field marshall1
JF-Expert Member
- Sep 17, 2017
- 1,171
- 2,732
Uongo umeshakuwa kitu cha kawaida katika nchi yetu, Serikali yetu haikuwahi kuaminika na itaendelea kutoaminika.
Rais si mkweli, mbabe, ukandamizaji wa haki za raia, matumizi mabaya ya madaraka, matumizi mabaya ya fedha za umma (Bado tunadaiwa mabilioni kama siyo matrillioni ya shillingi kutokana na tabia yake ya kukosa uvumilivu na kuvunja mikataba ovyo ovyo).
Mawaziri hawasemi ukweli kuanzia kwenye ukuaji wa uchumi hadi kwenye elimu ndiyo maana unasikia siku hizi tamko linatolewa halafu linafutwa utadhani linafanywa na watoto wa darasa la kwanza! Tunaambiwa uchumi unakua....kivipi? Bank ya dunia imeshasema haukui kama jinsi ilivyotabiriwa (Projected) serikali inasema unakuwa kwa 7.2% World Bank wanasema unakua chini ya 6.6% na ni sekta moja ya ujenzi ndiyo unakua kwingine kote hakuna ukuaji...hivyo hakuna uwiano wa ukuaji na wakifanya uchunguzi kwenye quarter hii inayokuja uchumi wetu unaweza ukawa umekuwa kwa asilimia chini ya 5.
Kwenye elimu huko nako wanajichanganya....ni propaganda tupu. Huyu waziri haeleweki anafanya nini? Anachofanya kwa ufanisi ni kuvifunga Vyuo vikuu badala ya kuvisaidia ili vikue....yeye anakomesha tu, Wahitimu wa darasa la saba wengi kwa malaki waliofaulu wamekosa nafasi ya kuingia kidato cha kwanza.....wanafunzi hawa watakuwa mitaani wakipigana vikumbo na wanafunzi wa vyuo vikuu binafsi na wa vyuo vya kati, na vya waalimu waliomaliza ambao hawana ajira kwa miaka mitatu sasa, TUMEAMBIWA HAKUNA KUAJIRI SASA HADI KIBALI KITAKAPOTOLEWA NA SASA IMESHAPITA MIAKA MITATU na hakuna mpango wa kuwasaidia, Hawa wahitimu watakaa bila kazi kwa miaka yote hii?
Serikali ikiambiwa hilo ni bomu linalosubiri kupasuka wanaanza kukamata hao wanaowakumbusha wajibu wao! Gavana wa benki kuu yeye kazi yake kufunga Mabenki badala ya kuyasaidia ili yakue yaweze kuwafikia wananchi hadi wa vijijini...... Gavana hana elimu ya fedha, alikuwa mwalimu wangu pale Mlimani.
Waziri wa Fedha anasema hali itakuwa ngumu kwa kuwa wafadhali wamepunguza misaada.....Hivi kweli kupunguza misaada tu kunaweza kufanya hali ikawa mbaya hivi? Hapo bado hawajakata misaada yote! Mbona tuliambiwa tunafanya miradi kwa PESA ZETU WENYEWE! Rais kasema kwa msisitizo kuwa pesa zipo sasa waziri anaongea nini? Mpango anatuambia kuwa masharti tuliyopewa ni kukubaliana na ushoga kitu ambacho si ukweli.......SHAME ON WAZIRI MPANGO!
Mbona kuna mambo kumi na tano (15) hataki kuyasema....anaona hilo moja la ushoga tu? Hata hilo la ushoga kama anavyosema huyo waziri halilazimishi nchi kuwatambua mashoga bali linataka lisivunje haki zao za msingi kama kuwakamata na kuwafunga....Mbona Makonda alitajwa? Hiyo sheria ya kuwakamata washukiwa wa ushoga inavunja haki za msingi za binadamu.
Kila waziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wanaropoka angalau waonekane na Magufuli huku wananchi wakiumia.
Mkuu wa majeshi inaonekana naye ana taaluma ndogo (semi-illiteracy) anaingilia mambo ya polisi na mahakama wakati kazi ya jeshi inafahamika ni kulinda mipaka yetu siyo kusimamia ununuzi wa korosho, anafanywa mjinga na rais wake, jeshi linashushwa hadhi limekuwa la propaganda, Juzi akiongea bila aibu amesema jeshi letu kwa ubora ni la 27 duniani.....NI KWA UBORA UPI?
Jeshi hili lenye obsolete equipments kama ndege za mwaka 1965 za shenyang J-6 na J-7 ambazo hazitumiki tena duniani zipo kwenye museum, au helicopters (Eurocopters, bells)ambazo siyo "gunship" kwa strength tupo namba 98 na 99 kwa ubora, level moja na Sudan kusini, tumeshindwa na majirani zetu isipokuwa Burundi tu.
Mkuu wa majeshi kudanganya hakusaidii sana....uwe mkweli acha habari za kuokoteza au hisia zako.....Tafuta facts la sivyo utajiabisha na kuaibisha nchi yetu.
Mkuu wa polisi na polisi wake hawa ndiyo maarufu kwa kudanganya ila uwongo wao hauna akili hata kidogo....Hilo la MO Dewji limewaondolea heshima, utekaji feki mlioufanya hata kwenye michezo ya katuni ya watoto haupo.....Ahsanteni sana kwa kutupa moyo kuwa watekaji wa MO walimrudisha salama na bunduki zao.....HILO LINAWEZEKANA TANZANIA TU! Mmetuaminisha kuwa watekaji hao ni watu wema sana na wameshaacha uhalifu.....Vipi kuhusu vidole vyao (Fingerprints zao kwenye bunduki na kwenye hilo gari fake?) mmeshazipata? Mmetuacha hoi na hiyo CCTV zenu............Hongereni sana!
Makonda aliwaona wazungu wawili ila walibadilika baadaye wakawa wa- South Africa weusi......Kweli hiyo Bongo movie ni kali.
Tanzania tunarudi nyuma miaka 50. kwa uongozi huu wa Magufuli na wasaidizi wake.