Rais wa Awamu ya Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi afikisha miaka 95. Heri ya kuzaliwa Mzee Ruksa!

Rais wa Awamu ya Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi afikisha miaka 95. Heri ya kuzaliwa Mzee Ruksa!

ilikuwaje mpaka yeye ndie aonekane tena anafaa wakati taswira yake ni kama ilishachafuka kutokana na kujiuzulu kwake uwaziri wa Mambo ya Ndani.

Mliokula chumvi msaada tafadhali.
Mh! Unatushangaza sana Bw. Mdogo. Kwa hiyo kwa unavyoelewa wewe mtu akijiuzulu nyadhifa flan basi taswira yake imeshachafuka?? Huo ndio ufahamu wako?? !!
 
Huyu mzee ngoma ngumu sana
Mazoezi, Chakula bora na asili vimemsaidia sana

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
... naomba nitofautiane na wewe. Kuna wanaofanya mazoezi kuliko yeye; kuna wanaopata chakula bora na cha asili kuliko yeye lakini "zikifika zimefika". Ni kwa neema tu, yupo hivyo alivyo maana maisha marefu ni kitu ambacho mwanadamu aliyejaliwa hupewa bila kustahili. Na hiyo ndio maana halisi ya neema.
 
Ali Hassan Mwinyi (amezaliwa 8 Mei 1925) alikuwa Rais wa Pili wa Tanzania kuanzia 1985 hadi 1995.

Aliyemtangulia ni Mwalimu Julius Nyerere, na aliyemfuata ni Benjamin Mkapa.

Pia, Mwinyi alikuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzia 1990 hadi 1996.

Mzee Mwinyi aliwahi pia kuwa Rais wa Zanzibar, Makamu wa Rais na Waziri wa Mambo ya Ndani.

Wakati wa utawala wake wa mihula miwili, Mwinyi alichukuwa hatua za mwanzo kubadilisha sera za ujamaa za Mwalimu Nyerere. Alilegeza vikwazo vya manunuzi ya nje na kuhamasisha watu kuanzisha biashara.

View attachment 1443335
Picha ya Rais iliyokuwa ikibandikwa katika ofisi wakati wa utawala wake

Ni katika muhula wake wa pili ambapo mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania ulianzishwa kufuatia shinikizo kutoka kwa wafadhili wa kigeni.

Akifahamika zaidi kama Mzee Ruksa (Kila kitu ruksa), aliwapa watu ruksa ya kufanya kile wakitakacho pasipo na kuvunja sheria.

Baada ya kustaafu, Mwinyi huonekana kwa nadra hadharani na anaendelea kuishi jijini Dar es Salaam.
Mungu ampe maisha marefu yenye heri , Mzee wetu huyu hapendi shari kabisa
 
Allah akupe maisha marefu zaidi Mzee wetu Alhaji Ali H. Mwinyi
 
HBP Mwinyi, mwaka jana akizungumzia siri ya maisha yake ni kufurahi, kuto kukasirika, na kufanya mazoezi.

Alisema hata kama kutatokea jambo la kukukasirisha, usiliruhusu, samehe

Hata yule jamaa aliye wahigi kumpiga kibao, alimsamehe pale pale na kuwasisitiza wale jamaa wa usalama wamwache, ila jamaa walimngangania ili tuu kujiridhisha he was real insane and was acting alone na hajatumwa !.
P
Alikuja kukata moto nadhani haijapita miaka miwili, kijana kwao palikuwa manzese
 
Long live Babu Mwinyi,
Busara zako na Upendo ulionao ndio vinakufanya uzidi kunawiri,

Najivunia kukujua.

Boost your Immune System to fight a Covid-19.
 
HBP Mwinyi, mwaka jana akizungumzia siri ya maisha yake ni kufurahi, kuto kukasirika, na kufanya mazoezi.

Alisema hata kama kutatokea jambo la kukukasirisha, usiliruhusu, samehe

Hata yule jamaa aliye wahigi kumpiga kibao, alimsamehe pale pale na kuwasisitiza wale jamaa wa usalama wamwache, ila jamaa walimngangania ili tuu kujiridhisha he was real insane and was acting alone na hajatumwa !.
P
Ilikuaje akapigwa kibao? Mwaka gan?

Hii ya kutokukasirika ngumuu dah,kuna jamaa nimetoka kulifokea muda si mrefu hapa na nimekasirika kinoma.

Ngoja nilisamehe tu,papai hili.
 
HBP Mwinyi, mwaka jana akizungumzia siri ya maisha yake ni kufurahi, kuto kukasirika, na kufanya mazoezi.

Alisema hata kama kutatokea jambo la kukukasirisha, usiliruhusu, samehe

Hata yule jamaa aliye wahigi kumpiga kibao, alimsamehe pale pale na kuwasisitiza wale jamaa wa usalama wamwache, ila jamaa walimngangania ili tuu kujiridhisha he was real insane and was acting alone na hajatumwa !.
P
Yule jamaa japo alisamehewa ila alifungwa.
 
Duh! Na bado mzee yupo very strong.Mazoezi yanasaidia
 
Hongera sana Mzee mwinyi ,siku zote ukiwa na huruma na wenzako kama kiongozi utaishi maisha marefu maana Dua za heri zinakuwa nyingi.

Nakiri sijawahi kumsikia Mzee Mwinyi akiwadharau wananchi wake. Big up zako Mzee mwinyi.
Unamaanisha hajawahi kutuita "Malofa?" au enzi zake hajawahi kutishia kuwatandika "Shangazi zetu?"
 
Back
Top Bottom