Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Raisi Uhuru amewatangazia Kenya kwamba muda wowote watasikia mabadiliko makubwa yakitangazwa. Wengine watafurahi, wengine watakasirika, wengine wataumia, na labda yatakuwa ni makosa, lakini lazima nchi iende kwa kubadilika. Na Raisi huyu ameyasema haya baada ya Raila Odinga naye kutamka maneno kama hayo siku kadhaa zilizopita.
Ikumbukwe kwamba baada ya shubiri ya uchaguzi wa Kenya iliyokua na mtifuano mkubwa kati ya Uhuru na Odinga, wawili hawa walifanya makubaliano ya amani na kushikana mkono na kuwa marafiki wanaoshirikiana kwa faida ya Kenya (fikiria Magufuli na Mbowe wawe marafiki kuiendesha nchi).
Ilifikia hadi Uhuru kupeleka jina la Odinga AU ili kuwa mwenyekiti wa AU nadhani (Magufuli apeleke jina la Mbowe, thubutu!)
Sasa watu wanajiuliza, haya mabadiliko yanahusu nini? Je, Ruto ataondolewa kama Makamu wa Rais, kwa kuwa amekuwa na tuhuma nyingi za kufanya kampeni za uraisi mapema, kukigawa chama chake na hata rushwa. Je, Odinga atarudi serikalilini?
Haya, tutajulishana. Ngoja tusubiri. Labda kuna jambo Watanzania (au Magufuli wetu) tutajifunza kutoka Kenya.