Donald Trump ni deal maker hakuna ubishani,Mafanikio Yake ni makubwa kibiashara na siasa kwa Sasa.Ndani ya Miaka ya Urais amefanya makubwa kuliko mtangulizi wake Obama.Nlichojifunza ni kwamba kwenye forum hii wengi tunabisha ila hatuna fact wala atufatilii
Nawe fact gani uliyotoa kuprove kwamba amefanya makubwa kuliko Obama? Kama huuoni ubaguzi unaoongoza hizo dhidi ya people of color in general na Obama in particular, ngoja nielezee kidogo.
One thing is clear: mambo ya ufidhuli aliyoyafanya Trump, angefanya Obama, angekuwa jela na hata uraisi asingeupata.
-kwanza kabisa chaos ya White House ambayo inajidhihirisha kwa nje kwa jinsi watu wanavyofukuzwa au kujiuzulu au kufuatwa na mkono wa serikali na mikashifa kibao.
-kaoa mara tatu, na amecheat na wote hao. Tena hii moja na porn star. Imagine kama Obama angefanya hivyo. Kwanza wangesema watu weusi wote ni sex maniac.
-kaanzisha Trump University ikagunduliwa kuwa ni feki na haikusajiliwa (kesi bado inaendelea)
-alitamba kwamba he could grab p**** bila kupata shida yoyote.
-anasema uongo kila siku: ya sasa, kwamba hakumfukuza Comey kwa sababu ya Russia issue. Lakini alisema hivyo mwenyewe alipohojiwa na Lester Holt. Majuzi alidai kuna "deep state" ndani ya Justice Dept na FBI kwamba waliweka spy kwenye kampeni yake na akaiita spygate. Uchunguzi wa Congress umeonesha wazi kwamba huo ni uzushi.
-anadai anaweza kujipa msamaha (mnakumbuka jinsi ambavyo Obama aliitwa dikteta na FoxNews?)
-alidai anataka ku 'drain the swamp' akimaanisha kuondoa influence ya politicians wa muda mrefu, lobbysts and big money kama Wallstreet. . Lakini sasa angalia baraza lake la mawaziri: S. Mnuchin (Treasury) kutoka Goldman Sachs (Wallstreet), J. Sessions (Justice) mwanasiasa wa miongo mingi ana background ya KKK. T. Price (Health, aliondoka baadae) alikuwa exec wa Lilly (Big Pharma). Betsy DeVos (Education) ana biashara kubwa ya kukusanya madeni ya mikopo ya wanafunzi. Kakake anaitwa Eric Prince mmiliki wa kampuni ya mamluki ya Blackwater. Siwezi kuendelea na listi ndefu mno.
-Alijaribu sana kuua sera ya afya kwa wote ya Obama, bado anakusudia kufanya hivyo kwani anataka tu kufuta legacy ya hasimu wake.
-Je, umefuatilia ongezeka la mauaji ya halaiki Marekani? Nani wanaoua hivyo. Na raisi anasema nini kuhusu jambo hilo? Yeye kashikilia kwamba wahamiaji ni animals?
-Mashamba mengi yamekosa wafanyakazi hivi karibu na kusababisha hasara kubwa kwa sababu wanazuia wafanyakazi wa msimu kutoka Central America.
Nisikuchoshe, ningeweza kuandika zaidi. Hoja yangu, watu tusimeze madai ya Trump na wapenzi wao wenye siasa zilizonjekwa kwa misingi ya kiubaguzi.