Rais Trump ashuhudia maandalizi makubwa ya kumpokea Masihi, nchini Israeli !!

Labda imani yao iko sahihi? Duh!!
Wanaemuomgelea hapo ni Yesu huyo huyo, Kwa wali kiroho wanaelewa Trump hajachaguliwa tu km watu wanavyodhani ,Mungu Yuko kazini Ili baadhi ya nabii zitimie sio coincidence
Trump it's a sign to this end times..
Hata ye kutumika kuufanya Jerusalem kuwa makao makuu watu wanafikiria imetokea tu !
No ana ana assignment ukiacha mambo yao ya siasa

Hapo ni sehemu qmbayo hawa wapuuzi walipora wakajenga mavitu yao SS itarudi kwa wahusika na patajenfwa hekaou la 3 ,ila muda Bado ni maandalizi ti hayo
 
Hii habari ni muhimu sana kuisoma na kuielewa, nahitaji kujua Trump ni muumini wa ukristo ambao wayahudi awautambui, sasa itakuwaje?
Njia za Mungu sio za mwanadamu. Mungu anaweza kumtumia mtu yeyote kutimiza mapenzi yake.

Unakumbuka Pilato alivyosema: "Niliyoandika, nimeyaandika" katika Yohana 19:22? Pilato alikuwa anawajibu Mafarisayo waliotaka abadilishe maandishi juu ya msalaba wa Yesu. Hiyo ilikuwa ni baada ya Pilato kuandika juu ya msalaba wa Yesu maneno: "Yesu wa Nazareti, Mfalme wa Wayahudi" (Yohana 19:19). Mafarisayo wakataka ayabadilishe, lakini Pilato alikataa. Pilato hakuwa mfuasi wa Yesu lakini alitumiwa kueleza ukweli kwamba Yesu ni Mfalme.
 
Dome of the Rock.jpg

Jews believe this site is meant for the Third Temple, yet the Dome of the Rock remains—will the temple ever rise again?
 
Ndugu zangu, habari ya mjini ndio hii. Kiongozi mwenye mamlaka makubwa ya kidini nchini Israeli ametamka wazi mbele ya Rais Trump kuwa Waisraeli wanajiandaa kujenga hekalu la tatu, kubwa, mjini Yerusalemu. Ujenzi wa hekalu la tatu ni hatua muhimu sana kwa Waisraeli katika maandalizi ya kumpokea Masihi wao. Hekalu la kwanza lilijengwa na Sulemani na kuharibiwa na Wababeli mwaka 586 KK, na la pili lilijengwa upya lakini likabomolewa na Warumi mwaka 70 BK. Kwa imani ya Wayahudi, ni lazima kwanza wajenge hekalu la tatu kabla ya ujio wa Masihi wao na kwamba hekalu la tatu litarudisha ibada ya dhabihu na uwepo wa Mungu katikati yao, kama ilivyokuwa zamani. Je hekalu la tatu litajengwa katika eneo gani Israeli? 'Tega masikio' kwa makini.

Hekalu la kwanza la Wana wa Israeli lilijengwa mjini Yerusalemu, katika eneo la Mlima Moria. Hili ndilo hekalu ambalo Mfalme Sulemani alilijenga kwa agizo la Mungu(1 Flm 6:1-38; 2 Nyk 3:1). Eneo hili linahusiana na eneo ambalo Ibrahimu alitaka kumtoa Isaka kuwa sadaka (Mwanzo 22:2). Hekalu hili lilibomolewa na Wababeli mwaka 586 KK chini ya Mfalme Nebukadneza. Hekalu la pili lilijengwa katika eneo hilohilo la Mlima Moria mjini Yerusalemu wakati Wayahudi waliporudi kutoka uhamishoni Babeli. Kazi ya ujenzi ilikamilika mwaka 516 KK (Ezra 6:15). Hekalu hili liliharibiwa tena na Warumi mwaka 70 BK.

