Rais Uhuru awatangazia Kenya kutegemea mabadiliko makubwa karibuni: Makamu wa Rais Ruto anaondolewa? Odinga anarudishwa Serikalini?

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Raisi Uhuru amewatangazia Kenya kwamba muda wowote watasikia mabadiliko makubwa yakitangazwa. Wengine watafurahi, wengine watakasirika, wengine wataumia, na labda yatakuwa ni makosa, lakini lazima nchi iende kwa kubadilika. Na Raisi huyu ameyasema haya baada ya Raila Odinga naye kutamka maneno kama hayo siku kadhaa zilizopita.

Ikumbukwe kwamba baada ya shubiri ya uchaguzi wa Kenya iliyokua na mtifuano mkubwa kati ya Uhuru na Odinga, wawili hawa walifanya makubaliano ya amani na kushikana mkono na kuwa marafiki wanaoshirikiana kwa faida ya Kenya (fikiria Magufuli na Mbowe wawe marafiki kuiendesha nchi).

Ilifikia hadi Uhuru kupeleka jina la Odinga AU ili kuwa mwenyekiti wa AU nadhani (Magufuli apeleke jina la Mbowe, thubutu!)

Sasa watu wanajiuliza, haya mabadiliko yanahusu nini? Je, Ruto ataondolewa kama Makamu wa Rais, kwa kuwa amekuwa na tuhuma nyingi za kufanya kampeni za uraisi mapema, kukigawa chama chake na hata rushwa. Je, Odinga atarudi serikalilini?

Haya, tutajulishana. Ngoja tusubiri. Labda kuna jambo Watanzania (au Magufuli wetu) tutajifunza kutoka Kenya.
 
Ile ziara walienda wote nilisema anamuandaa Odinga kuwa Rais ajae
Ndoto yake itatimia kwani fikiria Uhuru bado umri unamruhusu sasa akimaliza mda wake akacheze karata?
Hapo natabiri tu kwa ndoto Uhuru atakuwa Waziri Mkuu (ajira mpya)
Na Raila President au mnaonaje jirani zetu
 
Anataka akiondoka amkabidhi Odinga madeni na mengineyo kwa Amani 😁😁
 
Anataka akiondoka amkabidhi Odinga madeni na mengineyo kwa Amani [emoji16][emoji16]
Aende wapi haondoki huyu na sasa anawaanda kisaikolojia [emoji23][emoji23]
Madeni atasema kwani nilikopa kununua kuku zangu [emoji23][emoji23]
 
Ila Uhuru anakuwa rais Wa mfano aisee
 
Wenzetu wapo vizuri, hawana roho za korosho
 
Huwezi kumlinganisha Uhuru na Magufuli. I remember to have said it here sometime that both guys come from different historical backgrounds.

The guys have different mentality and attitude. When one believes in consensus as the way of reaching decisions, the other one believes in coercion and bullying to achieve his goals.

When one favours dialogue and tolerance as the approaches to dealing with his political opponents the other guy prefers intimidation and repression as political tools to crush the opposition.

So the two have vividly contrasting character that keeps them miles apart.
 
Kama alivyofanya Raisi Putin wakati ule.
 
Sidhani kama SIZONJE anweza jifunza kitu kwa roho yake mbaya alonayo !!!! Bravo Kenya hakika mko juuu......
 
Na wametoka kwenye maisha tofauti kabisa
Uhuru amelelewa kutoka katika familia ya utawala tangu babu yake
Ameandaliwa tangu Mtoto
 
Hkuna kitu inafanyika isikuwe na madhara kwa jamii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…