Rais Samora Machel, alimchukiza Mungu kuliko maraisi wote Africa

We mleta mada uliwasiliana na huyo mungu na akakuthibitishia kama ulivyohitimisha hapo kwenye heading yako..!?

nafikiri ata mimi ndio swali nilikua nataka kumuuliza mkuu,thanks alot kwa kunisaidia hilo.
 
 

Haohao waliotuletea dini Afrika ndio haohao waliooandika hicho kitabu unategemea wataandika mazuri kuhusu Samora ikumbukwe kwamba kabla ya Wazungu na waarabu hawajaja Afrika kulikuwa hakuna Ukristo wala Uislamu. kwahiyo kwa upande mwingine Samora inabidi aeleweke kwanini alifanya hivyo. "Afrika dini zililetwa tu"- Afande Sele
 
hivi ni kosa kwa kikundi cha watu kuamua kumuita Osama bin laden mtakatifu kama wao wana amini hivyo? na hata kanisa katoliki likiamua kumuita nyerere mtakatifu ni uamuzi wake
 

Samora alikuwa shujaa wa kweli. Alichofanya dhidi ya dini ni sahihi kabisa. Hizi dini ni fujo tu.
 
Soma kitabu hicho kwanza halafu njoo ukanushe. Sasa kama alimpinga mkoloni , ndio alikuwa na haki ya kufuta uhuru wa kuabudu? yesu kamkosea nini mpaka avunje altare yake ?

Kanisa au Msikiti au nyumba yoyote ya ibada ambayo inatumika kinyume na matakwa ya Mungu (Haipo kwa maslahi ya Mungu), inamkera Mungu pia! Hicho kitabu sikitafuti wala sikihitaji, kwamaana hata nikisoma bado pia naweza kupinga yaliyoandikwa kama ni ya kupotosha na kujipendekeza kwa Mungu kuwafurahisha wanadamu.

Usimshuhudie jirani yako uongo a.k.a Acha unafiki. Makanisa yale yalikiuka hii amri
 
ungeuliza kwanini wakatoliki wanataka kumfanya nyerere mtakatfu ningekuelewa

Nyerere mwenyewe alishakataa suala la kanisa katoliki kumfanya yeye mtakatifu, kuna kipindi walimfuata wakamdokeza kuhusu hilo suala.
Hapa swali ni je kanisa katoliki linamjua Nyerere kuliko yeye mwenyewe anavyojijua?
 
who alleges must prove,come forward with cogently arguments sio hizi street rumans zako.
 
Dini za kigeni zilitangulia kusafisha njia ya ukoloni kuja afrika; kwani wewe hulijui hilo? Kwani wewe unadhani utakatifu lazima mtu aamini dini? Hao waliokua wanawachuuza waafrika kama bidhaa walikua wanakwenda misikitini na makanisani kusali.
 
Ukweli upo pale pale, samora hakustahili heshima aliyopewa na nyerere. nimekupa kitabu na page ya kusoma ili usome na uone mwenyewe ukweli wa samora, je kosa lipo wapi?
Wewe ndio mburula kweli! Nyerere alipambana na hao akina reagan kwa kuwasaidia wareno dhidi ya ukombozi wa msumbiji sasa unatuambia tusome kitabu chao kuhusu ubaya wa nyerere.
 

