Mganguzi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 1,604
- 3,715
Asalaam ndugu zangu..
Nianze kumpongeza Rais kwa kusikiliza hoja za watu wa kada mbalimbali hasa wa mlengo wa kisiasa wakidai katiba mpya. Wamesikilizwa, na ninasikia mchakato karibia utaanza. Ni jambo jema. Lakini tupo sisi ambao hatukubaliani na mchakato huo. Hatuhitaji katiba mpya na tuna hoja na sababu za msingi. Nchi yetu imekuwa na amani kwa miaka zaidi ya 50 kwa katiba hii. Nchi yetu imekuwa na uchumi unaokuwa vizuri kwa katiba hii.
Kwa sisi tusiotaka katiba, utatusikiliza lini? Na sisi tuna haki ya kusikilizwa kama ulivyowasikiliza hao wanaotaka katiba mpya! Mimi na wenzangu wengi tu tusiotaka katiba mpya, tutasikilizwa lini? Hatutaki kabisa katiba mpya! Tumeona nchi jirani zilizokimbilia katiba mpya kwa minajiri ya ustawi kisiasa na maisha ya watu wetu, lakini imekuwa kinyume chake!
Kenya vurugu tupu! Afrika Kusini vurugu tupu! Nchi zote zilizothubutu kubadilisha katiba ziliingia kwenye migogoro isiyoisha. Please, Rais, hakuna legacy yoyote utakayoiacha kwa kuleta katiba mpya zaidi ya fujo na vurugu.
Asanteni.
Pia soma: Serikali: Mchakato wa Katiba Mpya na maboresho ya Sheria ya vyama vya Siasa na Uchaguzi, sasa kuanza