Kikabila ndio nini hicho, fahamu sisi Wakenya tunajivunia uwezo wa kuongea lugha nyingi zikiwemo zetu za jadi, hatujatekwa akili kama mambumbumbu kuongea lugha moja kama watu wasio na asili. Wanasayansi wametoa utafiti unaodhihirisha kwa mtu kutumia lugha zaidi kunamfanya anaboreka hata kiakili, na hii ndio imetufanya Wakenya kuwa wajanja.
Tunazo redio zinazoongea lugha nyingi, lugha zetu za asili za Kiafrika, tunazo zinazoongea lugha za kubuniwa kama Kingereza na Kiswahili pia. Watoto wetu huwa tunawahamasisha kujifunza kuongea lugha kadhaa. Nimesema hapa mara nyingi kuwa mimi binafsi watoto wangu wanaongea lugha yangu ya asili pamoja na ya kwa kina mke wangu, pia wanaongea Kingereza, Kiswahili na wanajifunza hadi Kifaransa shuleni, na juzi nilishangaa sana kuona wanawasiliana wenyewe kwa wenyewe wakitumia lugha ya ishara bila kuongea, kumbe wanafunzwa tayari shuleni.
Kizazi cha sasa kinataka mjanja wa lugha sio kilaza umekomalia lugha moja na hata hiyo lugha yenyewe bado unaandika uharo, haujaimudu inavyofaa.