Rais Samora Machel, alimchukiza Mungu kuliko maraisi wote Africa

ungetafakari kwanza hao wazungu unaowasifia walileta dini kwa manufaa ya nanikiasi kikubwa dini hizo zilitumika vibaya hao renamo unaowasifia waliua mamia ya wananchi wa Msumbiji pia walikuwa wanashirikiana na makaburu ambao ni wabaguzi wa rangi tena wauaji
 
Tarehe 25/12 nchini msumbiji wanasherehekea sikukuu ya familia(dia de familia) na Hii inatokana na ukweli kwamba machel alipiga marufuku kusherehekea siku Hii kama Xmas na pia alipinga mapadre kutokuoa na kuwaambia Mungu kasema tuijaze dunia Sasa ninyi hamtaki kuoa tutaijazaje mbona mnapingana na kile mnachokihubiri? Tunatakiwa tuzaane kwa wingi Ili kuziba lile gap la ndugu zetu waliokufa vitani.

Turudi kwenye Xmas kubadilishwa na kuitwa siku ya familia(dia de familia) pamoja na Samora kupigana marufuku kusherehekewa kwa siku hiyo ila raia walikuwa wameshazoea kila ifikapo tarehe hiyo walikuwa hawakubali kwenda makazini ila waliamua kukaa nyumbani na familia zao (kwa ilikuwa ngumu kwenda kanisani siku hii)ndipo walipoona nguvu ya umma imewakaba koo na kuamua kuibadilisha jina kutoka Xmas na Kuwa dia de familia,tunaidhimisha siku Hii kwa kukutana wanafamilia wote,tunakula,tunakunywa na kufurahi pamoja kifamilia Ni siku muhimu sana kwa familia kukutana ila wale ambao wana Iman na dini ya kikristo huwa wanasherehekea vitu viwili kwa siku moja(Xmas na dia de familia)
Karibuni Msumbiji.
Nalog off
 
Alikuwa anafanya jambo maana sana kutokomeza hizi dini za kigeni kwa maana nyingine alikuwa anawasaidia watu wake waondokane na slave mentality ambayo wengi wenu hadi leo mnaikumbatia mkidhani ndio njia ya kuwafikisha peponi....
 
hakupenda wakoloni
na dini ililetwa na wakoloni
sasa utapendaje mapokeo yao ilihali wao huwapendi....
ndio maana akataka kufutilia mbali nyayo zao ikiwemo dini.
 
Mwaka 1977 raisi Samora alilivamia kanisa katoliki mjini maputo akingia ndani ya kanisa akishika nyundo na kuibomoa altare kwa mikono yake miwili mpaka ikapasuka pasuka nyang'a nyang'a huku akizungukwa na masista waliokuwa wanalia na kuangalia kwa huzuni kubwa sana sana! wakiangalia kwa uchungu Siku hiyo ndipo alipolitangazia taifa la msumbiji kuwa uhuru wa kuabudu umepigwa marufuku nchini kwake akitahadhalisha kuwa" he who believe in god cannot became the member of the party-FRELIMO.

Mbali na hayo, alifunga makanisa katoliki kumi na nane kwa mpigo na kuwafunga mapadri na wanasiasa wote waliopinga uamuzi wake wa kifashisti na wa kidhalimu.

Samora alitangaza chama chashika hatamu ndani ya msumbiji, na watendaji wote walioshika nafasi nyeti za uongozi walilazimika kutokuwa na dini ili wapate ajira. Baraza lote la mawaziri pamoja na mke wake Samora na watoto wao walimkana mungu na kuchagua majina ya kienyeji.Jumapili, pasaka,Iddi, ramadhani, na xmass
, zote zilip[igwa mafuku na kufutwa.

