Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Rais wa Cameroon, Paul Biya (91) hajaonekana hadharani kwa zaidi ya siku 60, lakini bado anaendelea kutekeleza majukumu yake ya urais akiwa nje ya nchi. Hali hiyo imewafanya watu wengi kujiuliza kuhusu afya yake, mahali alipo na jinsi serikali inavyoendeshwa wakati kiongozi huyo haonekani hadharani.
Paul Biya ameendelea kutumia mamlaka yake ya urais. Amewapandisha vyeo makanali watano kuwa majenerali brigedia, amewateua maafisa katika nyadhifa muhimu za kijeshi, na kumteua tena Raymond Jean Charles Beko'o Abondo kuwa kamanda wa Kikosi Maalum cha Walinzi wa Rais nafasi ambayo ameishikilia tangu mwaka 2013.
Hii si mara ya kwanza. Biya amekuwa akiongoza Cameroon tangu mwaka 1982, na kutokuwepo kwake hadharani kwa muda mrefu kumekuwa kukizua mara kwa mara maswali na minong'ono kuhusu alipo na jinsi nchi hiyo inavyoongozwa.
Aidha, kwa mujibu wa Waziri wa Mawasiliano wa Cameroon, René Emmanuel Sadi amesema "Rais Biya yuko hai na atarejea nchini hivi karibuni."
Upinzani unasema kutoonekana kwa rais kwa muda mrefu kumeleta hali ya kutokuwa na uhakika. Makamu wa rais wa CRM, Mamadou Mota, anasema kwamba kutooneka hadharani kwa Biya kwa muda mrefu kumeacha "pengo kubwa la kiutawala" nchini Cameroon.
SOURCE: BBC Swahili