Nyerere na Samora Machel au TANU na FRELIMO jambo walilokuwa nalo common ni ukombozi wa msumbiji au uhuru wa msumbiji. Tanzania ilianzisha ujamaa kupitia azimio la arusha mwaka 1967 kama aina moja wapo ya African socialism ingawa mifumo Fulani ilifanana na ya kikomunisti kasoro ile ya socialist revolution na mambo ya kutoamini mungu et.c. Samora aliingiza Socialism through socialist revolution mwaka 1977 na misingi iliyofuatwa ni ile ya kikomunisti kama urusi na kyuba, ambayo inasema hakuna socialism nyingine zaidi ya ile itokanayo na revolution, na iongozwayo na politburo.....Tanzania haikuwa hivyo kwa ajili ya imani kwa demokrasia ya level yetu Enzi hizo, ndiyo maana ujamaa wa tz ulidharauliwa na akina samora, warusi, ethipia n.k. kwamba usingekuwa na impact kuleta maendeleo kwa maana haukuwa na mabavu ya kutosha. Nyerere hakuwa na tabia ya kuingilia mambo ya nchi za watu kama haukuleta madhara kwenye mission yake kubwa ya ukombozi. Ndiyo maana hakuwa na tabia ya kuchagua vyama vya ukombozi na aliunga mkono vyama vyote hata vyama hasimu bora tu vina lengo la kukomboa nchi zao ila hakujiingiza kwenye tofauti zao na aliacha mpaka fate iamue. Hivyo aliwaunga wafuatao; Mozambique-frelimo kwani hawakuwa na chama kingine, Afrika Kusini - ANC na PAC ( Baadhi ya wakereketwa wa ANC walimchukia Nyerere kwa hilo), Angola - MPLA, UNITA ya savimbi na FNLA ya Lobeto, Uganda timu ya obote na ile ya museveni. Kuhusu ugomvi wa samora na makanisa baki ya ukomunisti, samora alikuwa na kisasi kwa kuwa inadaiwa kuwa mapadri walikuwa wana wasalia au kuwabariki askari waendapo vitani n.k Lakini ukweli ni kwamba Mozambique ilikuwa jimbo moja wapo la ureno kwa mamia ya miaka kama Australia, NZ, USA et.c. kwa raia wa kawaida ambao kwa wazungu about 100% wakatoliki na waafrika about 90% ya wenye dini ni wakristu au wakatoliki, hawakuelewa maana ya ile vita, zaidi ya kuona kuwa lile jeshi la mreno ndiyo jeshi lao. Kwa ukatoliki, uhuru na nafasi ya kuabudu ndiyo muhimu hivyo padre akipata nafasi ya kupenyeza huduma ya kiroho atafanya iwe kwa mfungwa, gaidi, chama tawala au yoyote yule. Samora hakuona hilo akawaadhibu lakini nyerere kwa upande wake asingeacha kushirikiana na samora kwa mambo ya kitaifa kwa ajili ya tofauti zao kuhusu uelewa wao wa mambo ya kiroho kwani hiyo yaweza kuwa siyo wito wake, kwani hata tz alikuwa na marafiki wakubwa ambao spiritually misimamo yao ni tofauti na yake ndiyo maana wale wanaosema alileta MFUMO KRISTU Tanzania inabidi waione hii contradiction kwenye nchi ambayo walimsikiliza lakini hakuitumia hiyo nafasi kufurahisha hisia zake.
 

Well said mkuu wakati mwingine kung'ang'ania hizi western religious and believes ndiio maana hatuendelei

Samora aliiona hawa watu walikuja kwa kisingizio cha dini kututWala hvyo wanaweza tumia mbinu hyohyo kujipenyeza upya na ndio ilivyo sasa
 

Umejawa na chuki tu roho yako yakisuta yote haya hutak nyerere awe mtakatifu sio,hila na roho mbaya haztokusaidia subr mchakato utimie tumshangilie mtakatifu wetu Nyerere
 
Mkoloni alitumia njia nyingi kutawala so mimi simlaumu samora hivyo alikuwa anakata mizizi ya kikoloni. .halafu bro kuandika article au kitabu sio uthibitisho tosha coz alieandika alizingatia hisia zake saaana kuliko mahitaji ya mwafrika wa msumbiji
 
Hata hivyo umandika kwamba kitabu hicho kimetungwa na.............Hivyo kama kimetungwa huwez sema samora ndio alifanya hivyo tune u're mind samora hakufanya hivyo.Mungu akubariki kwa kumpenda.
 
me nadhan ww mtoa mada dini huifahamu, dhambi ni dhambi tu hakuna grades za dhambi... so ww ukisema uongo huna tofaut na hzo habar za samora machel! title yako haipo right
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…