Rais tunaomba usikilize vilio vya watanzania, mfumuko wa bei ni mkubwa mno

hahahhahah eti unashindia kiporo
 
 
sio kuomba sema tunamtaka afanye hivyo ni wajibu wake na anapaswa kuwa hivo. Kuombwa ndio kuna mfanya ajisikie Mungu
 
Hakika, mambo yanaenda kiholela sana...
 
Harafu hapa Tzn watu mnadeka Sana,yaani bei zinazolalamikiwa ni ndogo Sana kulinganisha na Nchi zote za EAC.

Kwamba Rais ndio kapandisha bei kwa sababu kawaambia kwamba Bei zitapanda sio? πŸ˜„πŸ˜„ Idiot..

Narudia kukufundisha biashara ni ya ushindani na hakuna mwenye monopoly kwa hiyo ukipandisha tunakimbia.

Narudia pandisha bei hata hapo kwako afu tuone kama utauza shida iko wapi?

Kasome hii article ya BBC itakusaidia πŸ‘‡

 
Leo nimeenda kununua Tambi za MO ambazo zilikua zinauzwa 1200 Leo wameniambia 1600 nikatoka nduki... Dah kwakweli Mama anafail pakubwa sana kwenye kuzuia mfumuko wa bei.. Jioni hii petrol imeongezwa hadi 2900 hadi 3000 kuanza keshokutwa maana yake nauli lazima itapanda, bei ya vitu nayo itapanda dah naiona nchi yangu ipo kwenye free fall 9.8g/s... Naona km Waziri mkuu kaamua kumuachia liNchi lijiendee linavyoweza lenyewe... Kufikia December Thamani ya shilingi yetu itashuka sana uku bei yakila bidhaa ikiwa haikamatiki..
By December this yr
1KSh =30Tsh mark my words
 
Ikiwa huku ambapo vita haipiganwi na ni mbali kwa kiasi chake na kunakopiganwa vita kupo namna hii vipi huko kwenye vita kwenyewe kuna hali gani ?
 
Tanganyika tunahitaji uhuru wetu, tunahitaji mabadiliko makubwa ya ki utawala na katiba.
 



Mfumuko wa bei ni janga la Dunia sio Tanzania. USA imetoka 2% mpaka 6.8% hivyo jitihada zinafanyika Dunia nzima. Vita ya Urusi nayo ni tatizo hasa kwenye mafuta na bei ya ngano
 
Huu ni uhuni,jaribu kufikiria ndoo ya mafuta ya lita 20 ilikuwa sh.60000/-hivi sasa ni sh.140000/-ongezeko la sh.80000/-kweli hii ni sawa?
 
Shida yako umekalia hiyo unayofikiria, fanya utafiti mdogo utagundua bidhaa nyingi zimepaa bei. Nikuulize wewe hizo bodhaa zinatoka Urusi na Ukraine
 
Shida yako umekalia hiyo unayofikiria, fanya utafiti mdogo utagundua bidhaa nyingi zimepaa bei. Nikuulize wewe hizo bodhaa zinatoka Urusi na Ukraine
Sasa wewe umeelewa nilichoandika? Nani kasema bei hazijapanda? Suala nalozingua ni kwamba kupanda Kwa bei sio kwa kuita mfumuko wa bei.
 
Waziri wa fedha ni Mwigulu nchemba unatarajia nini?
 
Punguzeni ujinga wa uchumi. Mafuta yakipanda bei, kila kitu kitapanda bei. Hata bidhaa zinazozalishwa nchini, hata chakula kinachotoka nchini kitapanda bei. Ng'ombe wanafugwa mikoani, wanaletwa Dar kuchinjwa lazima mafuta yatumike. Mafuta ndiyo damu ya uchumi, yakiongezeka bei au yakiadimika yanagusa kila kitu.
 
Hebu tuongee ukweli huu mfumuko wa bei uko tanzania pekee?,huu mfumuko kauleta samia?na kwamba huo mfumuko samia unataka afanye nini?
Hii nchi mbumbumbu ni wengi sana, yani kila kitu lawama ni serikali, mfumuko wa bei ni dunia nzima na ni effect ya covid maana viwanda vingi vilifungwa na kwa kiasi vita ya Urusi.

Nchi tajiri wanatoa ruzuku kupunguza mfumuko kupunguza mfumuko wa bei, sasa tujiulize nchi za ulimwengu wa tatu zina uwezo huo?

Kwa mfano tukisema tupunguze kodi kwenye ushuru wa forodha ili bidhaa kama mafuta nk viingie kwa bei chini, serikali itakosa mapato kwa kiasi kikubwa sana, inaweza kushindwa hata kufanya matumizi ya kawaida kama kulipa mishahara nk

Bado kama nchi hatujafika kwenye viwango vya kutegemea kodi za ndani kama ilivyo nchi zilizoendelea, customs duties ndio zinaendesha nchi hii.

Huo ni ukweli mchungu ambao Mama Samia huwa anausema kama ulivyo na sisi tunakasirika, lakini hakitabadilika kitu, tujifunze kuogelea kwenye mawimbi
 
Acha upumbavu wewe Kenyata, Kagame wanajaribu kusubsidize mambo ili kusaidia wananchi siyo kuwapiga vijembe ,askini huku ukisisitiza bei lazima ipande mara tatu kwenye hotuba yake anasisitiza wakati kule zanzibar wanahangaika bei ya vyakula isipande au wao wanatumia mafuta gani?
 
Serikali inapo subsidize vitu inatumia hela. Bei ya mafuta inategemea na soko la dunia kwa hiyo serikali iki subsidize mafuta inalipa tofauti. Sasa hiyo hela iko wapi Tanzania? Mmeng'ang'ania siasa za Ujamaa na Kujitegemea miaka 60 leo uchumi hoi. Halafu hali ikiwabana mnaanza kupiga kelele.
 
Unakomaa na visingizio pamoja na excuses wakati majirani wanaokoa watu waoπŸ’πŸ’πŸ’
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…