Rais wa Awamu ya Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi afikisha miaka 95. Heri ya kuzaliwa Mzee Ruksa!

ilikuwaje mpaka yeye ndie aonekane tena anafaa wakati taswira yake ni kama ilishachafuka kutokana na kujiuzulu kwake uwaziri wa Mambo ya Ndani.

Mliokula chumvi msaada tafadhali.
Mh! Unatushangaza sana Bw. Mdogo. Kwa hiyo kwa unavyoelewa wewe mtu akijiuzulu nyadhifa flan basi taswira yake imeshachafuka?? Huo ndio ufahamu wako?? !!
 
Huyu mzee ngoma ngumu sana
Mazoezi, Chakula bora na asili vimemsaidia sana

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
... naomba nitofautiane na wewe. Kuna wanaofanya mazoezi kuliko yeye; kuna wanaopata chakula bora na cha asili kuliko yeye lakini "zikifika zimefika". Ni kwa neema tu, yupo hivyo alivyo maana maisha marefu ni kitu ambacho mwanadamu aliyejaliwa hupewa bila kustahili. Na hiyo ndio maana halisi ya neema.
 
Mungu ampe maisha marefu yenye heri , Mzee wetu huyu hapendi shari kabisa
 
Allah akupe maisha marefu zaidi Mzee wetu Alhaji Ali H. Mwinyi
 
Alikuja kukata moto nadhani haijapita miaka miwili, kijana kwao palikuwa manzese
 
Long live Babu Mwinyi,
Busara zako na Upendo ulionao ndio vinakufanya uzidi kunawiri,

Najivunia kukujua.

Boost your Immune System to fight a Covid-19.
 
Ilikuaje akapigwa kibao? Mwaka gan?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ya kutokukasirika ngumuu dah,kuna jamaa nimetoka kulifokea muda si mrefu hapa na nimekasirika kinoma.

Ngoja nilisamehe tu,papai hili.
 
Yule jamaa japo alisamehewa ila alifungwa.
 
Duh! Na bado mzee yupo very strong.Mazoezi yanasaidia
 
Hongera sana Mzee mwinyi ,siku zote ukiwa na huruma na wenzako kama kiongozi utaishi maisha marefu maana Dua za heri zinakuwa nyingi.

Nakiri sijawahi kumsikia Mzee Mwinyi akiwadharau wananchi wake. Big up zako Mzee mwinyi.
Unamaanisha hajawahi kutuita "Malofa?" au enzi zake hajawahi kutishia kuwatandika "Shangazi zetu?"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…