Rais wa Brazil yuko sahihi, kwanini Waziri Jr Shemtembo hakucheza?

Rais wa Brazil yuko sahihi, kwanini Waziri Jr Shemtembo hakucheza?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Tumefika hapo tulipofika kwa kuwatumia wachezaji wetu wa ndani akina Shemtembo, kwanini kocha alibadili gear angani akaacha kuwatumia? Wachezaji wa nje wana miguu ya pesa, wanawaza timu zao zinazowapa fedha.

Wachezaji wa ndani wanajituma sana ili waende kucheza nje, lakini wale wa nje wanajituma sana kwenye timu zao ili wapate pesa zaidi na sio kwenda kucheza kwenye nchi zao nyumbani. Hii imegundulika kwa nchi nyingi duniani.
 
Tumefika hapo tulipofika kwa kuwatumia wachezaji wetu wa ndani akina Shemtembo, kwanini kocha alibadili gear angani akaacha kuwatumia? Wachezaji wa nje wana miguu ya pesa, wanawaza timu zao zinazowapa fedha.

Wachezaji wa ndani wanajituma sana ili waende kucheza nje, lakini wale wa nje hawajitumi sana kwenye timu zao ili waje kucheza ndani ya nchi zao.
Endeleeni kuyaita hayo yenye uchuro na mikosi kina Samata wakati hawana faida yeyote na Timu.
 
Endeleeni kuyaita hayo yenye uchuro na mikosi kina Samata wakati hawana faida yeyote na Timu.
Rais wa Brazil, Lula da Silva amewashtukia wachezaji wao wanaocheza Ulaya, hawataki kabisaa kwenye timu yake. Hawapambani kivileee kama kwenye timu zao.

Mchezaji kama Saidun, Sulemani Mwalimu, Waziri jr, Kibabage, Balua, Mzize, Kibwana, Kihimbwa, Andabwile unawaona kabisa wanavyopambana wakiwa uwanjani (do or die) lakini looo!!
 
Huyo mchezaji wa nje hata akicheza kwenye kiwango cha kawaida tu mchezaji wa ndani hawezi kumfikia.

Mtu anacheza na kina De Brune karibu kila wiki umfananishe na mtu anayecheza na Mbuni Fc.

Wabongo hatuna respect kabisa na wachezaji wa nje. Kule sio kwepesi asee.

Halafu siku ukivaa jezi ya Taifa na ukapoteza mechi utabadili mtazamo wako kwamba wachezaji hawajitumi. Tumekuwa watu wa lawama sana.

Ghana alidondosha point kwenye uwanja wa nyumbani kidogo wapigwe na mashabiki. Lakini hizi mechi mbili moja wamedroo nyingine wamefungwa.
Yaani pamoja na kutaka kupigwa lakini bado wamepoteza points? Unahisi hawakujituma ile yasitokee yale mambo?

Hakuna mchezaji anayependa kupoteza mechi hasa akiwa analiwakilisha Taifa lake. Samatta kuomba kustaafu timu ya Taifa sio kupenda. Ni vile anaona vile anavyojitoa kwa ajili ya Taifa lake halafu anaambulia matusi.

Na kingine mnajikuta nyie wakubwa sana. Kipa namba moja wa timu ya Taifa ni kipa namba tatu wa klabu yake. Foward line inaongozwa na mabench warmer. Halafu mnafungwa na timu iliyowazidi kila kitu mnaanza lawama.

Ushauri wangu, kocha aite wachezaji wanaopewa game time na wapo kwenye fomu huku wale wanaocheza nje akiwapa kipaumbele. I mean wale wanaocheza ligi za kueleweka mfano yule dogo Kelvin John anayecheza ligi kuu Denmark. Kuna yule Charles Mbomwa sijui yupo ligi kuu ya Australia na kuna bwana mdogo alikuwa ligi kuu ya Serbia somebody Morice. Team selection iangaliwe upya asee.
 
