Rais wa Burkina Faso Capt Ibrahimu Traore anatarajiwa kuja Tanzania January, 2025. Je, atatingisha jukwaa kama alivyofanya nchini Ghana?

Rais wa Burkina Faso Capt Ibrahimu Traore anatarajiwa kuja Tanzania January, 2025. Je, atatingisha jukwaa kama alivyofanya nchini Ghana?

Huku kapteni Traore ni muumini wa JPM
1737626115882.jpeg

Picha maktaba : Captain Traore akigonga salaamu.

Toka maktaba:​

Hili ndio baraza la mawaziri la Magufuli​

Sandu GeorgeDecember 10, 2015 - 2:38 pm
1 minute read
Magufuli.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli leo ametangaza baraza jipya la mawaziri katika serikali ya awamu ya tano.
20151210035203

Rais Magufuli amesema kuwa baadhi ya wizara hazitakuwa na manaibu waziri, Lengo likiwa ni kuwa na baraza dogo kupunguza gharama.
Hili ndio Baraza la Magufuli:

1. Ofisi ya Rais, Tamisemi Utumishi na Utawala Bora – Mawaziri: George Simbachawene, Angela Kairuki, Naibu: Selemani Jafo

2. Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira – Waziri: January Makamba, Naibu Waziri:Luhanga Mpina

3. Ofisi ya Waziri mkuu , Sera , Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu – Waziri:Jestina Muhagama, Manaibu: Dr Abdallah Possi, Anthony Mavunde
4.Kilimo, Mifugo na Uvuvi – Waziri: Mwigulu Nchemba, Naibu: William Nasha

5. Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano – Waziri: Bado hajapatikana, Naibu: Injin. Edwin Ngonyani

6. Fedha na Mipango: Waziri: Bado hajapatikana, Naibu: Ashantu Kizachi

7. Nishati na Madini – Waziri: Sospeter Muhongo, Naibu: Medalled Karemaligo

8. Katiba na Sheria – Waziri: Harrison Mwakyembe

9. Mambo ya nje, Afrika Mashariki – Waziri: Augustine Mahiga, Naibu: Suzan Kolimba

10. Ulinzi na jeshi la kujenga taifa – Waziri: Hussein Mwinyi

11. Mambo ya ndani – Waziri: Charles Kitwangwa

12. Ardhi nyumba na makazi – Waziri: William Lukuvi, Naibu: Angelina Mabula

13. Maliasili na Utalii – Waziri: Bado hajapatikana, Naibu:Ramol Makani

14. Viwanda na uwekezaji – Waziri : Charles Mwijage

15. Elimu, sayansi, Teknolojia na Ufundi – Waziri: Bado hajapatikana, Naibu:Inj. Stella Manyanya

16. Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto – Waziri: Ummy Mwalimu, Naibu:Hamis Kigwangala

17. Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo – Waziri: Nape Nnauye, Naibu: Anastasia Wambura

18. Maji na umwagiliaji: Waziri: Prof. Makame Mbarawa, Naibu: Isack Kamwela
 
My Take
Diplomasia ya Samia inazidi kuihwshimisha Nchi.

Kazi Iendelee 👇 👇

==
Rais wa mpito wa Bukina Faso, Capt. Ibrahim Traoré ni miongoni mwa marais 25 watakaoshiriki mkutano wa nishati uliopangwa kufanyika Dar es Salaam Januari 27 na 28 mwaka huu.

Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeshughulikia masuala ya nishati na mabadiliko ya hali ya hewa, Dk Kevin Kariuki amesema pia mawaziri wa fedha na nishati 60 wa Afrika watashiriki mkutano huo.
Aidha, viongozi wengine wa kimataifa watashuhudia wakuu wa nchi za Afrika wakikubaliana kusaini Mpango Mahususi wa Nishati wa Afrika, awamu ya kwanza utakaozishirikisha nchi 14. Nchi hizo ni Tanzania, Malawi, Chad, Nigeria, Burkina Faso, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Niger, Liberia, Msumbiji, Madagascar, Zambia, Mali, Ivory Coast na Mauritania.

Alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mkutano huo unadhaminiwa na Benki ya Dunia, AfDB na washirika wengine wa maendeleo kuhakikisha watu milioni 300 Afrika wanafikiwa na umeme ifikapo mwaka 2030.

