JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametunukiwa Tuzo ya Uongozi Bora wa Mageuzi pamoja na Wakenya wengine saba katika hafla Kongamano la Tuzo za Sekta ya Umma Afrika (APSCA) liliyofanyika Accra, Ghana.
Waandalizi wa hafla hiyo walisema kuwa Rais Uhuru alituzwa kwa uthabiti wake wa kutoa uongozi wa mabadiliko katika mwaka uliopita.
Mbali na kuongoza Kenya, anahudumu kama Mwenyekiti wa Mkutano wa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na pia mkuu wa Ushirikiano wa Viongozi wa Afrika Kupambana na Malaria(ALMA).
Muungano huo ni unawaleta pamoja viongozi wa Afrika wanaoendeleza mradi wa uhamasishaji wa rasilimali na uwajibikaji katika makabiliano dhidi ya Ugonjwa wa Malaria kote barani Afrika.
Chini ya uongozi wake, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza kuwa chanjo ya kwanza ya Malaria Duniani ilikuwa tayari Oktoba 2021. Kenya ilitangazwa kuwa mojawapo ya nchi tatu za Afrika zilizopendekezwa kutumia chanjo hiyo.
Wakenya wengine waliotuzwa ni Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya Kenya Power, Rosemary Oduor ambaye alipewa Tuzo ya Mwanamke Bora katika Nguvu.
Mkuu wa Benki Kuu ya Kenya, Patrick Njoroge na Mkurugenzi Mkuu Msimamizi wa Shirika la Ndege la Kenya Allan Kilavuka pia walitajwa miongoni mwa viongozi 50 Bora wa Sekta ya Umma barani Afrika.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kitaifa ya Usimamizi wa Mazingira Mamo Mamo pia alitajwa kuwa kiongozi bora barani katika kitengo cha mazingira.
Chanzo: Tuko