Trump alipa fadhila kwa Putin. Uchaguzi wa awamu ya kwanza uliomwingiza Trump kwenye Urais kwa mara ya kwanza, alisaidiwa na KGB ya Russia katika kufanya udukuzi wa wapinzani wake. Na hiyo ilikuwa taarifa rasmi ya CIA. Who knows, kama msaada uliishia kwenye udukuzi pekee?
Wakati wa kampeni za safari hii, Ulaya ilionekana wazi kutopenda Trump awe Rais wa Marekani, bahati hailuwa kwao, Trump kashinda, huku akijua wazi kuwa Ulaya haikumtaka. Na inaonekana Trump ni mtu wa visasi, wote ambao hawakywa upande wake, anataka kuwakomoa. Fuatilia hata kule USA, wakuu mbalimbali ambao walionekana kuunga mkono USA kuipatia misaada na silaha Ukraine, wote amewaondoa, akianzia na mkuu wa majeshi. Na baada ya Ukraine kumkatalia takwa lake la kuvuna madini yote ya nchini mwake, Trump anatafuta njia ya kuiadhibu Ukraine.