za kuwepo kwa mkutano huo mkuu wa kumi wa utunzaji wa kumbukumbu instantly kwasababu ya platforms za kupashana habari za kidigitali

Hapa inabidi tu ukubali ukipenda Asali pia kubali manundu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…