Chini ya FRELIMO, elimu ya dini ilipigwa marufuku mashuleni na kila kijana wa miaka kumi na nne hupelekwa camp kuja kuwa mwananchama wa frelimo huku mkazo ukiwa kuikana dini yake! Kila kijana akikutwa na kitabu cha dini, rozali au kalatasi zenye maandiko ya dini yele kifungo ni miezi sita jela!

makanisa mengi na misikiti vilifungwa,Hospitali zote za Mission na taasisi zake zote,zilitaifishwa pamoja na shule zote na wataalamu wote wa kimisionari kufukuzwa au kufungwa! kwa wiki moja idadi ya madaktali 661 ilipungua hadi kufikia 60, wamisionaty wote walinyang'anywa nyumba zao, magari na walifukuzwa kazi popote walipo kitaalamu!

RENAMO ikiongozwa na Alfonso Drakama, walianzisha mapambano ya bunduki dhidi ya FRELIMO moja ya madai yao makubwa yalikuwa ni kurudisha uhuru wa wanamsumbiji wa kuabudu ambano samora alikataaa katakata akisaidiwa na majeshi ya CUBA.RENAMO walifanikiwa kidogo kuziokoa sehemu za kusini mwa msumbiji na hivyo kuja wapa watu ahueni ya kwenda kusali, kuwa na jumapili, pasaka na Xmass kurudihswa.

sasa, swali: viongozi wetu wa wamu ya kwanza , ambao walimuunga mkono Samora na sera zake zote hizo mbaya, wakimpelekea misaada ya kijeshi, pesa na wataalamu wa propaganda, je wanastahili kuitwa watakatifu?

Source:Ripoti ya balozi wa UN nchini msumbiji mwaka 1977. ambayo ipo katika kitabu kiitwacho: Ronald Reagan in his own hand. Kilichotungwa na Kiron K skinner, Anelise Anderson na Martin Anderson.

Ukienda bookshop yeyote pale Tanzania wape tittle hiyo na kama hawana basi watakuagizia.

My take: naomba sana balaza la maaskofu katoliki tanzania wakisome kitabu hichi page183-194, halafu wajiulize kwa nini viongozi wetu wa awwawamu ya kwanza walimuunga mkono samora huku akiwa na sera chafu za kufuta dini zote za kiislamu na kikristo nchini mwake. halafu watuelezee umma, utakatifu maana yake ni nini?

Wakomunist wote walikuwa waovu mno. Kuna mwingne ambaye vijana wa kileo wanapenda sana picha yake anaitwa Cheguevara naye alipiga marufuku dini huko Cuba na kupambana kuhakikisha uhuru wa kuabudu na imani kwa Mungu inakufa.

Ajabu ni kwamba yy leo anaonekana shujaa mbele ya ulimwengu. Hapo ndipo naamini shetani ni Bwana wa huu Ulimwengu.
 
Wawaulize kwanza wakoloni, kwanini walitumia dini vibaya kuwanyanyasa na kuwapeleka watu utumwani. Yeye alikua anapambana na mkoloni aliekua anajificha nyuma ya dini (Kama mkoloni mpya wa mashariki ya kati anavyojificha ndani ya misikiti na kutumia kinywa cha Lipumba na Ponda)

Hutafika popote na kampeni zenu za kumchafua Nyerere!
Wareno ni Wakatoliki kama ilivyo Kiswahili na Mswahili. Samora kuchukia Ukatoliki ninadhani ilichangiwa na yale mateso waliyoyapata kutoka kwa Wareno haswa wakati wa kupigania uhuru.
 
Mwaka 1977 raisi Samora alilivamia kanisa katoliki mjini maputo akingia ndani ya kanisa akishika nyundo na kuibomoa altare kwa mikono yake miwili mpaka ikapasuka pasuka nyang'a nyang'a huku akizungukwa na masista waliokuwa wanalia na kuangalia kwa huzuni kubwa sana sana! wakiangalia kwa uchungu Siku hiyo ndipo alipolitangazia taifa la msumbiji kuwa uhuru wa kuabudu umepigwa marufuku nchini kwake akitahadhalisha kuwa" he who believe in god cannot became the member of the party-FRELIMO.

