Rais wa Cameroon Paul Biya afanya Mkutano wa Kampeni yake ya kwanza, baada ya kutoonekana kwa muda mrefu

Rais wa Cameroon Paul Biya afanya Mkutano wa Kampeni yake ya kwanza, baada ya kutoonekana kwa muda mrefu

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Rais wa Cameroon mwenye umri wa miaka 92, Paul Biya, ameonekana hadharani Jumanne Oktoba 7, 2025 katika mkutano wake wa kwanza wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu ujao, ambapo kiongozi huyo mkongwe zaidi duniani anawania muhula wake wa nane madarakani

Akihutubia maelfu ya wafuasi katika uwanja wa michezo ulioko mjini Maroua, Kaskazini Mashariki mwa nchi, Biya aliahidi kuongeza usalama katika eneo hilo linalokumbwa na mashambulizi ya vikundi vya kigaidi, kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana, na kuboresha miundombinu ya barabara pamoja na huduma za kijamii endapo atachaguliwa tena katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 12, 2025

Mkutano huo ulikuwa wa kwanza kwa Biya tangu kuanza kwa kampeni, baada ya kutokuwepo kwa muda mrefu, huku akirudi hivi karibuni kutoka mapumziko ya wiki moja nchini Uswisi. Ingawa hakutoa maelezo rasmi kuhusu safari hiyo, imezoeleka kwamba kwa miaka ya karibuni Biya amekuwa akisafiri mara kwa mara Ulaya kwa mapumziko binafsi na matibabu

Rais huyo ambaye sasa huonekana hadharani mara chache, amekuwa akikosolewa vikali na wapinzani wanaodai kwamba umri wake mkubwa umeathiri uwezo wake wa kuongoza taifa


Soma pia



Source: African news
 
Back
Top Bottom