Kocha hapendi kuita mchezaji anaeweza kumpa changamoto ya kuhoji maamuzi ya mwl. Anataka wachezaji ambao anawaswaga tu, YES MEN. Dickson Job alijaribu kumpa challenge kocha akakiona cha mtemakuni. Wachezaji wa nje huwa wanahoji, sio wazuri, lakini wanawaza what if nitaumia hapa!!! TFF na seikali wanawaza posho zao na kugharamia safari na kaa yao kwenye timu ya taifa. TFF na makocha wazaa hawataki mtu anaehoji. Kocha anaehoji na asiyetaka kupangiwa timu na wachezaji hatakiwi kabisaa. Wanataka kocha anaechagua kwa kuangalia wangapi wanatoka Simba na wangapi wanatoka Yanga bila kuangalia mahitaji.
 
Yule Mzanzibar jeuri sana, hana kiwamgo cha kuwa kocha hata wa timu ya wanawake!
 
Yule Mzanzibar jeuri sana, hana kiwamgo cha kuwa kocha hata wa timu ya wanawake!
Ile timu kama watapewa Baresi na Ahmad Ally tungeona maajabu makubwa, wana jicho la kuona nani acheze na acheze vipi wakati gani. Ameongezeka kijana mmoja anaeitwa Muya wa Fountain gate.
 
Hii timu wangepewa hata AHMED ALLY na ALLY KAMWE sasa hivi ingekuwa inaongoza kwenye kundi, DRC angekuwa wa pili!
 
Wachezaji wanalihujumu hili taifa. Hawajitumi ipasavyo
 
Ndani mechi nje mechi cheza ndani cheza nje, chezea nje nje chezea ndani mechi ni wachezaji wazuri walioandaliwa kwa muda, jiulize tuna academy hata moja kubwa ya mpira? Hao wachezaji wazuri utatoa wapi? Malipo yao je? Ni duni sio, sasa usitegemee ushindi
 
Rais wa Brazil, Lula da Silva amewashtukia wachezaji wao wanaocheza Ulaya, hawataki kabisaa kwenye timu yake. Hawapambani kivileee kama kwenye timu zao.

Mchezaji kama Saidun, Sulemani Mwalimu, Waziri jr, Kibabage, Balua, Mzize, Kibwana, Kihimbwa, Andabwile unawaona kabisa wanavyopambana wakiwa uwanjani (do or die) lakini looo!!

Hujui mpira wewe, unabwabwaja tu

Congo DR wapo bora sana kwasbb kikosi chao kati ya wachezaji 24 ni wawili tu wanacheza ligi za África,, Inonga na Mayele (anayeanziaga benchi mechi nyingi) waliobaki 22 wote wanacheza Ulaya na Asia , quality ya wachezaji ipo juu kuliko sisi

Ukiangalia mataifa kama Nigeria, Senegal, Ivory Coast, Morroco, Cameroon wanatamba África ktk michuano ya Afcon na FIFA kwasbb wanabebwa na quality ya players wanaocheza Vilabu vya Ulaya
Huko wanapata exposure kubwa sana ya kiushindani, tough games, quality technical Managers (makocha) nk

Sisi Tz hawa local players wetu hata wajitume vp National team Kamwe hatuwezi kuja kutamba África kwa kutegemea wachezaji wetu wanaocheza ligi ya ndani África tena wengi NBCPL kwasbb ubora wa ligi yetu ipo chini kulinganisha na mataifa ya Ulaya, América na Asia

Angalia mpishano wa quality ktk hizi Sub mechi ya jana

Sub za Congo Dr
Meshack Elia (Young Boys fc, Switzerland)
Nathaniel Mbuku ( Dynamo Zagreb, Croatia)
Sadiki (Royale Unión, Belgium)
Mayele ( Pyramids, Egypt)

Sub Starz
Mwamnyeto (Yanga, anakaa benchi)
Selemani Mwalimu (Fountain Gate)
Himid ( El Gaish, Egypt)

Wakati huo huo Starz tumeacha Mapro wetu wengi wanaocheza ulaya & Asia: Kwesi Kawawa, Morrice Abraham, Charles Mmombwa, Msuva, Nova, Baraka Majogoro, Haji Mnoga nk
 
Samata asipokwepo tunashinda,akiitwa tu basi gundu tupu kazi kunyanyua makwapa na mabega uwanjani
 
Back
Top Bottom