Rais tunaomba usikilize vilio vya watanzania, mfumuko wa bei ni mkubwa mno

YEYE MWENYEWE ZAIDI YA MARA TATU KACHOCHEA HILO LA BEI KUPANDA KWENYE HOTUBA ZAKE UNATRAJIA AONGEE NINI? NI KAMA ANAFURAHIA VILE WATU WAKITESEKA WAKATI KULE KWAO ZANZIBARA WANAHANGAIKA VYAKULA VISIPANDE SIJUI TUNAKOMOLEWA TULIMKOSEA NINI HUYU MAMA?
 
Wapandisha hadi maji ya kunywa kutoka 1000 hadi 1500, 3500 hadi 4000 cjui tunaelekea wapi huku mishahara ikiwa ile ile kiduchu
 
Si bora DRC ni Waziri tuu ,kule Sri Lanka Baraza Zima la Mawaziri limejiuzulu,Ghana Rais na Mawaziri wamepunguziana malipo lakini unfortunately hakuna bei hata moja iliyopungua.

Swali la kufahamu ni kwamba uchumi wa Dunia wote unakabiliwa na mfumuko wa Bei,sio swala la Samia.

Mwisho serikali haiwezi kuvuruga bajeti yake Ili iweke ruzuku sijui kwenye vitu au ifute Kodi.Ikifanya hivyo itajiendeshaje? Itakwama na hutokuta hata panado hospital..

Kitu pekee serikali inaweza kufanya ni kujitahidi tuu kupunguza Kodi kwa baadhi ya maeneo,bahati nzuri hapa Tzn kinachoitwa mfumuko wa bei Kiko chini kuliko Nchi karibu zote zinazotuzunguka..

Hapo Kenya mafuta yameadimika sasa sijui ikifika huku mafuta hakuna itakuaje.

Uingereza wanasema mafuta ya alizeti yanaweza kupotea wiki zikazo na bei iko juu,kwa hiyo hili sio swala la Serikali bali ni swala la kufunga mikanda kwa kila mtu na kupunguza matumizi.

Bei zimepanda kwa sababu demand ni kubwa kuliko uzalishaji,sasa nyie mlitakaje?
 
Tanzania hapa kila kitu ni kusifia hata ujinga.

Bunge letu limekosa mamlaka ya kisheria kuchukua hatua mbalimbali kurekebisha mambo ya ajabu.

Ngoja tusubiri na tuone mwisho wake, japo tutakuwa tumechoka tukisubiri muafaka.
Leta suluhisho sio kuharisha ujinga hapa,Bei zimepanda Tzn tuu?
 
watanzania wapi unatusemea, kwa upande wangu maisha yamekuwa mepesi sana nyakati za mhe. SSH ukilinganisha na dikteta uchwara
 
watanzania wapi unatusemea, kwa upande wangu maisha yamekuwa mepesi sana nyakati za mhe. SSH ukilinganisha na dikteta uchwara
Hata mimi au uliza hata mafundi,Bora mfumuko wa bei uwepo lakini pesa iwe inapatikana.

Turkey kule mfumuko wa bei uko karibu 40% tena toka mwaka Jana na maisha yanaendelea.
 
Reactions: PhD
Wapandisha hadi maji ya kunywa kutoka 1000 hadi 1500, 3500 hadi 4000 cjui tunaelekea wapi huku mishahara ikiwa ile ile kiduchu
Ubunifu walioweza kuufanya ni kuweka tozo kila pahala ili wakamue akiba za wanyonge, watu tunalimwa VAT kutoa pesa kwenye akaunti ya akiba na hapo hapo ukienda kununua bidhaa na huduma unalimwa VAT. Mwarobaini wa yote haya ni katiba mpya, huwezi kumwapisha mtu awe rais kwa miaka minne wakati hakuchaguliwa na wananchi kwenye hiyo nafasi.​
 
Kwa kukusaidia ni hivi ;
CCM hakuna ushauri ambao wataweza kuuchukua isipokuwa ule tu utakaofanya waendelee kutawala.
Hii mada hapa ni kama changamsha genge tu
 
Tozo hazijaenda kuliwa bali kufanya Kazi na Matokeo ya tozo ndio haya hapa sasa 👇









 

Ukiona bei kubwa ujue ni Bei ya Soko , kwenye Dunia ya ushindani huwezi kujipandishia,wewe kama una duka hebu jipandiehie tuone.
 
Kwa kukusaidia ni hivi ;
CCM hakuna ushauri ambao wataweza kuuchukua isipokuwa ule tu utakaofanya waendelee kutawala.
Hii mada hapa ni kama changamsha genge tu
Mtoa mada ametoa ushauri gani zaidi ya kulaumu na kulalamika kama Kawaida ya Watzn?

Nimemuuliza baada ya Bunge kusema Waziri ajiuzulu vitu vimeshuka bei? Hajanijibu hadi saizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…