Hao bado ni vijana wadogo sana wana miaka 31 😆😆😆😆Mheshimiwa Mbwana na Mao wapunzike kwa amani kwenye timu zao, msiwasumbue tena na milele.
Endeleeni kuyaita hayo yenye uchuro na mikosi kina Samata wakati hawana faida yeyote na Timu.Tumefika hapo tulipofika kwa kuwatumia wachezaji wetu wa ndani akina Shemtembo, kwanini kocha alibadili gear angani akaacha kuwatumia? Wachezaji wa nje wana miguu ya pesa, wanawaza timu zao zinazowapa fedha.
Wachezaji wa ndani wanajituma sana ili waende kucheza nje, lakini wale wa nje hawajitumi sana kwenye timu zao ili waje kucheza ndani ya nchi zao.
Rais wa Brazil, Lula da Silva amewashtukia wachezaji wao wanaocheza Ulaya, hawataki kabisaa kwenye timu yake. Hawapambani kivileee kama kwenye timu zao.Endeleeni kuyaita hayo yenye uchuro na mikosi kina Samata wakati hawana faida yeyote na Timu.
Hahahahahaha...mie ninekuelewaMechi za nje zina mshawasha wake
Mechi za ndani zinakinaisha mapema
Kocha hapendi kuita mchezaji anaeweza kumpa changamoto ya kuhoji maamuzi ya mwl. Anataka wachezaji ambao anawaswaga tu, YES MEN. Dickson Job alijaribu kumpa challenge kocha akakiona cha mtemakuni. Wachezaji wa nje huwa wanahoji, sio wazuri, lakini wanawaza what if nitaumia hapa!!! TFF na seikali wanawaza posho zao na kugharamia safari na kaa yao kwenye timu ya taifa. TFF na makocha wazaa hawataki mtu anaehoji. Kocha anaehoji na asiyetaka kupangiwa timu na wachezaji hatakiwi kabisaa. Wanataka kocha anaechagua kwa kuangalia wangapi wanatoka Simba na wangapi wanatoka Yanga bila kuangalia mahitaji.Huyo mchezaji wa nje hata akicheza kwenye kiwango cha kawaida tu mchezaji wa ndani hawezi kumfikia.
Mtu anacheza na kina De Brune karibu kila wiki umfananishe na mtu anayecheza na Mbuni Fc.
Wabongo hatuna respect kabisa na wachezaji wa nje. Kule sio kwepesi asee.
Halafu siku ukivaa jezi ya Taifa na ukapoteza mechi utabadili mtazamo wako kwamba wachezaji hawajitumi. Tumekuwa watu wa lawama sana.
Ghana alidondosha point kwenye uwanja wa nyumbani kidogo wapigwe na mashabiki. Lakini hizi mechi mbili moja wamedroo nyingine wamefungwa.
Yaani pamoja na kutaka kupigwa lakini bado wamepoteza points? Unahisi hawakujituma ile yasitokee yale mambo?
Hakuna mchezaji anayependa kupoteza mechi hasa akiwa analiwakilisha Taifa lake. Samatta kuomba kustaafu timu ya Taifa sio kupenda. Ni vile anaona vile anavyojitoa kwa ajili ya Taifa lake halafu anaambulia matusi.
Na kingine mnajikuta nyie wakubwa sana. Kipa namba moja wa timu ya Taifa ni kipa namba tatu wa klabu yake. Foward line inaongozwa na mabench warmer. Halafu mnafungwa na timu iliyowazidi kila kitu mnaanza lawama.
Ushauri wangu, kocha aite wachezaji wanaopewa game time na wapo kwenye fomu huku wale wanaocheza nje akiwapa kipaumbele. I mean wale wanaocheza ligi za kueleweka mfano yule dogo Kelvin John anayecheza ligi kuu Denmark. Kuna yule Charles Mbomwa sijui yupo ligi kuu ya Australia na kuna bwana mdogo alikuwa ligi kuu ya Serbia somebody Morice. Team selection iangaliwe upya asee.
Ile timu kama watapewa Baresi na Ahmad Ally tungeona maajabu makubwa, wana jicho la kuona nani acheze na acheze vipi wakati gani. Ameongezeka kijana mmoja anaeitwa Muya wa Fountain gate.Yule Mzanzibar jeuri sana, hana kiwamgo cha kuwa kocha hata wa timu ya wanawake!
Mao dah....alii RIP Stars.Mheshimiwa Mbwana na Mao wapunzike kwa amani kwenye timu zao, msiwasumbue tena na milele.
Rais wa Brazil, Lula da Silva amewashtukia wachezaji wao wanaocheza Ulaya, hawataki kabisaa kwenye timu yake. Hawapambani kivileee kama kwenye timu zao.
Mchezaji kama Saidun, Sulemani Mwalimu, Waziri jr, Kibabage, Balua, Mzize, Kibwana, Kihimbwa, Andabwile unawaona kabisa wanavyopambana wakiwa uwanjani (do or die) lakini looo!!