Rais tunaomba usikilize vilio vya watanzania, mfumuko wa bei ni mkubwa mno

Hebu tuongee ukweli huu mfumuko wa bei uko tanzania pekee?,huu mfumuko kauleta samia?na kwamba huo mfumuko samia unataka afanye nini?
Yani hujui kiongozi na selikali yake anapaswa kufanya nini, sasa tunawaweka madarakani kwa ajili gani?bro inaonekana huu mjadala sio saizi yako, au kuna uwezekano pia bado unatimiziwa mahitaji ndiomana huwezi kuona madhara yoyote kwa upande wako.
 
Sio swala la ccm,ukiacha South Africa na Egypt,Nchi zingine zote za Africa ziko ulimwengu wa tatu..
Nchi nyingine zote za Afrika kuwa katika ulimwengu wa tatu haihalalishi uzembe wa serikali ya CCM kushindwa kuiletea maendeleo Tanzania wala kuipa CCM hifadhi katika uzembe huo.Kwa hiyo sisi kama Taifa tuache kujishughulisha ili tutoke katika nchi za ulimwengu wa tatu kisa nchi nyingi duniani zipo katika ulimwengu wa tatu?
Kwani kote huko ni CCM imetawala? Kwani ni Tzn pekee iliyozidiwa na Korea Kusini? South Korea imeizidi hadi Russia sijui unasemaje..
Again,nchi nyingi duniani kuzidiwa na south Korea katika maendeleo haihalalishi uzembe wa CCM katika kuiletea Tanzania maendeleo na wala haiwezi kuipa CCM hifadhi katika uzembe wao.Kwa hiyo sisi kama Taifa tuache kujishughulisha ili kuwa sawa na Korea ya kusini au kuipita Korea ya kusini kisa nchi nyingi duniani zimepitwa na Korea ya Kusini?
Bara la Africa iliko Tanzania inakabiliwa na limitations nyingi,ingekuwa Tzn pekee ndio iko third world country na Nchi zingine za Africa zimejikwamua ingekuwa ni hoja ya maana..
Hakuna nchi ambayo haijawahi kuwa na limitations nyingi,hata nchi ambazo sasa hivi zipo katika ulimwengu wa kwanza zilikuwa na limitations nyingi pia ila zikajikwamua.Kisingizio unacholeta hakina maana bali ni chaka la kuficha na kutafuta hifadhi ya uzembe wa CCM.TZ kutokuwa katika third country peke yake haiwezi kuhalalisha Tanzania kuwa it is OK kuwa katika third countries.Kwa hiyo tulale usingizi wa pono katika masuala ya maendeleo kisa siyo sisi peke yetu tupo katika nchi za ulimwengu wa tatu?
Ulipo hapo huna hata mbinu hata moja ya kuiweka mezani Ili tutoke hapa umeishia kulaumu ccm kwa sababu tuu hujapata madaraka unayoyahangaikia.
Hizo ni hisia zako mfu kwa sababu huna ushahidi kuwa sina mbinu za kuikwamua nchi hii.Nailaumu CCM kwa sababu imetawala Taifa hili kwa miaka sitini bila ya kutuvusha.
 
Kwa upande wa sisi wananchi tumeshajibana mpaka mwisho ndiomana vilio vimeanza.Selikali inawajibu wa kutoa majibu ya vitendawili vya wananchi kwani ndio tuliyoipa dhamana ya kusimamia mambo haya.
Binafsi nategemea selikali kupitia wizara au taasisi husika zikitoa majibu ya namna ipi ya kukabiliana na crisis hiyo na sio kushabikia vita na kuacha wafanyabiashara wakijipangia bei watakavyo.
 
Mbinu huna ndio maana kutwa kucha kulaumu na kutukana,toka nimekufahamu hujawahi kuja na ushauri wowote zaidi ya matusi na kulaumu.Hii inadhihirisha huna huo uwezo..

Serikali ya CCM imejitahidi kukabiliana na changamoto lukuki ndio maana Leo hii mahali tulipo sio sawa na mwaka 1961..kwa mantiki hiyo hakuna uzembe.

Ukweli unabakia pale pale kwamba gari ya tairi nne haiwezi kwenda kwa speed inayotakiwa ikiwa mojawapo ya tairi imepata shida,hivyo hivyo Kwa Tzn sio kisiwa kama majirani mnaotakiwa kushirikiana hamko pamoja haiwezekani wewe kufika unakotaka..

Nchi ilikuwa kwenye vita na Uganda,Nchi ilikuwa inahigadhi wakimbizi wa Nchi jirani,Nchi ilikuwa inatoa mafunzo na kupeleka askari kufanya ukombozi wa Nchi jirani na Nchi ilikuwa haina wataalamu wa kutosha kwenye fani zote ilipopata uhuru achilia mbali wanachi kuwa wajinga..

Wananchi ndio wanaleta maendeleo ya Nchi na sio Nchi kuwaletea wananchi maendeleo,hii dhana haipo kazinya serikali ninkuweka mazingira wezeshi sasa ukikaa hapo unashindia kiporo unasubiri serikali ikuletee maendeleo utasubiria Sana,unresponsible citizen
 
Mkuu fanyeni juu chini mzuie, Leo raisi kakiri Tanzania ni maskini.
 
Mkuu fanyeni juu chini mzuie, Leo raisi kakiri Tanzania ni maskini.
Lini hiyo Tzn uliwahi kuwa tajiri? Kuzuia ni kuzalisha au kuwa na ziada..

