Rais Trump Ametimiza Tena Unabii Mwingine!!

Turampu ana miaka minne tu, mambo yatarejea kama kawaida.

Hakuna unabii, hiyo ni coincidence tu.
 
TAFUTENI ZA KWENU KAMA TAIFA...UNALETA LETA LIA LIA YA UMASKN HAPA ILI IWEJE?
UNADHANI MISAADA NI BARAKA?
 
Mkuu sio kweli kwenye swala la misaada hapo. Tatizo mtu akisaidiwa kwa muda mrefu anaanza kuona kuwa hiyo misaada ni haki yake. Kwa sasa yeye na serikali yake wameamua hizo fedha za walipa kodi wa Marekani zitumike kuinufaisha Marekani kwanza, halafu wewe umekaa kulalamika na tafsiri za Biblia ambazo sio halisi. Tuache utegemezi, maamuzi ya Trump ni wito kwetu kuamka kutoka usingizini. Mtegemea cha nduguye hufa masikini.
 
Hapa cha msingi watu waache ngono over. Hakuna cha Nuhu wala gharika.
 
Point yangu hapo ni kwamba dalili hizo zinaendana na dalili nyingine alizotaja Yesu za kuja kwake ambazo tayari pia zimetimia. Kwa mfano pestilences(magonjwa mabaya kama Covid-19), kuongezeka kwa maasi(angalia habari za vita na machafuko Africa), kuongezeka kwa maarifa(angalia jinsi maarifa ya AI yalivyobadili maisha ndani ya muda mfupi).

Wakati wa Nuhu watu waliambiwa hivihivi kutakuwa na gharika wakamcheka Nuhu, mwisho wa siku wakarambwa na maji.
 
Kwamba Ubinafsi huu wa leo wa kina Trump ni mkubwa na wa hatari kuliko wa enzi za kina Karl Peters ? Mbona hizo siku za mwisho zitakuwa zilianza zamani sana ?

The only new thing in this world is the history you do not know...
 
Je, unaweza ukanitajia mfano wa Ushoga wa nyakati za sasa ambao unazidi ule uovu wa sodoma na Gomola?
Tofauti ya ushoga wa sasa na ule wa enzi za Sodoma na Gomora ni kwamba dhambi hiyo ambayo zamani ilifanywa kwa siri, sasa hivi imehalalishwa waziwazi na hata kushinikizwa ikubalike kama jambo la kawaida. Leo, ushoga haupo tu kama dhambi ya mtu binafsi bali unalindwa kisheria, unafundishwa shuleni kwa watoto, na hata kuingizwa katika taasisi za kidini. Leo hii video za ushoga zinaonyeshwa kwenye mitandao ya kijamii bila kificho. Hii inaashiria ongezeko la uovu unaozidi ule wa Sodoma na Gomora.
 
Kitendo cha Rais Donald Trump kutoa agizo la kusitisha misaada ambayo Marekani ilikuwa ikitoa kwa nchi mbalimbali, kinatimiza unabii huo(watu watakuwa na ubinafsi).
Wewe ni maskini wa akili, msaada sio lazima, ni hisani tu. Lawama unazipeleka sehemu sio sahihi. Na kutumia andiko kuhalalisha umaskini ni umaskini*2.
 
Kwamba Ubinafsi huu wa leo wa kina Trump ni mkubwa na wa hatari kuliko wa enzi za kina Karl Peters ? Mbona hizo siku za mwisho zitakuwa zilianza zamani sana ?

The only new thing in this world is the history you do not know...
Nimetoa tu mfano wa Trump. Lakini Trump anawakilisha idadi kubwa ya watu. Enzi za kina Karl Peters, wenye ubinafsi hawakuwa wengi kama leo. Siasa za Ujamaa kwa mfano zilipinga ubinafsi. Leo hii nani anazungumzia tena ujamaa?
 
Na kutumia andiko kuhalalisha umaskini ni umaskini*2.
Hujasoma Mathayo 26:11?
Maskini mtakuwa nao siku zote...

Maneno hayo Yesu aliyasema kusisitiza umuhimu wa kuwasaidia maskini.
Umaskini upo na utakuwepo mpaka Yesu anarudi. Hivyo kama Mungu amekubariki na hutaki kuwasaidia maskini maana yake ni kwamba unatimiza unabii. "Siku za mwisho watu watakuwa na ubinafsi, watajipenda wenyewe..."
 

Kumbe ukiacha kutumia chatgpt, akili zinarudi
 
Huyo hamna kitu
 
Amina mtumishi. ubarikiwe na Bwana, Bwana Yesu.
 
Kwenye upande wa USAID wameeleza baadhi ya pesa nyingi zilivyokuwa zinatumika vibaya.... Kusupport Ushoga, kusapport baadhi ya vikundi vya ugaidi, kusupport tafiti mbalimbali za bioweapons, rushwa kubwa kubwa, matumizi mabaya etc.... Sasa hapo unataka kusemaje?? Ngoja nitafute ile clip ya ripoti ya DOGE....

DOGE yaweka hadharani vikundi vya magaidi vilivyokuwa vinafadhiliwa na USAID
 

Attachments

  • Screenshot_20250224-075424_X.jpg
    365.2 KB · Views: 1
  • 1741956299594.jpg
    738.8 KB · Views: 0
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…