Rais Uhuru aongoza marais kumi wa Afrika katika kupigia debe dawa ya Madagascar

Ohio,wazee wa vaccine, mlisema hamtumii miti shamba hiyo ni kazi ya Kinjekitile,mmeona mabwana zenu hawawatumii mmeamua kuju kiafrika?karibu kwenye mitishamba sisi tulikuwepo natunaendelea.Kenya wajinga sana! Jinga kabisa.
 
Safi sana! Hata kama ikitokea dawa hii haina mafanikio makubwa, ni jambo jema sana kwa Maraisi wetu Africa kupata ujasiri wa kufanya mambo yao bila kusubiri 'go ahead' toka kwa nchi za magharibi. Nimemsikia Rais wangu Magufuli leo akisema atatuma ndege Madagascar kwenda kuleta dawa. Ingependeza sana kama viongozi hawa wangetenga fungu la haraka kwa ajili ya utafiti wa kina juu ya chanjo au dawa ya Corona.
 
Ohio,wazee wa vaccine, mlisema hamtumii miti shamba hiyo ni kazi ya Kinjekitile,mmeona mabwana zenu hawawatumii mmeamua kuju kiafrika?karibu kwenye mitishamba sisi tulikuwepo natunaendelea.Kenya wajinga sana! Jinga kabisa.
Shida unaitana wajinga na mko busy kuzikana usiku wa manane,relook into your stupidity

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wako hadi na mganga mkuu wa taifa! 😂 😂 duh!
 
Ni vizuri kama mpaka Uhururu pia ameichukua... Lakini pia ingekuwa ni vizuri zaidi kama wangeishauri WHO iongoze kuifanyia research ili kama inamadhara ijulikane na sio kuipinga tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Marais wote hao ni wapumbavu tu!Hao marais wameshaifanyia majaribio hiyo dawa na kujiridhisha nayo wao kama wao?Mad presidents of Africa!
 
Baada ya Babu wa kikombe wa Loliondo sasa Babu wa chupa wa Madagasca! Kumbukeni huyu Rais Rajoelina wa Madagascar alikuwa DJ kabla ya kuingia madarakani.
Ila kuna kitu hawa jamaa wanafanya poa. We should borrow a leaf. Hamna vifo kwake. Labda ni kweli hii dawa inaponya.
 
Wazungu wamechanganyikiwa Waafrica tumewaharibia dili lao la kutunza vaccination
 
Shida unaitana wajinga na mko busy kuzikana usiku wa manane,relook into your stupidity

Sent using Jamii Forums mobile app
Eti aongoza marais Africa, hivi nyinyi wakenya mbona mnajiona mna akili sana wakati ni watu wa kawaida tu,hivi mentality, za kikoloni zitawatoka lini,mnawaona waafrika wenzenu ni 2nd class, inasikitisha sana.hii dawa ya Madagascar iliagizwa na nchi ya DRC Kwanza baadae nchi za Afrika magharibi zikafuata,alafu nchi yetu za EAC,ikiwemo Kenya.Na kwa hili swala la Corona, tungenyamaza Kwanza kwa sababu, Corona is here to stay,msijitape na mass testing na curfew, nakuhakikishia,kuna watu wataibika hapa EAC mda si mrefu.
 
This is what ails the Afrcan continent. We are stuck in the stone age. Tunaenda shule lakini haitusaidii.

What research has been done?
Whats the active ingridient?
How does it affect the virus?
Wafanye proper research, wafanye clinical trials wafanye patent, mass production alaf wapige hela. Ila kufanya vitu kienyeji kienyeji hivi kunapotezea Africa mapato na heshima.
Naona kikombe cha babu loliondo kimerudi tena!
 
Habari hii inanikumbusha kikombe cha babu huko loliondo. watu walikufa kwa mamia wamefuata upepo! sisi waafrika wakati mwingine huwa watu aina yake. mie ni nimehitimu na degree mbili. moja ni BSC horticulture-Egerton Kenya, na pili nikajiunga na chuo kimoja marekani na kutunukiwa associate degree in biotechnology 2019. hili ni baada ya kufanya kazi kenya kwa miaka kadhaa na kuingia masomoni tena baadaye 2016/2017. Kwa sasa najitayarisha kuingia masomo ya Masters japo sijaamua niegemee phamaceutical au agribiotechnology kwa sababu ya somo langu la hapo awali in horticulture. Lakini bahari la biotech ni pana nitafika tu!

Nirudi kwa mada, kutengeza dawa ya kutumiwa na umma upitia stage nne/tano kwa muda wa kama miaka saba kwenda kumi na kugarimu mamilioni ya fedha!
Drug Development Phases
  • Phase 1: Discovery and Development.
  • Phase 2: Preclinical Research.
  • Phase 3: Clinical Research.
  • Phase 4: FDA Review.
  • Phase 5: FDA Post-Market Safety Monitoring.
Sisi wafrika na kwingine mabara yenye umaskini wa kiwango cha juu tunakubali chochote mradi tu kinatupea tumaini bila kuuliza maswali nyeti. kwa mfano dawa imetengezwa na ni nini/active igredient? imepitia majaribio gani kudhibitisha usalama kwa binadamu. ilifanyiwa majaribio kwa binadamu au la? Na kama imepitia utafiti huru kando na madai ya mvumbuzi? La muhimau zaidi imechukua muda gani kiutafiti ata kama ni dawa ya kiasili!!

