Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 1,679
- 2,123
Mdogo, mdogo, mambo yaliyotabiriwa na kuandikwa kwenye Biblia yanazidi kutimia. Katika kitabu cha 2 Timotheo 3:1-17 BHN imeandikwa hivi:
"Kumbuka kwamba, katika siku za mwisho kutakuwa na nyakati za taabu. Watu watakuwa na ubinafsi, wenye tamaa ya fedha, wenye majivuno, wenye kujiona, wenye kumtukana Mungu, wasiowatii wazazi wao, wasio na shukrani na waovu; watatokea watu wasio na upendo moyoni, wasio na huruma, wachongezi, walafi na wakali; watachukia chochote kilicho chema; watakuwa wahaini, wakaidi na waliojaa kiburi; watapenda anasa kuliko kumpenda Mungu. Kwa nje wataonekana kama watu wenye kumcha Mungu, lakini wataikana nguvu yake."
Kitendo cha Rais Donald Trump kutoa agizo la kusitisha misaada ambayo Marekani ilikuwa ikitoa kwa nchi mbalimbali, kinatimiza unabii huo(watu watakuwa na ubinafsi).
Kitendo cha Rais Trump kutaka kusaini kwanza mikataba ya madini Ukraine na DRC ndio misaada ya ulinzi itolewe kinatimiza unabii huo(wenye tamaa ya fedha).
Kitendo cha Rais Trump kumnenea Rais Zelensky maneno yaliyomfanya anyong'onyee, kinatimiza unabii huo(wenye majivuno, wenye kujiona).
Hakika hizi ni siku za mwisho. Yesu amekaribia kuja. Hatuijui siku wala saa, lakini tukeshe kwa kuishi maisha matakatifu; maana kwa siku na saa tusiyodhani Yesu atakuja kuwanyakua wanaomwamini tu na kuwapeleka mbinguni. Watakaoachwa watabaki kwenye dhiki kuu ambayo haijawahi kutokea tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Habari za dhiki hiyo kuu zimeandikwa katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana.
Let all endowed with the faculty of hearing perceive and discern.