Informer
JF-Expert Member
- Jul 29, 2006
- 1,606
- 6,672
Aliyemtangulia ni Mwalimu Julius Nyerere, na aliyemfuata ni Benjamin Mkapa.
Pia, Mwinyi alikuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzia 1990 hadi 1996.
Mzee Mwinyi aliwahi pia kuwa Rais wa Zanzibar, Makamu wa Rais na Waziri wa Mambo ya Ndani.
Wakati wa utawala wake wa mihula miwili, Mwinyi alichukuwa hatua za mwanzo kubadilisha sera za ujamaa za Mwalimu Nyerere. Alilegeza vikwazo vya manunuzi ya nje na kuhamasisha watu kuanzisha biashara.
Picha ya Rais iliyokuwa ikibandikwa katika ofisi wakati wa utawala wake
Ni katika muhula wake wa pili ambapo mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania ulianzishwa kufuatia shinikizo kutoka kwa wafadhili wa kigeni.
Akifahamika zaidi kama Mzee Ruksa (Kila kitu ruksa), aliwapa watu ruksa ya kufanya kile wakitakacho pasipo na kuvunja sheria.
Baada ya kustaafu, Mwinyi huonekana kwa nadra hadharani na anaendelea kuishi jijini Dar es Salaam.