Waisraeli wanaamini kuwa Hekalu la Tatu litajengwa katika eneo hilohilo la Mlima Moria, Yerusalemu, ambapo mahekalu mawili ya kwanza yalikuwepo. Kwa sasa, eneo hilo lina Msikiti wa Al-Aqsa na “Dome of the Rock.” “Dome of the Rock” inaheshimiwa na Waislamu kwa kuwa imejengwa katika eneo hilo linalotambulika kuwa ni eneo la tatu takatifu katika Uislamu baada ya Mecca and Medina. Katika eneo hilo ndipo Wayahudi wanapotaka kujenga hekalu la tatu! Asomaye na afahamu!

Maandalizi ya kujenga hekalu la tatu katika eneo hilo “almost” yamekamilika. Kilichokuwa kinasubiriwa zaidi ni ndama wekundu(red heifers). Kulingana na Torati (Hesabu 19:2-10), ndama mwekundu anahitajika kwa ajili ya ibada ya utakaso wa kuhani kabla ya huduma kuanza katika hekalu.

Waisraeli wengi bado hawaamini kuwa Yesu Kristo aliyekuja takriban miaka 2000 iliyopita ndiye Masihi wao. Sababu kuu ni kwamba walitarajia Masihi atakayewakomboa kisiasa na kuwarudishia ufalme wa Daudi (Yohana 6:15, Luka 24:21). Yesu, badala yake, alikuja kama Masihi wa kiroho, kuleta msamaha wa dhambi na wokovu kwa kila aaminiye(Yn 3:16). Kwahiyo kwa Waisraeli wengi, Masihi waliyemtarajia bado hajaja. Lakini kwa sasa wanaamini kuwa anakaribia kuja kutokana na ishara wanazoziona.

Ingawa Waisraeli wengi kwa sasa hawaamini kwamba Yesu aliyekuja ndiye Masihi, Mungu atawakomboa sawasawa na Warumi 11:25-26.
"Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msijue siri hii, msije mkajiona wenye akili; ya kwamba ugumu kwa sehemu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa utakapowasili. Hivyo Israeli wote wataokolewa, kama ilivyoandikwa, Mkombozi atatoka Sayuni, atamwondolea Yakobo maasia yake." (Warumi 11:25-26). Andiko hili linahusiana na unabii wa Isaya 59:20-21, unaosema: "Mkombozi atakuja Sayuni, kwa wale wa Yakobo waachao maasi yao, asema Bwana." Pia, Nabii Zekaria katika Zek 12:10 anatabiri kuwa siku inakuja ambapo Waisraeli watamtambua Yesu kuwa ni Masihi wao: "Nami nitamimina roho ya neema na kuomba...juu ya wenyeji wa Yerusalemu; nao watamtazama yeye waliyemchoma, nao watamwombolezea..."

Kwa Wakristo, maandalizi hayo ni dalili muhimu za nyakati za mwisho kama alivyotabiri Yesu. Kwa hiyo, tunapaswa kuwa macho na kujiandaa kiroho kwa ujio wa Bwana wetu Yesu Kristo. Mungu atusaidie tukeshe kama wale wanawali watano wenye busara(Mt 25:1-13). Amen.
Kwa habari zaidi tazama:
View: https://youtu.be/Puh80LhMJiY?si=9Bz9ygu0Mm0T0l-C

Kwa hiyo masihi wao ni nani
 
makaafiri babu zako, kenge wewe.
Mtu akikutukana, usimrudishie tusi. Kutukana ni dhambi inayoweza kumfanya mtu akose kuurithi ufalme wa Mungu. Soma 1 Wakorintho 6:9-10 imeandikwa hivi:
Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wezi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.
 
Maombi ya Amida(Amida prayer) ni sehemu muhimu ya sala ya Wayahudi. Sala au maombi hayo hufanyika mara tatu kwa siku watu wakiwa wamesimama kuelekea Yerusalemu. Maneno yafuatayo yamo katika sala hiyo. Ni maneno ya kumuomba Masihi aje Yerusalemu aishi katika mji huo kama alivyoahidi na afanikishe ujenzi wa hekalu la tatu upesi na kuweka kiti cha enzi cha Daudi:
הַשֵּׁב שְׁכִינָתְךָ לְצִיּוֹן עִירֶךָ, וְתִבְנֶה אוֹתָהּ בְּקָרוֹב בְּיָמֵינוּ בִּנְיַן עוֹלָם, וְכִסֵּא דָוִד מְהֵרָה לְתוֹכָהּ תָּכִין.
(Transliteration):
"Hashiv Shekhinat’cha l’Tziyon irekha, v’tivneha b’karov b’yameinu binyan olam, v’kisei David meheira l’tocha tachin."
Return in mercy to Your city, Jerusalem, and dwell therein as You have promised. Rebuild it soon in our days as an everlasting structure, and speedily set up in it the throne of David
View attachment 3276599
Wayahudi wakisali maombi ya Amida
Mbona wana bharagashia kichwani?
 