Mbali na hayo, alifunga makanisa katoliki kumi na nane kwa mpigo na kuwafunga mapadri na wanasiasa wote waliopinga uamuzi wake wa kifashisti na wa kidhalimu.

Samora alitangaza chama chashika hatamu ndani ya msumbiji, na watendaji wote walioshika nafasi nyeti za uongozi walilazimika kutokuwa na dini ili wapate ajira. Baraza lote la mawaziri pamoja na mke wake Samora na watoto wao walimkana mungu na kuchagua majina ya kienyeji.Jumapili, pasaka,Iddi, ramadhani, na xmass
, zote zilip[igwa mafuku na kufutwa.

Chini ya FRELIMO, elimu ya dini ilipigwa marufuku mashuleni na kila kijana wa miaka kumi na nne hupelekwa camp kuja kuwa mwananchama wa frelimo huku mkazo ukiwa kuikana dini yake! Kila kijana akikutwa na kitabu cha dini, rozali au kalatasi zenye maandiko ya dini yele kifungo ni miezi sita jela!

makanisa mengi na misikiti vilifungwa,Hospitali zote za Mission na taasisi zake zote,zilitaifishwa pamoja na shule zote na wataalamu wote wa kimisionari kufukuzwa au kufungwa! kwa wiki moja idadi ya madaktali 661 ilipungua hadi kufikia 60, wamisionaty wote walinyang'anywa nyumba zao, magari na walifukuzwa kazi popote walipo kitaalamu!

RENAMO ikiongozwa na Alfonso Drakama, walianzisha mapambano ya bunduki dhidi ya FRELIMO moja ya madai yao makubwa yalikuwa ni kurudisha uhuru wa wanamsumbiji wa kuabudu ambano samora alikataaa katakata akisaidiwa na majeshi ya CUBA.RENAMO walifanikiwa kidogo kuziokoa sehemu za kusini mwa msumbiji na hivyo kuja wapa watu ahueni ya kwenda kusali, kuwa na jumapili, pasaka na Xmass kurudihswa.

sasa, swali: viongozi wetu wa wamu ya kwanza , ambao walimuunga mkono Samora na sera zake zote hizo mbaya, wakimpelekea misaada ya kijeshi, pesa na wataalamu wa propaganda, je wanastahili kuitwa watakatifu?

Source:Ripoti ya balozi wa UN nchini msumbiji mwaka 1977. ambayo ipo katika kitabu kiitwacho: Ronald Reagan in his own hand. Kilichotungwa na Kiron K skinner, Anelise Anderson na Martin Anderson.

Ukienda bookshop yeyote pale Tanzania wape tittle hiyo na kama hawana basi watakuagizia.

My take: naomba sana balaza la maaskofu katoliki tanzania wakisome kitabu hichi page183-194, halafu wajiulize kwa nini viongozi wetu wa awwawamu ya kwanza walimuunga mkono samora huku akiwa na sera chafu za kufuta dini zote za kiislamu na kikristo nchini mwake. halafu watuelezee umma, utakatifu maana yake ni nini?

Ndugu, naona kusoma kwako kitabu hicho kumekufanya uhitimishe kuwa ukweli umo humo....haina maana vitabu vyote vina ukweli vingine huandikwa kwa ajili ya kuwapaka wahusika matope. Sio kuwa haiwezekani Samora kufanya hivyo lakini tupate hizo habari kutoka vyanzo vingine vingi tofauti ili kupata ushaidi Zaidi kabla hatujaanza kuchangia hii mada.
 
Wakomunist wote walikuwa waovu mno. Kuna mwingne ambaye vijana wa kileo wanapenda sana picha yake anaitwa Cheguevara naye alipiga marufuku dini huko Cuba na kupambana kuhakikisha uhuru wa kuabudu na imani kwa Mungu inakufa.

Ajabu ni kwamba yy leo anaonekana shujaa mbele ya ulimwengu. Hapo ndipo naamini shetani ni Bwana wa huu Ulimwengu.
Weeeeee unahakika na ulichosema hapo kuhusu Che...?????!!!
 
Back
Top Bottom