Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
RAIS SAMIA AFURAHISHWA NA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA
"Nimefurahishwa pia kwamba Watoto mmeniimbia wimbo mzuri san. Wimbo ulionihakikishia kwamba huduma zote zinapatikana. Na nimekwenda kuona bwalo tu, nimeona huduma zote zinapatikana. Kilichonifurahisha zaidi ni matumizi ya nishati safi ya kupikia. Huu ni mradi wangu nilioubeba kwa ajili ya wanawake wa Afrika,” Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
SSH-TUMIENI VIZURI FURSA YA ELIMU MLIYOPATA
"Lakini jengine niwatake Watoto wangu mliopata fursa ya elimu kuitumia vizuri sana nafasi hii. Sitaki nisikie shule hii in amsururu wa walipata zero, hawakupata vyeti sijui daraja la nne aaah aaah, na mmeniambia kwenye kupasi hakuna wasiwasi,” Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
SSH-WATUNZENI WATOTO TUSIJE KUSIKIA KESI ZA UJAUZITO
"Nizungumze kidogo na walimu, kwanza hongereni mwalimu mkuu hongera na walimu wenzio wote ambao mmekabidhiwa Watoto hawa. Nalotaka kuongea nanyi ni kwamba tumewakabidhi Watoto wetu, mazingira ni mazuri lakini niwaombe sana ninyi ndiyo Mungu amewachagua kuwa na watoto hawa, naomba watunzeni,” Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.