Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Ndugu zangu, habari ya mjini ndio hii. Kiongozi mwenye mamlaka makubwa ya kidini nchini Israeli ametamka wazi mbele ya Rais Trump kuwa Waisraeli wanajiandaa kujenga hekalu la tatu, kubwa, mjini Yerusalemu. Ujenzi wa hekalu la tatu ni hatua muhimu sana kwa Waisraeli katika maandalizi ya kumpokea Masihi wao. Kwa imani ya Wayahudi, ni lazima kwanza wajenge hekalu la tatu kabla ya ujio wa Masihi wao na kwamba hekalu hilo litarudisha ibada ya dhabihu na uwepo wa Mungu katikati yao, kama ilivyokuwa zamani. Je hekalu la tatu litajengwa katika eneo gani Israeli? 'Tega masikio' kwa makini.
Hekalu la kwanza la Wana wa Israeli lilijengwa mjini Yerusalemu, katika eneo la Mlima Moria. Hili ndilo hekalu ambalo Mfalme Sulemani alilijenga kwa agizo la Mungu(1 Flm 6:1-38; 2 Nyk 3:1). Eneo hili linahusiana na eneo ambalo Ibrahimu alitaka kumtoa Isaka kuwa sadaka (Mwanzo 22:2). Hekalu hili lilibomolewa na Wababeli mwaka 586 KK chini ya Mfalme Nebukadneza. Hekalu la pili lilijengwa katika eneo hilohilo la Mlima Moria mjini Yerusalemu wakati Wayahudi waliporudi kutoka uhamishoni Babeli. Kazi ya ujenzi ilikamilika mwaka 516 KK (Ezra 6:15). Hekalu hili liliharibiwa tena na Warumi mwaka 70 BK.
Waisraeli wanaamini kuwa Hekalu la Tatu litajengwa katika eneo hilohilo la Mlima Moria, Yerusalemu, ambapo mahekalu mawili ya kwanza yalikuwepo. Kwa sasa, eneo hilo lina Msikiti wa Al-Aqsa na “Dome of the Rock.” “Dome of the Rock” inaheshimiwa na Waislamu kwa kuwa imejengwa katika eneo hilo linalotambulika kuwa ni eneo la tatu takatifu katika Uislamu baada ya Mecca and Medina. Katika eneo hilo ndipo Wayahudi wanapotaka kujenga hekalu la tatu! Asomaye na afahamu!
Maandalizi ya kujenga hekalu la tatu katika eneo hilo “almost” yamekamilika. Kilichokuwa kinasubiriwa zaidi ni ndama wekundu(red heifers). Kulingana na Torati (Hesabu 19:2-10), ndama mwekundu anahitajika kwa ajili ya ibada ya utakaso wa kuhani kabla ya huduma kuanza katika hekalu.
Waisraeli wengi bado hawaamini kuwa Yesu Kristo aliyekuja takriban miaka 2000 iliyopita ndiye Masihi wao. Sababu kuu ni kwamba walitarajia Masihi atakayewakomboa kisiasa na kuwarudishia ufalme wa Daudi (Yohana 6:15, Luka 24:21). Yesu, badala yake, alikuja kama Masihi wa kiroho, kuleta msamaha wa dhambi na wokovu kwa kila aaminiye(Yn 3:16). Kwahiyo kwa Waisraeli wengi, Masihi waliyemtarajia bado hajaja. Lakini kwa sasa wanaamini kuwa anakaribia kuja kutokana na ishara wanazoziona.
Ingawa Waisraeli wengi kwa sasa hawaamini kwamba Yesu aliyekuja ndiye Masihi, Mungu atawakomboa sawasawa na Warumi 11:25-26.
"Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msijue siri hii, msije mkajiona wenye akili; ya kwamba ugumu kwa sehemu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa utakapowasili. Hivyo Israeli wote wataokolewa, kama ilivyoandikwa, Mkombozi atatoka Sayuni, atamwondolea Yakobo maasia yake." (Warumi 11:25-26). Andiko hili linahusiana na unabii wa Isaya 59:20-21, unaosema: "Mkombozi atakuja Sayuni, kwa wale wa Yakobo waachao maasi yao, asema Bwana." Pia, Nabii Zekaria katika Zek 12:10 anatabiri kuwa siku inakuja ambapo Waisraeli watamtambua Yesu kuwa ni Masihi wao: "Nami nitamimina roho ya neema na kuomba...juu ya wenyeji wa Yerusalemu; nao watamtazama yeye waliyemchoma, nao watamwombolezea..."
Kwa Wakristo, maandalizi hayo ni dalili muhimu za nyakati za mwisho kama alivyotabiri Yesu. Kwa hiyo, tunapaswa kuwa macho na kujiandaa kiroho kwa ujio wa Bwana wetu Yesu Kristo. Mungu atusaidie tukeshe kama wale wanawali watano wenye busara(Mt 25:1-13). Amen.
Kwa habari zaidi tazama:
View: https://youtu.be/Puh80LhMJiY?si=9Bz9ygu0Mm0T0l-C