Swala la kuzalisha sio la serikali ni la nyie ndio maana Rais kawaambia amewawekea mazingira mazuri hamtakuta ingieni kwenye kilimo tokeni mitandaoni kupiga domo

 
Hii dhana ya kudhani serikali ndio itawaletea maendeleo ni dhana mfu na ya hatari inayolea uzembe.

Serikali imeweka mazingira safi komaeni, yaani Kwa mfano tunazalisha 1/3 tuunya mafuta ya kula harafu kilochobaki tunaagiza na huko tunakoagiza kwa sasa yameadimika na yanapatikana kwa bei ghali badala mlime mchangamkie fursa mnalaumu serikali, yaani serikali ije iwalimie?

Hakuna aliyejibana kwa kiwango unachosema kwa sababu bidhaa nyingi hususani za chakula ambacho ndio muhimu bado bei ziko chini na affordable so msizushe mambo.
 
Uangaliege na watu wa kuwalilia. Magufuli alikuwa na roho mbaya ila alikuwa na huruma sometimes...
 
We jamaa unaongea nini!unazungumzia wananchi kuzalisha wakati pembejeo zilipanda bei kabla hata ya msimu kuanza matokeo yake wakulima wengi wameshindwa kumudu gharama za mboleo na kuathili uzalishaji. Hakuna aliyesema selikali itulimie na wala haijawahi kufanya hivyo, labda nikuulize ni mazingira yapi safi ambayo selikali imeyaweka kumuwezesha mkulima kufanikisha uzalishaji?
Yani nyanya mbili kwa sh.500/=
Nyama kilo sh.9000/= kutoka 7000/= wakati huo wafanyabiashara wananunua ng'ombe kutoka kwa wafugaji kwa bei ileile ya awali, na wewe upo hapa kudai bei za bidhaa ni affordable,bro! ni mwendawazimu tu ndio anaweza kuelewa unachojaribu kukitetea.
 
Wengine uwezo wa kununua chapati moja 500 tushasahau habari za chai sahizi tunakula mchana na usiku
 
Uangaliege na watu wa kuwalilia. Magufuli alikuwa na roho mbaya ila alikuwa na huruma sometimes...
Unakaribu kumdanganya nani labda? Pembejeo zimepanda kuanzia mwaka Jana kwa hiyo miaka yooote Nchi ilikuwa inajitosheleza? Nimekwambia over the years mafuta ya kula uzalishaji ni 1/3 tuu na hata hizo mbolea wala hazitumiki kwenye alizeti na Mazao mengine ya mafuta..

Huko kwenu kama nyanya 2 ni jero mkome kwa sababu kwetu fungu la nyanya bei ni 200-500 kutegemea wingi na ubora..

Nyama ni luxury sio lazima ule,kwanza kwenu huko ndio nyama ilikuwa 7000 sisi ilikuwa 3500-4500 sasa hivi ni 6000-7000 na bado zinaisha buchani..

Siokila kupanda Kwa bei kunaitwa mfumuko wa bei bali ni kupanda Kwa kawaida ndio maana bei za 2015 sio sawa na za 2020 na haziqezi kuwa sawa na za 2022..

Hivyo vitu vingekuwa havitoki ndio ungekuja hapa kusema kuna shida ila kama vinanunuliwa ujue havina athari zozote bali zinakuza uchumi ndio maana unaona mapato ya serikali yanaongezeka na shughuli za watu zinazidi kuongezeka..

Awamu ya 5 tulisikia maelfu ya biashara kufungwa licha ya Bei ndogo,vipi saizi umesikia biashara ngapi zimefungwa?
 
Ungekuwa umewahi kuuza hata vitumbua ungefahamu wafanyabiasha wanatumia vigezo gani kupanga bei za bidhaa. Tanzania ndio mmojawapo ya nchi za kibepari zilizobaki ambazo serikali inaangilia sana biashara ya sekta binafsi ikiwemo kutoa miongozo ya bei. Hili ni jambo baya sana kwenye uchumi wa soko.
 
Njia nyepesi ya kumfanya mtu aliyeficha mafuta nyumbani ayatoe mafichoni ni serikali kuruhusu mafuta mengi kutoka nje, sio polisi kukimbizana na wafanyabiashara kama panya Road. Usipewe ushirikiano wowote.
 
Nchi hii hii Tanzania. Shida mpo wengi mnaotetea hata upuuzi. Rais kauli zake zimechangia kupanda kwa bidhaa. Wafanyabiashara wakubwa wa Tanzania nadhan huwajui vizuri. Hata kama imeadimika sio hivyo unavyodhan. Na usifikirie kila anayeposti anaikosoa Serikali kakaa kizembe. Mimi nina kazi yangu nimejiajili. Kwenye ukwel lazima tuseme hii nchi ya watanzania wote sio wachache wanemeeke tu
 
umemjibu vyema kabisa tatizo la nchi yetu lipo kwetu wenyewe badala ya kuwa wamoja kukataa upuuzi wa watu kuna majitu yapo tu kwa ajili kutetea ujinga ilmradi buku 7000 amelipwa
 
Sijamaanisha unavyofikiria. Kwa bei za bidhaa hasa za Msingi wafanyabiashara wanapanga wenyewe bila mlaji wa mwisho. Nafanya pia biashara ila nimeathirika pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…