Rais Samora Machel, alimchukiza Mungu kuliko maraisi wote Africa

ungetafakari kwanza hao wazungu unaowasifia walileta dini kwa manufaa ya nanikiasi kikubwa dini hizo zilitumika vibaya hao renamo unaowasifia waliua mamia ya wananchi wa Msumbiji pia walikuwa wanashirikiana na makaburu ambao ni wabaguzi wa rangi tena wauaji
 
Alikuwa ni mtu wa kipekee sana asiye mwoga wa Wazungu!
 
Tarehe 25/12 nchini msumbiji wanasherehekea sikukuu ya familia(dia de familia) na Hii inatokana na ukweli kwamba machel alipiga marufuku kusherehekea siku Hii kama Xmas na pia alipinga mapadre kutokuoa na kuwaambia Mungu kasema tuijaze dunia Sasa ninyi hamtaki kuoa tutaijazaje mbona mnapingana na kile mnachokihubiri? Tunatakiwa tuzaane kwa wingi Ili kuziba lile gap la ndugu zetu waliokufa vitani.

Turudi kwenye Xmas kubadilishwa na kuitwa siku ya familia(dia de familia) pamoja na Samora kupigana marufuku kusherehekewa kwa siku hiyo ila raia walikuwa wameshazoea kila ifikapo tarehe hiyo walikuwa hawakubali kwenda makazini ila waliamua kukaa nyumbani na familia zao (kwa ilikuwa ngumu kwenda kanisani siku hii)ndipo walipoona nguvu ya umma imewakaba koo na kuamua kuibadilisha jina kutoka Xmas na Kuwa dia de familia,tunaidhimisha siku Hii kwa kukutana wanafamilia wote,tunakula,tunakunywa na kufurahi pamoja kifamilia Ni siku muhimu sana kwa familia kukutana ila wale ambao wana Iman na dini ya kikristo huwa wanasherehekea vitu viwili kwa siku moja(Xmas na dia de familia)
Karibuni Msumbiji.
Nalog off
 
Alikuwa anafanya jambo maana sana kutokomeza hizi dini za kigeni kwa maana nyingine alikuwa anawasaidia watu wake waondokane na slave mentality ambayo wengi wenu hadi leo mnaikumbatia mkidhani ndio njia ya kuwafikisha peponi....
 
hakupenda wakoloni
na dini ililetwa na wakoloni
sasa utapendaje mapokeo yao ilihali wao huwapendi....
ndio maana akataka kufutilia mbali nyayo zao ikiwemo dini.
 


Wakomunist wote walikuwa waovu mno. Kuna mwingne ambaye vijana wa kileo wanapenda sana picha yake anaitwa Cheguevara naye alipiga marufuku dini huko Cuba na kupambana kuhakikisha uhuru wa kuabudu na imani kwa Mungu inakufa.

Ajabu ni kwamba yy leo anaonekana shujaa mbele ya ulimwengu. Hapo ndipo naamini shetani ni Bwana wa huu Ulimwengu.
 
Wareno ni Wakatoliki kama ilivyo Kiswahili na Mswahili. Samora kuchukia Ukatoliki ninadhani ilichangiwa na yale mateso waliyoyapata kutoka kwa Wareno haswa wakati wa kupigania uhuru.
 

Ndugu, naona kusoma kwako kitabu hicho kumekufanya uhitimishe kuwa ukweli umo humo....haina maana vitabu vyote vina ukweli vingine huandikwa kwa ajili ya kuwapaka wahusika matope. Sio kuwa haiwezekani Samora kufanya hivyo lakini tupate hizo habari kutoka vyanzo vingine vingi tofauti ili kupata ushaidi Zaidi kabla hatujaanza kuchangia hii mada.
 
Weeeeee unahakika na ulichosema hapo kuhusu Che...?????!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…