Mwisho, vidudu vya virus havina dawa. kwa mfano ukimwi (HIV ni retrovirus(RNA) hii ni baadhi yapingamizi kuu kwa kupata chanjo/dawa-somo la siku nyingina hilo) magojwa yote yanayotokana na virus uwa ni chanjo kutumika kujikinga. vidudu vya virus ni vigumu kuwangamiza kwa sababu unawili ndani ya vidudu vingine sana sana bacteria wanaowatumia kuendeleza uzao wao. Ni vigumu kuwalenga ili kuwaua.

Kama madagascar kuna dawa ya kuua virusi vya corona, tutashukuru wa lakini ninashauku kubwa. Naomba tu isiwe ni Kikombe chaa Loliondo chapter 2 ndani ya Malagasy yaani Madagascar!
 
Kumbuka pia watu asymptomatic yaani hawana dalili za corona japo wana ugojwa wanapona ata bila ufahamu waliugua COVID-19. Kwa hivyo bila utafiti wa kina, hauwezi kutoa vibitisho dawa hii ndio kaponya hawa wagojwa!

katika jiji la chelsea, MA ambalo ni jirani yangu walikwenda kwa street na kuomba volunteers watoe damu kupimwa corona (antibody test) pasipo kutambulishwa. Asilimia 33 ya samples waligunduliwa kuugua corona na kupona pasipo wao kuhisi wagonjwa kamwe!

Na kwa taarifa yako ukiwa ni mtu na afya zako na hauna shinda za kiafya zinazokusumbua, kuugwa corona ni faida kubwa. Unapata anti-bodies kwa jina memory B cells ambazo udumu kwa mwili hadi kufa kwa mtu.hizi unapata baada ya maambukizi ya virusi. Na ndio kazi ya chanjo. Wanakutia mwilini vidudu vya ukambi na kupelekea mwili kugenerate antibodies (memory B cell) halafu kingi ya ukambi unaipata. virusi vya ukambi vikishambulia tena memory B cells wanakumbuka maumbile ya antigen za ukambi na kuziangamiza!
 

Binafsi nakiri kwamba mimi sio mtaalam wa haya mambo hivyo siwezi nikawa msaada sana kwenye kuchangia, ila ninachofahamu ni kwamba hao marais kumi wana kundi kubwa la wataalam nyuma yao wanaowashauri, kwa mfano rais wa Afrika Kusini anaongoza taifa lenye wataalam wa kuaminika, hivyo wote hawa haiwezekani wakawa wanajikanganya.

Yaani kabla yao kuipigia dawa upatu lazima kuna namna fulani wataalam wao wamelijadili hili suala na kufikia hayo maamuzi, ingekua yanasemwa na rais mmoja tungedhani labda ni ukaidi wake tu anakurupuka au anatafuta uungwaji mikono kwenye mwaka wa uchaguzi, lakini wote kumi, inatia dukuduku fulani.

Anyway tusubiri tuone mwisho wake, virusi kweli havina dawa ila tumeona watu wanatibiwa UKIMWI kwa kutumia ARV mpaka wanapima tena na kirusi kutoonekana kwenye damu, japo hajapona kabisa lakini kirusi kinalemazwa kabisa.
 
Nakumbaliana na wewe juu ya marais kuwa na makundi makubwa kiutaalamu lakini kumbuka focus ni hilo kombe la babu chapter 2.

Wapi data za development, trials na nakadhalika! Most of the drugs za ARV huwa haziui virusi vya HIV moja kwa moja mbali ni blockers katika stages tofauti tofauti katika reproduction au division kwa virusi! kwa njia hizi zinapunguza kwa sehemu kuwa HIV kuenea mwilini na namba zake kupungua kama ulivyosema.

Kwa hivyo inawezekana pia kwa Corona japo changamoto kubwa ya corona ni respiratory virus. compare with a flu virus. Hata chanjo ikipatikana inawezekana utahitaji kurudi kila mwaka au baada ya muda fulani kwa marudio. reason- virusi vya maambukizi kupitia njia ya mfereji wa kupumua ni vigumu kupata immunity kikamilivu yaani ata kuamkukiza corana, wale Memory B cells (anti-bodies) itakua temporary immunity. Na hii ndio sababu south korea wanapata watu wanapata maambukizi mara ya pili COVI-19.
 

Kikombe cha babu hakikuidhinishwa na kiongozi yeyote nje ya Tanzania, kawaida unajua Tanzania wataalam wao huwa wapo wapo tu bila msaada wowote, hawana uwezo wowote wa kuhoji chochote, na ndio maana hata rais wao leo hii anataja vitu vya kiajabu kuhusu Corona huku wataalam wakikunja mikia na kumsifia bila kumhoji.

Lakini hii ya Madagascar imetengenezwa na Malagasy Institute of Applied Research kwa kushirikiana na National Pharmacology Research Centre ina maana hizi taasisi zinaweza zikaboronga bila kumakinika, humo hamna wataalam wa kueleweka?

Mimi nashauri wataalam wa Afrika waungane na hao wa Madagascar na kuwekeza nguvu zao humo mpaka kieleweke kimoja.

Hii Corona nimeona kila mtu anaibuka na mbinu zake alizotumia kuimaliza, ukipitia Youtube utaona watu waliopona wanatolea mbinu zao, kunao wanasema walitumia chai ya rangi yenye ndimu, wengine maji moto kila baada ya dakika kumi na tano, yaani mbinu nyingi tu, hivyo hiki kitu kuna namna ya kukimaliza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…