G
Maombi ya Amida(Amida prayer) ni sehemu muhimu ya sala ya Wayahudi. Sala au maombi hayo hufanyika mara tatu kwa siku watu wakiwa wamesimama kuelekea Yerusalemu. Maneno yafuatayo yamo katika sala hiyo. Ni maneno ya kumuomba Masihi aje Yerusalemu aishi katika mji huo kama alivyoahidi na afanikishe ujenzi wa hekalu la tatu upesi na kuweka kiti cha enzi cha Daudi:
הַשֵּׁב שְׁכִינָתְךָ לְצִיּוֹן עִירֶךָ, וְתִבְנֶה אוֹתָהּ בְּקָרוֹב בְּיָמֵינוּ בִּנְיַן עוֹלָם, וְכִסֵּא דָוִד מְהֵרָה לְתוֹכָהּ תָּכִין.
(Transliteration):
"Hashiv Shekhinat’cha l’Tziyon irekha, v’tivneha b’karov b’yameinu binyan olam, v’kisei David meheira l’tocha tachin."
Return in mercy to Your city, Jerusalem, and dwell therein as You have promised. Rebuild it soon in our days as an everlasting structure, and speedily set up in it the throne of David
View attachment 3276599
Wayahudi wakisali maombi ya Amida
Pole wewe mkuuPole sana
Sasa wewe jamaa huyo Trump anaingiajje kwenye nabii kuhusu wayahudiPole wewe mkuu
Maana mnadandia msiyoyajua Kila kiti mnafikiri kinatokea tu
Mkidhani judaisim na christian ni tofauti 😂
Yesu yuaja upesi kuwanyakua waliotubu dhambi zao na kuwapeleka mbinguni. Wasioamini wataachwa hapahapa duniani katika dhiki kuu.Ataachwa kwenda wapi mkuu
Sasa akiwachukua atatumia usafiri gani mpaka huko anapowapeleka ...?!Yesu yuaja upesi kuwanyakua waliotubu dhambi zao na kuwapeleka mbinguni. Wasioamini wataachwa hapahapa duniani katika dhiki kuu.
1Thes 4:13-18
"Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Maana, ikiwa tunaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa tunawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele..."
Nikiona mtu anaongelea huu upuuzi namdharau sana. Kwahiyo kwa akili zako hekalu likijengwa Mungu anarudi kukaa kwenye hema moja yaani Mungu anaacha kupatikana kwa wote eti anakua anapatikana kwenye kachumba kamoja hapo Jerusalem? Na unakuta washirika wanapiga makofiUjenzi wa hekalu la tatu ni hatua muhimu sana kwa Waisraeli katika maandalizi ya kumpokea Masihi wao. Kwa imani ya Wayahudi, ni lazima kwanza wajenge hekalu la tatu kabla ya ujio wa Masihi wao na kwamba hekalu hilo litarudisha ibada ya dhabihu na uwepo wa Mungu katikati yao, kama ilivyokuwa zamani. Je hekalu la tatu litajengwa katika eneo gani Israeli? 'Tega masikio' kwa makini.
Why not, acha wajiandae na Messiah wao. Wayahudi wa israel wanaamini Yesu alikua tapeli na muongo
Labda imani yao iko sahihi 🙌.
Mjinga wewe unayetaka kubishia imani za watu wengine.Mjinga wewe
Ndugu yangu kama unaamini ibada itakuwa rohoni, hiyo dharau kwa ndugu yako inatoka wapi?. Hujui kwamba amdharauye mwenzake afanya dhambi? (Mithali 14:21).Nikiona mtu anaongelea huu upuuzi namdharau sana. Kwahiyo kwa akili zako hekalu likijengwa Mungu anarudi kukaa kwenye hema moja yaani Mungu anaacha kupatikana kwa wote eti anakua anapatikana kwenye kachumba kamoja hapo Jerusalem? Na unakuta washirika wanapiga makofi
Ulishaambiwa saa inakuja..... ibada itakua rohoni hayo ya mahekalu ni kujazana ujinga tu.
Sasa ujinga wao wa kudhani Mungu ataacha kukaa rohoni mwa watu aje kukaa kwenye kachumba inahusiana nini na ujio wa Yesu??Ndio sababu wanajiandaa kujenga hekalu la tatu, kwa sababu kulingana na Agano la Kale, Mungu alikuwa anakaa hekaluni. Kujengwa kwa hekalu la tatu ni ishara muhimu sana ya ujio wa Yesu.
Kujengwa kwa hekalu la tatu Israeli ni jambo muhimu sana kuhusiana na timeline ya mambo yatakayotokea duniani kabla na baada ya ujio wa Yesu. Soma uzi huu uzingatie zaidi point no. 7Sasa ujinga wao wa kudhani Mungu ataacha kukaa rohoni mwa watu aje kukaa kwenye kachumba inahusiana nini na ujio wa Yesu??
Maana pazia la hekalu lilishachanika kitambo tu ndio maana siku hizi tunaomba tu moja kwa moja hatutegemei kuhani au kuchinja ndama!!
Ila sasa huu ujinga wa kusema sijui ndama mwekundu, sijui hekalu litajengwa hauingii akilini.
Acheni kupotosha watu, Yesu atakuja tu abruptly wala msidanganywe mkawa mnasubiri hekalu, biblia ni lugha ya mafumbo sana
Hekalu kujengwa ndio ina maana gani sasa? Kuhani mkuu ni Yesu sasa hapo kuhani atakua nani na ilihali pazia lilishachanika miaka kibao!!Kujengwa kwa hekalu la tatu Israeli ni jambo muhimu sana kuhusiana na timeline ya mambo yatakayotokea duniani kabla na baada ya ujio wa Yesu. Soma uzi huu uzingatie zaidi point no. 7
Yajue mambo mazito yatakayotokea wakati Yesu atakapokuja
Heshima zenu wakuu. Leo nawaletea mpangilio(timeline) au mtiririko wa mambo mazito sana yatakayotokea Yesu atakapokuja. Maandalizi yanayofanyika nchini Israeli, ya kujenga hekalu la tatu, ni ushahidi wa wazi kuwa Yesu amekaribia kuja...www.jamiiforums.com