Rais wa Cameroon Paul Biya hajaonekana kwa siku 50 sasa. Wananchi wanataka kujua yuko wapi?

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Mjadala umeibuka nchini Cameroon baada ya Rais wa nchi hiyo, Paul Biya kutoonekana kwenye majukwaa mbalimbali na shughuli za kiserikali, huku taarifa rasmi iliyotolewa hivi karibuni ikielezwa yupo nchini Uswisi.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Serikali ya nchi hiyo ilieleza kuwa kiongozi huyo aliondoka nchini humo Juni 7, 2026 kwa ajili ya ziara fupi ya faragha akiwa ameambatana na mkewe ambapo mpaka sasa bado hajarejea.

Tovuti ya African News leo Julai 28, 2026, imeeleza kuwa hivi karibuni Rais Biya amekuwa akifanya safari za mara kwa mara kwenda Geneva. Biya mwenye miaka 93, ndiye mkuu wa nchi mwenye umri mkubwa zaidi duniani na amekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 40.

Afya yake imeendelea kuwa chanzo cha uvumi, huku Serikali ya Cameroon ikisisitiza kuwa yuko katika hali nzuri. Ikijibu taarifa zilizochapishwa mwezi Juni, Serikali ya Cameroon amekanusha madai kwamba rais huyo amelazwa hospitalini mjini Geneva.

Kwa upande mwingine, mwanasiasa wa upinzani, Mamadou Mota, ameeleza kuwa kutokuwapo kwa Biya nchini kumesababisha "pengo kubwa la kiutendaji katika taasisi za dola."

Soma Zaidi: Rais wa Cameroon Paul Biya afanya Mkutano wa Kampeni yake ya kwanza, baada ya kutoonekana kwa muda mrefu

Kiongozi wa Cameroon Democratic Union (UDC), Patricia Tomaino Njoya ameitoa wito kwa serikali kuweka wazi iwapo mkuu wa nchi amepoteza uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa muda au kwa kudumu. Hii siyo mara ya kwanza madai ya aina hiyo kutolewa. Mwishoni mwa mwaka 2024, Biya alikosolewa kutokana na kutokuwapo nchini humo kwa siku 50 mfululizo.

000-A7X96PZ.jpg

Source: Africa News
 
View attachment 3638674

Source: Africa News
Nakumbuka kipindi hayati Magufuli Kuna kipindi hakuonekana watu wakaanza kuuliza you wapi rais wa nchi.

Akaja Mr Katelefoni akasema huyo bwana mkubwa yupo ikulu maana haonekani hivyo kama anafanya kazi kariakoo
 
Enhee tayari huko! Yale yale. Hapo usalama wa nchi hiyo watamwambia boya mmoja aseme raisi yupo anaendelea na majukumu yake! 😊
 
Huyu raisesi ndiyo Anaishi maisha yake yote uswiss huyu?
 
Labda yuko Pariii. Kuna masonic lodges kule, ziliwaingiza sana mkenge wazee wa Francophone countries

Wanawapa mpaka mademu wa kizungu ili wajisikie kama wafaransa, huku ufaransa ikiendesha uchumi wake kwa kutumia nchi zao.
Halafu baadae tunaacha nyuma total damage
 
Back
Top Bottom