Ndugu zangu, habari ya mjini ndio hii. Kiongozi mwenye mamlaka makubwa ya kidini nchini Israeli ametamka wazi mbele ya Rais Trump kuwa Waisraeli wanajiandaa kujenga hekalu la tatu, kubwa, mjini Yerusalemu. Ujenzi wa hekalu la tatu ni hatua muhimu sana kwa Waisraeli katika maandalizi ya kumpokea Masihi wao. Kwa imani ya Wayahudi, ni lazima kwanza wajenge hekalu la tatu kabla ya ujio wa Masihi wao na kwamba hekalu hilo litarudisha ibada ya dhabihu na uwepo wa Mungu katikati yao, kama ilivyokuwa zamani. Je hekalu la tatu litajengwa katika eneo gani Israeli? 'Tega masikio' kwa makini.

Hekalu la kwanza la Wana wa Israeli lilijengwa mjini Yerusalemu, katika eneo la Mlima Moria. Hili ndilo hekalu ambalo Mfalme Sulemani alilijenga kwa agizo la Mungu(1 Flm 6:1-38; 2 Nyk 3:1). Eneo hili linahusiana na eneo ambalo Ibrahimu alitaka kumtoa Isaka kuwa sadaka (Mwanzo 22:2). Hekalu hili lilibomolewa na Wababeli mwaka 586 KK chini ya Mfalme Nebukadneza. Hekalu la pili lilijengwa katika eneo hilohilo la Mlima Moria mjini Yerusalemu wakati Wayahudi waliporudi kutoka uhamishoni Babeli. Kazi ya ujenzi ilikamilika mwaka 516 KK (Ezra 6:15). Hekalu hili liliharibiwa tena na Warumi mwaka 70 BK.

Waisraeli wanaamini kuwa Hekalu la Tatu litajengwa katika eneo hilohilo la Mlima Moria, Yerusalemu, ambapo mahekalu mawili ya kwanza yalikuwepo. Kwa sasa, eneo hilo lina Msikiti wa Al-Aqsa na “Dome of the Rock.” “Dome of the Rock” inaheshimiwa na Waislamu kwa kuwa imejengwa katika eneo hilo linalotambulika kuwa ni eneo la tatu takatifu katika Uislamu baada ya Mecca and Medina. Katika eneo hilo ndipo Wayahudi wanapotaka kujenga hekalu la tatu! Asomaye na afahamu!

Maandalizi ya kujenga hekalu la tatu katika eneo hilo “almost” yamekamilika. Kilichokuwa kinasubiriwa zaidi ni ndama wekundu(red heifers). Kulingana na Torati (Hesabu 19:2-10), ndama mwekundu anahitajika kwa ajili ya ibada ya utakaso wa kuhani kabla ya huduma kuanza katika hekalu.

Waisraeli wengi bado hawaamini kuwa Yesu Kristo aliyekuja takriban miaka 2000 iliyopita ndiye Masihi wao. Sababu kuu ni kwamba walitarajia Masihi atakayewakomboa kisiasa na kuwarudishia ufalme wa Daudi (Yohana 6:15, Luka 24:21). Yesu, badala yake, alikuja kama Masihi wa kiroho, kuleta msamaha wa dhambi na wokovu kwa kila aaminiye(Yn 3:16). Kwahiyo kwa Waisraeli wengi, Masihi waliyemtarajia bado hajaja. Lakini kwa sasa wanaamini kuwa anakaribia kuja kutokana na ishara wanazoziona.

