Rais Samia: Watunzeni Watoto wetu tusije kusikia kesi za Ujauzito

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Your browser is not able to display this video.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mchepuo wa Sayansi na Sanaa Namtumbo Mkoani Ruvuma iliyopewa jina la ya Dr.Samia Suluhu Hassan ambayo ujenzi wake umegharimu Shilingi Bilioni 4.6 leo September 27,2024.

RAIS SAMIA AFURAHISHWA NA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA
"Nimefurahishwa pia kwamba Watoto mmeniimbia wimbo mzuri san. Wimbo ulionihakikishia kwamba huduma zote zinapatikana. Na nimekwenda kuona bwalo tu, nimeona huduma zote zinapatikana. Kilichonifurahisha zaidi ni matumizi ya nishati safi ya kupikia. Huu ni mradi wangu nilioubeba kwa ajili ya wanawake wa Afrika,” Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.



SSH-TUMIENI VIZURI FURSA YA ELIMU MLIYOPATA
"Lakini jengine niwatake Watoto wangu mliopata fursa ya elimu kuitumia vizuri sana nafasi hii. Sitaki nisikie shule hii in amsururu wa walipata zero, hawakupata vyeti sijui daraja la nne aaah aaah, na mmeniambia kwenye kupasi hakuna wasiwasi,” Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.



SSH-WATUNZENI WATOTO TUSIJE KUSIKIA KESI ZA UJAUZITO
"Nizungumze kidogo na walimu, kwanza hongereni mwalimu mkuu hongera na walimu wenzio wote ambao mmekabidhiwa Watoto hawa. Nalotaka kuongea nanyi ni kwamba tumewakabidhi Watoto wetu, mazingira ni mazuri lakini niwaombe sana ninyi ndiyo Mungu amewachagua kuwa na watoto hawa, naomba watunzeni,” Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…