Chanzo: HabariLeo
Tunataka viongozi wakubwa wenye mamlaka wa Marekani, Canada, Ulaya, Brazil, Korea Kusini, Indonesia, Vietnam Singapore na Israel ndio waje Tanzania. Tunahitaji teknolojia zaidi kuliko kupiga story na majirani tunaofanana.
 
Hapa kwetu hawezi kufanya hayo mambo, niliwahi kushuhudia Kagame na vijana wake walikuja na mbwembwe kama hizo Ikulu ya mwanza wakambiwa hii ni Nch! ya amani huo utaratibu wa kuonyesha siraha kwenye msafara wa vingozi sisi hatuutaki na waka tii sheria
 
Tunataka viongozi wakubwa wenye mamlaka wa Marekani, Canada, Ulaya, Brazil, Korea Kusini, Indonesia, Vietnam Singapore na Israel ndio waje Tanzania. Tunahitaji teknolojia zaidi kuliko kupiga story na majirani tunaofanana.
Kwani hawajakuja au unajisahaulisha?
 
Huyo dogo ana kipi jipya tofauti na harakati za kizamani za resource nationalism kama akina Mugabe ambazo hazina tija, Rasilimali kama huwezi kuzitumia ni bure hata kama ukizikumbatia
Kinachofanyika DRC kwa rasilimali zao ni sahihi au siyo sahihi?
 
Tofautisha uchaguzi wa golden standards na zile chaguzi za kihuni ulizozizoea
Replica ya Magu hiyo.

Safari hii mabeberu tunawapelekea moto mpaka msalimu amri.
 
Tunataka viongozi wakubwa wenye mamlaka wa Marekani, Canada, Ulaya, Brazil, Korea Kusini, Indonesia, Vietnam Singapore na Israel ndio waje Tanzania. Tunahitaji teknolojia zaidi kuliko kupiga story na majirani tunaofanana.
Nje ya mada ila ni kwa ajili ya tafakuri:
Uliona viongozi wa nchi ambazo Trump aliwaalika kwenye sherehe za uapisho wake? Wakubwa na traditional US allies wote hakuwaalika!!
 
Nje ya mada ila ni kwa ajili ya tafakuri:
Uliona viongozi wa nchi ambazo Trump aliwaalika kwenye sherehe za uapisho wake? Wakubwa na traditional US allies wote hakuwaalika!!
Kwanza ni vizuri ufahamu pia Trump ndio rais wa kwanza wa Marekani kualika viongozi wa nchi za nje katika uapisho wa Rais kwa mara ya kwanza katika historia ya Marekani. Sio utamaduni kwa marais wa Marekani kualika viongozi wa nje wakati wa uapisho.
 
What's so special about this young man..Hana jipya huyu jamaa
 
Traore amejizolea umaarufu mkubwa Duniani hasa kwa ulinzi wa rasilimali. Amekuwa na nguvu kubwa ya mapokezi kila anapokwenda. Amekuwa mwana mapinduzi anayetisha mabepari kwa misimamo yake.

Natambua Watanzania siyo wafuatiliaji wa siasa za nje, ila naamini ujio wa Traore ukifanyiwa matangazo vizuri nje ya nchi itakuwa sehemu yakitangaza nchi kiuchumi na kiutalii.

Katika mbinu za kuitangaza nchi tunayo kila sababu ya kuruhusu vyombo vyetu vya habari vifanye matangazo makubwa kuanzia mapokezi yake hadi hotuba zake.

Pia soma > Rais Ibrahim Traore wa Burkina Faso alikaa Jukwaa kuu na bunduki yake wakati wa uapisho wa Rais mpya wa Ghana

Tunapaswa kutumia fursa ya ujio wake kama njia ya kuifanya Duniani kufahamu ulinzi wa rasilimali zetu upo vipi na nini wafanye kuja kuwekeza.

Vyombo vya magharibi vitataka kumsikia anasema nini kuhusu nishati ! Vitataka kusikia anaeneza sumu gani kuwafanya waafrika wafikirie kujikomboa kwenye ukoloni Mamboleo. Fursa hii ina faida kwetu hasa pale tutakapounganisha matangazo ya nchi yetu na ujio wake.

Tunatakiwa kuitangaza Tanzania kwa kila opportunity tunayopata. Tuache kujifungia na ujamaa usio na tija. Chana wameweza na sasa wanajadiliwa Duniani kote, tutangaze nchi kibepari tuachane na ujamaa wakuabudi wazungu
eti duniani, nani anamjua? Siada za Africa —- strong man!
 
Back
Top Bottom