Ingawa Waisraeli wengi kwa sasa hawaamini kwamba Yesu aliyekuja ndiye Masihi, Mungu atawakomboa sawasawa na Warumi 11:25-26.
"Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msijue siri hii, msije mkajiona wenye akili; ya kwamba ugumu kwa sehemu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa utakapowasili. Hivyo Israeli wote wataokolewa, kama ilivyoandikwa, Mkombozi atatoka Sayuni, atamwondolea Yakobo maasia yake." (Warumi 11:25-26). Andiko hili linahusiana na unabii wa Isaya 59:20-21, unaosema: "Mkombozi atakuja Sayuni, kwa wale wa Yakobo waachao maasi yao, asema Bwana." Pia, Nabii Zekaria katika Zek 12:10 anatabiri kuwa siku inakuja ambapo Waisraeli watamtambua Yesu kuwa ni Masihi wao: "Nami nitamimina roho ya neema na kuomba...juu ya wenyeji wa Yerusalemu; nao watamtazama yeye waliyemchoma, nao watamwombolezea..."

Kwa Wakristo, maandalizi hayo ni dalili muhimu za nyakati za mwisho kama alivyotabiri Yesu. Kwa hiyo, tunapaswa kuwa macho na kujiandaa kiroho kwa ujio wa Bwana wetu Yesu Kristo. Mungu atusaidie tukeshe kama wale wanawali watano wenye busara(Mt 25:1-13). Amen.
Kwa habari zaidi tazama:
View: https://youtu.be/Puh80LhMJiY?si=9Bz9ygu0Mm0T0l-C

Pole sana ndugu
kumbe na wewe unautarajia mwisho ,
hauna tofauti na wayahudi sasa
 
Wanaemuomgelea hapo ni Yesu huyo huyo, Kwa wali kiroho wanaelewa Trump hajachaguliwa tu km watu wanavyodhani ,Mungu Yuko kazini Ili baadhi ya nabii zitimie sio coincidence
Trump it's a sign to this end times..
Hata ye kutumika kuufanya Jerusalem kuwa makao makuu watu wanafikiria imetokea tu !
No ana ana assignment ukiacha mambo yao ya siasa

Hapo ni sehemu qmbayo hawa wapuuzi walipora wakajenga mavitu yao SS itarudi kwa wahusika na patajenfwa hekaou la 3 ,ila muda Bado ni maandalizi ti hayo
Pole sana
 
Kama unakubaliana nao basi Yesu akija na wewe utaachwa.
Petro katika Matendo 4:11-12 aliwaambia viongozi wa Kiyahudi kuwa walimkataa Yesu, ambaye ndiye Jiwe Kuu la pembeni na wokovu pekee.
"Yeye ndiye jiwe lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni. Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote; kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo."

Yesu aliponya maelfu ya wagonjwa, vipofu waliona, viwete walitembea, mabubu waliongea kwa uwezo wake. Alifufua wafu, alibariki mikate michache na samaki wachache akawalisha maelfu. Alibadili maji yakawa divai. Alikufa akafufuka. Mambo mazito yote hayo yafanywe na tapeli?

Anyway, watakuja kutambua kuwa waliyemsulibisha ndiye Masihi.
Zekaria 12:10
Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.
Ataachwa kwenda wapi mkuu
 
Hujasoma 1 Petro 4:7? Imeandikwa hivi:
"Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia; basi iweni na akili, mkeshe katika sala."
Huo mwisho anaouongelea Petro nenda kasome tena kwa upya Mathayo 24 au Luka 21
ukiuelewa huo unabii wa Yesu ndiyo utamuelewa Petro na nyaraka zingine za mitume

Matthew 16v27-28
Kwasababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake ,ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadri ya matendo yake

Amin nawaambieni Pana watu katika hawa wasimamao hapa ambao hawataonja mauti kabisa hata watakapomuona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake

Marko 8v38 Marko 9v1
Luka 9v26
Ufunuo 1v7

Na hayo yote yalikuwa yanaihusu Yerusalem na kubomwoshwa kwa hekalu na kukomesha ibada za kiyahudi kwa mujibu wa TORATI ya Musa na kuleta Mamlaka ya Kristo Duniani
 
ukiielewa hi utakuwa Setfree kweli kweli
 
Back
Top Bottom