Katika hotuba yake (State of the Union addresss) aliyoitoa bungeni jana, Rais Uhuru Kenyatta amewaomba radhi wakenya wote aliowaudhi kwa matendo yake au matamshi yake wakati wa ucnaguzi mkuu uliopita ambao ulishuhudia mchuano mkali kati yake na Raila Odinga. Katika mchuano huo Mahakama ya Juu (Supreme Court) ilibatilisha matokeo ya uchaguzi uliofanyika Agosti 8, 2017 na kufanya uchaguzi huo kurudiwa Oktoba 26, 2017. Rais Kenyatta aliwaomba wakenya waungane na wawe kitu kimoja katika kujenga taifa. Je tunapata somo gani kwa Rais kuomba radhi wananchi wake?