Hapo shida siyo hiyo IEBC wapinzani wote akili zao zinafanana ni ndogo, hapo ni zaidi ya hiyo Tume na utaona hata kama hiyo Tume ikiondolewa watakuja na demands nyingine mpya na hilo Raisi
Uhuru Kenya analijua, lengo la Raila ni kama alivyokuwa fisadi Lowasa anataka kuwa sehemu ya Serikali yaani anataka kama vile mwaka 2007/08 aidha awe Raisi wa Kenya au ikishindikana kabisa basi waunde Serikali ya mseto hicho ndicho kiko nyuma yake kwa maana wanajua kwamba kwa hali ya kawaida hawawezi kumshinda Uhuru Kenya kwa kuwa Wakikuyu ndiyo kundi kubwa Kenya, hivyo ni kwa hila tu ndiyo wanweza kushinda!
Hata hiyo Katiba mpya wengi hawawelewi lkn lengo lilikuwa ni hilo hilo kuvunja nguvu ya Wakikuyu ili Raila aweze kuwa Raisi kwa maana kwa kura peke yake hawezi, na ndiyo maana unaona mambo yalivyo kwenda ndivyo sivyo Raila huyo huyo ambaye ndiye champion wa Katiba mpya na aliyeshiriki kuunda hiyo Tume inayoitwa huru leo hii haitaki, na sababu wala siyo ufanisi wa hiyo Tume la hasha, bali sababu ni kwamba imeshindwa kumuingiza madarakani hawo ndiyo wanasiasa wetu ...
Huwa sielewi mbona unakua mkurupukaji hivi na kurusha maneno kiholela bila uelewa. Jamii ya Wakikuyu ni asilimia 22% ya wananchi wa Kenya. Hapo wapo hadi watoto na watu ambao hawana uwezo wa kupiga kura. Halafu kumbuka nchi imeongozwa kwa miaka 24 na mtu asiye na asilia ya Kikikuyu. Sasa hizo hesabu zako sijui huwa unazifanyia ndani ya choo ukinya ama vipi.
Vyama tanzu vinavyounda Jubilee na waliompigia kura rais Uhuru, vina wabunge hadi kule kwa Wasomali, Waturkana, Wakisii, Waluhya n.k.
Jubilee ina wabunge kule Kinango Kwale,GARSEN, TANA RIVER, TAVETA, Fafi GARISSA, Mandera n.k.
Muungano wa rais una wabunge 135 na wa upinzani una wabunge 117, sasa una maana Wakikuyu ndio hao waliowapigia wabunge 135 kura???????????
Hamna siku kabila moja linaweza kumchagua rais wa nchi Kenya. Lazima rais awe na ushawishi maeneo mengi ndio aweze kuibuka mshindi kwa mujibu wa katiba. Sasa hivi cha msingi ni amani, haijalishi nani atakua rais, bora aingie akiwa na sera za kuboresha nchi, rais Uhuru amesema mara kadhaa kwamba hawezi kuwa king'ang'anizi, akishindwa atakwenda kijijini kulima na hapo Kenya tuendelee.
Kwenye kampeni kila mtu atamnadi mgombea wake, lakini atakayeibuka mshindi tunaanza kumpa support papo hapo ili Kenya idumishe uongozi wake EAC kwenye uchumi, miundo mbinu, elimu na vyote. Binafsi nitamchukia mtu yeyote atakayethubutu kuirudisha nchi nyuma kwa vyovyote vile, hata hawa viongozi wa upinzani wanafaa kufahamu ni bora wakaachiwa nchi ikiwa salama na yenye maendeleo ndio waendeleze zaidi.
Rais Uhuru amesema siku zote yeye yupo radhi kwa mazungumzo yafanyike ya kurekebisha IEBC japo lazima yafanywe kisheria maana utaratibu upo kwenye katiba. Karudia hilo tena na kusema kwake yeye cha muhimu ni wapiga kura, maana hao ndio wenye uwezo wa kumpiga chini.